杏MAP导航

Tafuta

2025.02.17 mazishi ya Monsinyo Joseph Ballung, katika Parokia ya Mtakatifu Maria huko Transpontina,Roma 2025.02.17 mazishi ya Monsinyo Joseph Ballung, katika Parokia ya Mtakatifu Maria huko Transpontina,Roma  

Mons.Ballong:shuhuda wa kinabii,jasiri na mwenye kuona mbali!

Ni shukrani kwa miaka mingi ya kazi yake katika Kipindi cha Kifaransa Afrika cha Radio Vatican,kikijumuisha kutangaza ziara 12 za kitume Barani Afrika na vikao 6 vya sinodi za Maaskofu.Shukrani kwa zawadi ya ushuhuda wake wa kinabii,ujasiri ambao unageuka kuwa dhamana ya kuendeleza mawasiliano ya Kanisa la sura ya Kiafrika.Haya yamo katika salamu za Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano,Dk.Ruffini wakati wa kumuaga Monsinyo Joseph Ballong aliyefariki tarehe Mosi Februari 2025.

Na Angella Rwezaula – Vatican.


Baraza la Kipapa la Mawasiliano na Umoja wa Jumuiya ya Watu wa Togo mjini Roma wameungana pamoja katika misa ya mazishi na kumuombea huku wakitoa salamu za mwisho kwa ajili ya Monsinyo Joseph Ballong, aliyefariki dunia tarehe Mosi Februari 2025 akiwa na umri wa miaka 76 na alihudumu kwa miaka 34 katika Radio Vatican. Misa ilifanyika Jumatatu asubuhi tarehe 17 Februari 2025 katika Parokia ya Mtakatifu Maria, huko Traspontina, Roma iliyoongozwa na Kardinali Giuseppe Bertello, kwa kushirikiana makardinali kadhaa: Kardinali Peter Kodwo Appiah Turkson, Kansela wa Taasisi ya Kipapa ya Elimu za Sayansi, Kardinali Francis Arinze, Mwenyekiti Mstaafu wa Baraza la Kipapa la Ibada na Nidhamu za Sakramenti za Kanisa, pia Kardinali Robert Sarah, Mwenyekiti Mstaafu wa Baraza la Kipapa la Ibada na nidhamu za Sakramenti za Kanisa, Monsinyo Lucio Adriàn Ruiz, Katibu wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano na uwepo wa idadi kubwa ya Mapadre na watawa wa Jumuiya ya Togo mjini Roma, wengine mapadre kutoka sehemu mbali mbali za Afrika walioko Roma pamoja na watawa na walei na wafanyakazi wa Vatican kwa ujumla.

Wakati wa Misa ya Mazishi ya Padre Ballong
Wakati wa Misa ya Mazishi ya Padre Ballong

Katika salamu zake, kabla ya kuanza Misa Takatifu kutoka kwa Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano, zilizosomwa na Katibu wa Baraza hilo, Monsinyo Lucio Adriàn Ruiz , kwa niaba yake, Dk, Paolo Ruffini, awali ya yote aliomba samahani ya kutokuwepo kwa sababu za kifamilia lakini akionesha uwepo wake pamoja na wote katika sala.  Alia alibanisha kuwa "Pazia la uchungu linatufunika daima mbele ya fumbo la kifo na maisha ambayo yanaendelea katika katika wakati na baada ya wakati. Lakini leo hii, katika kumuaga Monsinyo Joseph Ballong-Wen-Mewuda, tunapomsindikiza na maombi yetu katika safari yake ya kwenda nyumbani kwa Baba, tukikusanyika hapa katika ushirika unaotuunganisha zaidi ya wakati na nafasi, huzuni huyeyuka na kuwa tabasamu la shukrani. Ni shukrani kwa miaka mingi ya kazi yake katika Kipindi cha Kifaransa Afrika cha Radio Vatican, kikijumuisha kutangaza ziara kumi na mbili za kitume Barani Afrika na vikao sita vya sinodi za Maaskofu.” Ni shukrani kwa zawadi ya ushuhuda wake wa kinabii, ujasiri na wenye kuona mbali; ambao unageuka kuwa dhamana: kuendelea kuyapa mawasiliano ya Kanisa sura ya Kiafrika.”

Misa ya Mazishi ya Padre Ballong
Misa ya Mazishi ya Padre Ballong

Mkuu wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano aidha alibainisha kuwa:  “Niliambiwa methali ya Kiafrika isemayo: ‘sisi ni tabasamu la waliotutangulia.’ Hapa tunaweza na lazima tuwe, kila mmoja katika nafasi yake, uso wenye tabasamu wa Kanisa la Kiafrika, jijini Roma. Sauti inayozungumza Kifaransa katika Afrika na duniani kote, katika lugha mbalimbali, ya Kanisa la Roma. Sio kipaza sauti, lakini mtandao unaotuunganisha sisi sote, wajumbe wa mwili mmoja. Historia ya Padre Ballong imekuwa hivi, kwa miaka mingi sana. Lugha za Kiafrika tunazozungumza ni watoto wa historia hii. Tunajulikana kwa matunda yetu. Ni juu yetu sasa, kwa vile Padre Ballong atakuwa akiipongeza kazi yetu ya kila siku kwa Bwana, kuwa sawa na kazi hiyo. Uhakika wa kuwa ndani yake mwombezi mpya asiyechoka.” Alihitimisha.

