Kard.Czerny kwenye bandari ya Beirut,kukumbatiana na familia za wafiwa
Na Salvatore Cernuzio – Beirut.
Katika giza ambalo linaingia mapema kwenye bandari ya Beirut na kufunika korongo na moja ya maghala ambayo yalilipuka sana mnamo 2020, tabasamu zuri la Elias Khoury pekee ndilo linalojitokeza. Uso wa mvulana huyo, akiwa na umri wa miaka 15 mmoja wa wahanga vijana zaidi wa mkasa huo ulioshtua mji mkuu wa Lebanon, uliwekwa kwenye picha iliyoshikiliwa na mama yake Mireille yenye maneno Haki kwa Elias. "Angalia, anafanana na Carlo Acutis," alisema mwanamke huyo, alisogea, akikutana na Kardinali Michael Czerny tarehe 22 Februari, jioni akiwa katika ziara yake ya kitume tangu tarehe 19 hadi 23 Februari 2025 nchini Lebanon.
Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Kuhamasisha Maendeleo Fungamani ya Binadamu kwa hiyo akirejea kutoka vijiji vya kusini vilivyoharibiwa na mabomu ya Israel dhidi ya Hezbollah, baada ya zaidi ya saa mbili katika msongamano wa magari na pikipiki za wale waliofika mji mkuu kwa mazishi ya kiongozi wa kihistoria wa Harakati hiyo, Hassan Nasrallah - hakutaka kukosa kusimama Mashariki ya Kati na kuwa ishara ya maumivu ya Mashariki ya Kati. Ilikuwa ni muda mfupi wa kutua lakini ulioakisiwa na sala kwenye ukumbusho ambao kwenye ubao wa marumaru una majina ya waathiriwa zaidi ya 260 wa mlipuko wa Banadari na kukumbatiwa na baadhi ya ndugu na jamaa zao. Ikiwa ni pamoja na Mireille, kwa usahihi, ndiye pekee aliyekuwa ameshikilia picha ya mtoto wake ambaye, anaonekana na tabasamu safi, ambayo inamkubusha kweli kijana maarufu ambaye hivi karibuni atatangazwa mtakatifu (Carlo Acutis).
"Haki na Ukweli"
Wengine, hata hivyo, walimweleza Kardinali huyo kwa majina au walionesha kwenye simu zao picha tu za jamaa waliouawa katika mlipuko huo, ambao ulisababishwa, kulingana na mamlaka, na moto wa hifadhi kubwa ya mbolea yenye nitrati ya ammoniamu. Walikuwa, miongoni mwa wengine, Pierre Gemayel, aliyefiwa na kaka yake Yacoub, na wakili Cecile Roukoz, ambaye pia aliona kaka yake akifariki akiwa ameajiriwa katika kampuni ya meli, inayojulikana kwa kupigania "haki na ukweli". "Haki na ukweli", ndiyo: kilio ambacho familia zote za wafiwa na zaidi ya 7,000 waliojeruhiwa bandarini wamekuwa wakirudia kwa miaka mitano, katikati ya uchunguzi uliozuiliwa na kile wanachoita "uzuiaji."Ombi ambalo Papa pia alizindua katika moja ya mkutano na kiongozi wa Lebanon mjini Vatican mnamo Agosti 2024: "Pamoja nawe ninaomba ukweli na haki, ambao haujafika: ukweli na haki."
