杏MAP导航

Tafuta

Hospitali ya Kipapa  ya Watoto ni ya 6 kwa Ubora kati ya vituo 25 vya kimatibabu maalum Ulimwenguni. Hospitali ya Kipapa ya Watoto ni ya 6 kwa Ubora kati ya vituo 25 vya kimatibabu maalum Ulimwenguni. 

Bambino Gesù ni Hospitali ya 6 iliyo bora zaidi ya Watoto Ulimwenguni kwa mujibu wa jarida la Marekani!

Katika jarida la kila Juma la Marekani,limebainisha kuwa Hospitali ya Watoto Bambino Gesù ni hospitali pekee katika hospitali 25 iliyo bora kwa vifaa maalum Ulimwenguni.Tangu 2020,imekuwa Hospitali ya kwanza ya watoto nchini Italia katika orodha iliyotolewa na Jarida hilo la Marekani na ya kwanza nchini Italia.

Na Angella Rwezaula – Vatican.


Hospitali ya Kipapa ya Watoto ‘Bambino Gesù’ imejumuishwa mwaka huu 2025 katika nafasi ya Hospitali zilizo bora zaidi ulimwenguni kwa mujibu wa taarifa na tafiti zilizoandaliwa kuanzia 2019 na Jarida la ‘Habari za kila Juma’(Newsweek) la Marekani , pamoja na jukwaa la Akili Mnemba za data ulimwenguni. Kwa undani, Hospitali ya Bambino Gesù ndiyo hospitali bora zaidi ya watoto nchini Italiana ya 6 katika orodha ya kimataifa ya vituo maalum.

Maabara
Maabara

Hospitali inayoongoza nchini Italia katika uwanja wa watoto tangu 2020, mwaka huu 2025, Hospitali ya Kipapa ya Bambino Gesù imepanda ngazi tatu, kutoka nafasi ya 9 duniani kote mwaka 2024 hadi nafasi ya 6. Zaidi ya hayo, mnamo 2025, ndicho kituo pekee cha watoto cha Italia kilichojumuishwa katika zile 25 bora. Jarida la Marekani la (Newsweek) kila juma kupitia uainishaji wa Hospitali Bora Duniani - sasa katika toleo lake la saba - linatambua vituo bora zaidi vya huduma za afya ulimwenguni kulingana na mbinu ya tathmini inayozingatia mapendekezo ya hospitali, uzoefu wa mgonjwa na KPI za matibabu, yaani, viashirio muhimu vya utendakazi kama vile vya usalama wa mgonjwa, hatua za usafi na ubora wa matibabu.

Moja ya Picha ya Papa na Rais wa Hospitali ya Kipapa,Bwana Onesti(2023)
Moja ya Picha ya Papa na Rais wa Hospitali ya Kipapa,Bwana Onesti(2023)   (Vatican Media)

Mnamo 2025, safu ya Jarida la Kila juma la (Newsweek) liliundwa kwa kuchambua utendaji wa hospitali bora 2,445 zilizosambazwa katika nchi 30 tofauti ulimwenguni. Utambuzi huu unaongeza vyeti vya kimataifa vilivyopatikana na Hospitali kwa miaka mingi, ikijumuisha kibali cha JCI kama Kituo cha Matibabu cha Kielimu kwa shughuli zake kali katika uwanja wa mafunzo ya matibabu na utafiti wa kimatibabu na kisayansi. Kwa sasa, Bambino Gesù ni Kituo cha kwanza cha Madaktari wa Watoto barani Ulaya kulingana na idadi ya washirika (20 kati ya 24) kwa Mitandao ya Marejeo ya Ulaya kwa Magonjwa Adimu (ERN) na inasimamia moja ya mihimili mikubwa zaidi ya Ulaya katika taaluma zote za watoto, ikirekodi zaidi ya huduma milioni 2.5 za wagonjwa wa nje, Msaada wa kwanza 95,000 kwenye Chumba cha Dharura na zaidi ya taratibu 30,000 za upasuaji kwa mwaka.

Tiziano Onesti,Rais wa Hospitali ya Kipapa la Bambino Gesù
Tiziano Onesti,Rais wa Hospitali ya Kipapa la Bambino Gesù

"Kuweka nafasi kwa Hospitali ya Watoto ya Bambino Gesù katika viwango vya dunia vya Jarida la habari za kila Juma (Newsweek) inatuza njia ya ubora uliopatikana hadi sasa. Tuna jukumu la kuendelea kutoa huduma bora kwa wagonjwa wetu wadogo, bora na salama, lakini pia kusukuma mipaka ya utafiti na mazoezi ya kimatibabu katika uwanja wa watoto hata zaidi. Tumeitwa kuelewa na kusimamia vyema teknolojia mpya na uvumbuzi, daima tukibaki waaminifu kwa maadili yetu na kwa utume ambao Baba Mtakatifu anatukumbusha kila wakati: kuwaweka wagonjwa wetu wadogo na familia zao katikati ya kila kitu tunachofanya,” alisisitiza rais wa Hospitali hiyo Bwana Tiziano Onesti.

Hospitali ya Kipapa
27 Februari 2025, 16:33