Mahubiri Tumaini la njia ya Afrika

Katika mahubiri yaliyotolewa na Monsinyo Janvier Marie Gustave Yameogo, wa huduma ya kichungaji ya Baraza la Kipapa la Mawasiliano alielezea kuwa: Uwepo wetu ni kielelezo cha matumaini yetu ya kumwona Yosefu tena siku moja, kwa sababu sisi sote ni mahujaji wa matumaini: mada ya Mwaka wa Jubilei 2025. Maisha yote ya Mkristo ni hija ya kifo na ufufuko unaoendelea, kuishi pamoja na Kristo na ndani ya Kristo katika Roho, kiukweli kumbeba Kristo ndani yetu, "tumaini la utukufu". […] Kifo ni tukio la Pasaka, linalowekwa alama wakati huo huo kwa kuachwa na ushirika na Aliyesulubiwa na Kufufuka. […]. Kwa hiyo, kwa mapokeo makuu ya Kikristo, kifo ni dies natalis, siku ya kuzaliwa katika Mungu, ya kuibuka kutoka kwa tumbo la giza la Utatu wa uumbaji na ukombozi, kutafakari uso wa Mungu, katika umoja na Mwana, katika kifungo cha Roho Mtakatifu. Katika Afrika wanasherehekea… Katika moja ya michango yake ya mwisho kwa toleo maalum la "Utamaduni na Imani" alijadili ibada ya mababu. Tumaini liliashiria njia yake ya kuiambia Afrika, ambayo majanga yake yaliwakilisha kama Nia ya Msalaba ya watu wa Afrika kwa ukombozi wa wanadamu wote, kwa umoja, bila shaka, na sadaka ya Kristo.

Ziara za kitume za Kipapa

Mara nyingi aliniambia kwamba kukosa matumaini kwa jinsi historia ya Afrika ilivyosimuliwa kulimhuzunisha. "Licha ya hali ya uharibifu ambao Afrika inajikuta nao, kuna matumaini." Alitumwa kama mwandishi wa habari kwa ziara  12 za upapa barani Afrika: 10 akuwa na  Papa Yohane Paulo II na 2 na Papa Benedikto XVI. Wengi wanamkumbuka kuwa msindikizaji kusafiri mwenye kutegemeka na mwenye busara, aliyekuwepo bila kusumbua hata kidogo; wengine wanasisitiza juu ya hisia zake kuu za udugu, juu ya uaminifu wake wa ajabu ...Kwa njia hiyo licha ya hali yake ya afya kuwa dhaifu, mnamo Septemba Monsinyo BALLONG alitoa hoja ya kuheshimu ya kumbukumbu ya rafiki yake Askofu Mkuu wa Lomé nchini Togo kwa kuhudhuria mazishi. Aliporudi, Monsinyo BALLONG alikuwa akikaribia hatua ya mwisho ya saratani ya tumbo kama matokeo ya kile alichotambua  kwa uangalifu na kufafanua kama matokeo ya upasuaji wa "Billroth" aliokuwa amefanyiwa akiwa na umri wa miaka 21, jijini Roma alipokuwa mwanafunzi wa  Chuo kikuu cha Kipapa cha Urbaniana, Roma (1969-1974)Tangu Desemba 2023 tayari alijua hali yake lakini alikubali kwa ujasiri na heshima na akasema: "Mwanadamu hupendekeza na Mungu hutimiza."

Sala ya Mtakatifu Ambrose

Nyuma ya mwonekano wake mkali lakini  kulikuwa na moyo wa dhahabu ... kuhani ambaye alijua jinsi ya kusikiliza kwa uhalisi na kwa shauku ya kweli kwa watu aliokutana nao na kisha kuwaleta kwa uaminifu moyoni mwake na sala zake. Kwa hivyo, ningependa kutumia  sala ya huruma kutoka kwa Mtakatifu Ambrose: "Zaidi ya yote, nipe neema ya huruma. Nijalie kujua jinsi ya kuwahurumia wenye dhambi kutoka ndani ya moyo wangu. Kwa sababu hii ni fadhila kuu. Nipe huruma kila ninaposhuhudia anguko la mwenye dhambi. Nisimtukane kwa kiburi, bali niache nilie na kuhuzunika pamoja naye. Acha nimlilie jirani yangu, nijililie nafsi yangu, nikalitumie neno hili; yule kahaba ana haki kuliko wewe." Kwa imani hii tunampongeza ndugu yetu Monsinyo Yosefu BALLONG kwa huruma ya kibaba, na tunaomba sisi wenyewe faraja ya kuishi utengano huu kwa matumaini thabiti ambayo tutakutana naye katika maisha ambayo hayafi, katika urafiki wa Kristo na watakatifu wake wote.

mazishi mons Ballong

Ni mzaliwa wa Togo

Ikumbukwe Monsinyo Joseph Ballong-Wen-Mewuda, Padre wa Jimbo la Kara nchini Togo, aliyefariki akiwa na miaka 76 alijitolea miaka mingi ya maisha yake katika huduma ya Kanisa, kama Padre na katika Radio Vatican. Kwa muda wa miaka 34, kupitia masafa ya Radio, aliufahamisha ulimwengu kuhusu Papa, Vatican, Kanisa zima na la Afrika, jamii na mengine mengi. Kuanzia 1986 hadi 2013 alikuwa na jukumu Idhaa ya Kifaransa ya Radio Vatican, ambayo toleo lake la kila siku lilianzishwa kwa wimbo wa mada: 'Rendez-vous avec l'Afrique', 'kukutana na Afrika' kwa sauti yake. Kwa wasikilizaji wengi, “alikuwa mojawapo ya vyanzo vikubwa vya habari zenye kutegemeka.” Mnamo mwaka 2021, katika kuadhimisha miaka 60 ya matangazo ya kila siku ya Radio Vatican barani Afrika, Mons. Ballong alionesha kwamba, katika tasnia kubwa ya habari ya leo, kusambaza habari za kuaminika, sahihi na kuthibitishwa ndiko kulikoifanya Radio Vatican kuwa ya kipekee.

Kifo na Ufufuko
17 Februari 2025, 16:21