Sherehe ya Epifania:Fuatilia misa ya Papa tarehe 6 Januari 2025
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Ufunuo wa Mungu kwa Watu wa Mataifa(Epifania),ndiyo sherehe ya kila mwaka ifikapo tarehe 6 Januari. Kwa Mwaka 2025,sherehe hii inapata maana kubwa katika mwaka wa Jubilei unaoongoza na kauli mbiu ya “Mahujaji wa Matumaini.” Ni katika muktadha huo ambapo Ndugu msikilizaji/Msomaji wa Vatican news, usisahau kufuatilia Misa Takatifu ya Baba Mtakatifu Francisko katika siku ambayo inatukumbusha Mamajusi kutoka Mashariki ya Mbali walipokwenda kumwona ‘Mfalme’ aliyezaliwa huko Betlehemu.
Misa Takatifu itafanyika Mjini Vatican Jumatatu tarehe 6 Januari 2025 kuanzia saa 3.55 majira ya Ulaya.
Kwa njia hiyo fuatilia misa ya Epifania yaani Tokeo la Bwana katika vyombo vyetu vya Habari za Vatican – Vatican News na katika masafa mafupi ya Radio:
Kiingereza, Afrika: kHz 17540 OC
Kifaransa, Afrika: kHz 17525 OC
Kireno, Afrika: kHz 15565 OC