Mkutano na Papa mnamo 2024
“Tulitaka haki itendeke na tulifanya kila tuwezalo, lakini kwa kuwa kesi hiyo ilisitishwa, tulikwenda kukata rufaa kwenye Baraza la Haki za Binadamu kuanzisha uchunguzi wa kimataifa, ili angalau tujue ukweli. Huu ni uhalifu dhidi ya haki za binadamu! Hata hivyo, hatujapata uchunguzi wowote, ni taarifa tu,” Mireille Khoury aliviambia vyombo vya habari vya Vatican kando ya tukio hilo. Yeye si mwanamke anayeinua sauti yake, ambaye anatumia sauti kali; ni ombi la mama ambaye aliona mwanawe akitolewa kutoka kwake kutokana na majeraha aliyoyapata, baada ya siku za uangalizi maalum. Binti yake mkubwa, Nour, pia alilazimika kufanyiwa upasuaji kwenye mkono wake mmoja, na Mireille mwenyewe, aliyetupwa kutoka nyumbani kwake kwa nguvu ya mlipuko huo, aliumia mgongo na mbavu na akaachwa kwenye kiti cha magurudumu kwa muda mrefu. Lakini hakusema lolote kuhusu hilo wakati anasimulia. Lengo tu lilikuwa katika siku zijazo: "Uchunguzi sasa umeanza tena na, natumaini, utaendelea na serikali mpya na rais mpya." Alirudia pamoja na Cecile pia kwa Kardinali, ambaye alimkumbatia kila mmoja wa wale waliohudhuria na kutoa baraka zake.
Nyimbo na maombi
Hakukuwa na maneno kutoka kwa Kardinali, bali ilikuwa ni ukaribu, upole na sifa za Mungu zilizoombwa mara nyingi na Papa wakati wa maumivu. Kisha sala. Kardinali Czerny, akifuatana na mtawa mmoja Paolo Borgia, mapadre wengine na watu wa kujitolea, walikusanyika mbele ya ukumbusho. Padre mmoja aliimba “wimbo wa Pasaka” katika Kiarabu na kila mtu alisali sala ya Baba Yetu pamoja. Kisha kukumbatiana na misemo zaidi ilinong'ona faraghani. “Ziara ya Mwadhama ina thamani kubwa kwetu. Alikuwa mwenye kuunga mkono na mwenye fadhili na mwenye kuelewa,” familia za waathiriwa zilisema. "Uungwaji mkono wa Kanisa ni muhimu sana, kama ule wa Papa."Kardinali Czerny wakati akiondoka bandarini alisema: "Maumivu makubwa. Mchanganyiko wa janga la kibinafsi na kukataa kupata ukweli."
Mkutano na wahamiaji na wakimbizi
Mara tu baada ya hapo, Kardinali huyo alitembelea kituo cha Huduma ya Wakimbizi cha Kijesuit huko Beirut, si mbali na bandari, ambapo akikaribishwa na mseminari mdogo Mjesuit Michael Petro, aliyeitwa "ndugu" au "abuna" au "shujaa" kwa hiyo hapo alikutana na kundi la wahamiaji na wakimbizi zaidi ya 20. Wanawake na wanaume, vijana na wazee, walezi au wafanyakazi wa nyumbani wakati wa mchana, mara tu wanaharakati na viongozi wa jamii wanapotoka kazini ambao huwasaidia wenzao katika shida na pia Walebanon maskini na waliohamishwa. Wanatoka Ufilipino, Sudan Kusini, Ethiopia, India, Sri Lanka, Bangladesh. Hawa walikutana na Mwenyekiti wa Baraza la kipapa la Maendeleo Fungamani ya Binadamu na kushirikisha kazi zao, lakini zaidi juu ya vikwazo vyote vilivyokutana na kushinda katika miaka hii ya safari. Vikwazo vingi na shida nyingi. Hasa kwa wanawake, wanaokabiliwa na unyanyasaji wa kimwili, wajawazito baada ya dhuluma au wahasiriwa wa ubaguzi wa rangi na watu wa jamii zao kwa sababu tu ya kuwa na wanaume walioolewa wa mataifa mengine.
Mikataba ya uwongo, kazi ya utumwa, hakuna hati
Mariam, msichana kutoka Sierra Leone, kwa muda mrefu amekuwa akiripoti majanga yanayofanyiwa na jumuiya za kigeni, tangu kuondoka kwao kutoka katika nchi zao na "mawakala" ambao hutoa kazi na kuwafanya kusaini mikataba kwa Kiarabu, kifungu ambacho hakuna mtu anayeelewa. Mbali na hayo, malipo ya takriban dola elfu 3. Mara tu wanapofika Lebanon, hata hivyo, wahamiaji hukutana na "mabwana" ambao huwalazimisha kufanya kazi "kuanzia saa 3 asubuhu hadi usiku wa manane." Ikiwa wataomba kuondoka, wanatishwa au kuripotiwa kwa uhalifu ambao hawakuwahi kufanya, kama vile kuiba nyumbani. Kijana Sierra Leonean alieleza kuwa Wakijaribu kuondoka na kuwasiliana na mawakala, wanawaambia: Sawa, nirudishieni zile dola 3,000, imeandikwa katika mkataba. Zaidi ya hayo, hawana hati na hata hawajui jinsi ya kutoroka."
