Gallagher:Diplomasia ya Papa ni matumaini kama tiba ya Ulimwengu uliogawanyika
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Katika Kikao cha ngazi ya juu cha 58 cha kawaida cha Baraza la Haki za Binadamu kinachoendelea huko Jijini Geneva nchini Uswis, Jumanne tarehe 25 Februari 2025, Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa, alipata fursa ya kusisitiza baadhi ya mambo makuu aliyoyaibua Papa Francisko kwenye upapa wake katika hotuba yake. Askofu Mkuu alisema kwamba “Diplomasia ya matumaini,inayopendwa sana na Papa ni ujumbe muhimu na wa uponyaji kwa kushughulikia migawanyiko na mipasuko ya kimataifa, ili kujibu ukiukwaji wa haki za kimsingi na hitaji la ishara zinazoonekana za uaminifu"katika nyakati tunazoishi.”
Mwakilishi wa Vatican aliwasilisha hotuba yake kwa taswira ya Jubilei ya matumaini ikilinganishwa na ulimwengu unaokabiliana na maafa ya migogoro mingi, migogoro ya kimataifa na ukiukwaji unaoendelea wa haki za binadamu. Uingiliaji kati wake uliendelezwa kuhusu haki ya kuishi,"sharti la maendeleo ya haki zingine zote za binadamu. Kama Papa Francisko tayari amesisitiza, kuwa hakuna mtoto aliye na makosa au hatia ya kuwepo, na kama vile hakuna mzee au mgonjwa anayeweza kunyimwa matumaini na kutupwa.
Vatican inatumaini kwamba maadhimisho ya miaka 30 ya Kongamano la Dunia la Wanawake mjini Beijing litakuwa ni tukio la kusherehekea zawadi za kipekee za wanawake na kuunga mkono wito wa kuwa mama. Askofu Mkuu Gallagher aliunga mkono mwito wa Papa wa kukomeshwa kwa adhabu ya kifo, akibainisha kwamba leo takriban watu milioni 125 wanalazimika kuyahama makazi yao. Dawa ya mgogoro huu, daima akimnukuu Papa Francisko, ni kuundwa kwa"njia za kawaida na salama, pamoja na kuzingatia zaidi ya ubinadamu wa wakimbizi, ambao hawapaswi kuchukuliwa kama vitu vya kuwekwa.
Mwakilishi wa Vatican aidha a alizindua upya pendekezo la kufuta deni la nchi maskini, akisisitiza jinsi karibu nusu ya watu duniani wanaishi katika nchi zinazotumia zaidi kulipa nakisi hii kuliko kwenye afya na elimu. Hili ni swali la haki na ukarimu, kama ilivyoelezwa tayari na Papa, ambayo inahusishwa na deni la kiikolojia kati ya Kaskazini na Kusini mwa dunia.
Suala jingine lililoshughulikiwa na Askofu Mkuu Gallagher ni ukosefu wa uhuru wa kidini, unaofafanuliwa kama kizuizi kwa amani ya kudumu na maendeleo Fungamani. Leo, takriban Wakristo milioni 380 wanateswa kwa ajili ya imani yao, Katibu wa Vatican alikumbuka, akitumainia uhuru unaojumuisha madhehebu yote.
Askofu Mkuu Gallagher alihitimisha hotuba yake kwa kusisitiza jinsi changamoto za kimataifa zinavyoweza kushughulikiwa tu kupitia utawala wa pande nyingi ambao unaheshimu uhuru wa Nchi na kutumia lugha ya kawaida. Hatari, ilikuwa imeonesha na Papa, ni ile ya kunyonya hati katika masuala muhimu sanakubadilisha maana ya maneno au kutafsiri tena kwa upande mmoja yaliyomo katika mikataba ya haki za binadamu kuendeleza itikadi zinazogawanyika, zinazokanyaga maadili na imani ya watu. Aina ya itikadi ya kikoloni, Askofu Mkuu Gallagher aliongeza, ni ile inadhoofisha uhusiano wa kimataifa na kuhatarisha uadilifu wa taasisi za kimataifa, na kuvuruga umakini kutoka katika maswala yaliyo muhimu sana.