Vatican Ina Uhusiano wa Kidipomasia na Nchi 184 Ulimwenguni
Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.
Takwimu zinaonesha kwamba, Vatican ina uhusiano wa kidiplomasia na nchi 184 duniani. Mabalozi wakazi wanaoishi mjini Roma kwa sasa ni 89, wengine, ni mabalozi wanaowakilisha nchi zao wakiwa wanatoka nje ya Roma. Kuna Mashirika ya Kimataifa kama vile, Shirikisho la Nchi za Kiarabu pamoja na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR. Tarehe 26 Juni 2018, Vatican na nchi ya San Marino wameridhia kwa pamoja mkataba wa ushirikiano na Kanisa ili kutoa fursa ya kufundisha dini shuleni. Tarehe 23 Agosti 2018 Vatican na Benin zimeridhia mkataba wa ushirikiano kati ya Serikali na Kanisa na kwamba, kwa sasa Serikali ya Benin inalitambua Kanisa kisheria!
Mkataba wa Kihistoria wa Muda Mfupi kati ya Vatican na China Kuhusu Uteuzi wa Maaskofu Mahalia ulitiwa saini kwa mara ya kwanza tarehe 22 Septemba 2018; ukapyaisha tena tarehe 22 Oktoba 2020, 22 Oktoba 2022 na hatimaye 22 Oktoba 2024. Mkataba umeongezwa tena kwa muda wa miaka minne yaani hadi mwaka 2028. Baba Mtakatifu anapenda kuonesha uvumilivu unaosimikwa katika matumaini, ili kuwapatia watu wa Mungu wachungaji wema na watakatifu. Vatican na China vimetiliana sahihi mkataba wa muda unaotoa fursa na uwezo kwa Kanisa kuteuwa Maaskofu mahalia. Katika kipindi cha Mwaka 2024 Vatican imetia saini mikataba kati yake na Burkina Faso pamoja na Jamhuri ya Watu wa Czech.
Itakumbukwa kwamba, tarehe 16 Julai 2018, Vatican iliridhia Mkataba na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa, UNESCO kuhusu umuhimu wa utamaduni kama chombo cha kujenga na kudumisha amani na maridhiano kati ya watu, hasa mwaka huu, 2019 UNESCO inapoadhimisha kumbu kumbu ya Miaka 70 tangu kuanzishwa kwake. Ushirikiano huu unapania kujenga na kudumisha haki msingi za binadamu, demokrasia na utawala wa sheria Barani Ulaya. Itakumbukwa kwamba, tarehe 21 Machi 2018 Vatican imeridhia mkataba wa kufundisha elimu ya juu Barani Asia na kwenye Visiwa vya Pacific. Na hatimaye, tarehe 30 Novemba 2018 Vatican pia imejiunga na malipo ya huduma kwa kutumia Euro, maarufu kama (SEPA).