Mchezo wa Kriketi na shughuli zingine
Wakati wa vita, baadhi ya wanaume na wanawake hawa waliambiwa na waajiri wao "wewe baki hapa", wakati wao wanakimbia. Wahamiaji hao pia hatimaye walikimbia, lakini bila kujua wapi pa kupata makao. Kisha waligonga kwenye milango ya Shirila la Kijesuit (JRS) na huko wanasema hawakupata "wenzao" tu bali pia "familia." Familia inayoungana, inayokutana kwenye Misa au kufungua milango kwa vikundi vya maombi vya Wabuddha, ambavyo husaidia nje na kusaidiana ndani, bila kuangalia asili au dini. Kuna shughuli nyingi, kuanzia na kriketi ya dini nyingi na tamaduni nyingi ambayo hukusanya karibu watu 200-300 kila mwezi siku za Dominika. “Sisi hucheza kuanzia macheo hadi mawio ya jua,” alieleza Fernando, “kila Dominika Wakristo hufika na tunashiriki shangwe ya Misa, pamoja na wengine shangwe ya michezo. Ni njia ya uhusiano." "Wamejipanga na ni nzuri," Michael alisema. Na ni nzuri ukizingatia kwamba peke yao wangebaki wamejawa na "woga, uchungu, mateso, matamanio ya nyumbani ambayo tunakusanya ndani, bila kuhisi kuungwa mkono na serikali".
Zawadi ya picha ndogo iliyochorwa na bibi
“Asante kwa kushirikisha mapambano yenu Je! mnajua ni nini kinachoweza kuwafanya mjisikie vizuri zaidi? Kuwa hapa… Kuchukua utofauti na kuunda umoja katika utofauti,” Kardinali Czerny alisisitiza. Kisha aliwahimiza kuboresha "mawasiliano", kati yao na waandishi wa habari: "Shirikisheni historia zenu na kila kitu mlicho nacho ndani". Hatimaye, aliwapa wale waliokuwepo picha ndogo ya Familia Takatifu ikikimbilia Misri: "Bibi yangu aliichora, sisi pia ni familia ya wakimbizi."
Katika mazungumzo na ndugu
Kardinali alitoa zawadi hiyo kwa Wajesuit aliokutana nao katika Jumuiya ya Mtakatifu Yosefu, waliojishughulisha na utume , kazi za elimu, kazi za uchungaji wa kijamii au kwa mapadre wastaafu wasio na uhuru. Mwaliko kwao ni “kukutana, kusikiliza, kuunga mkono” maaskofu: “Kazi yetu ni kuwasaidia maaskofu na, tunaposema maaskofu, tunamaanisha watu wote wanaomsaidia kutekeleza utume wake.” Kisha kuwatia moyo kuwa "mawakala wa matumaini" katikati ya matukio mengi mabaya, ikiwa ni pamoja na vita na hatua dhidi ya wahamiaji ambayo inatikisa enzi hii. Jibu liko katika mafundisho ya Papa katika Waraka wake wa: "Fratelli tutti... Sio tu suala la Kitaalimungu na kichungaji bali ni pendekezo la Baba Mtakatifu kwa ulimwengu." Mchakato wa sinodi “pia ni mwitikio mwingine kwa changamoto za ulimwengu. Mbinu nyingine zote hazifanyi kazi tena: kinachohitajika ni kusikiliza na utambuzi,” Kardinali huyo alisema. Na mwisho wa mkutano huo, aliwaomba Wajesuit wa Lebanon wamwombee Papa hali ya afya yake.