杏MAP导航

Tafuta

2025.01.23 Kardinali George Jacob Koovakad 2025.01.23 Kardinali George Jacob Koovakad 

Papa Amemteua Kard.Koovakad kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwa Mazungumzo ya kidini

Kardinali huyo wa India anamrithi Kadinali Ayuso Guixot,aliyefariki Novemba mwaka 2024.Pia ataendelea kutekeleza jukumu lake kama mratibu wa safari za Upapa.

Vatican News

Baba Mtakatifu Francisko tarehe 24 Januari 2025 amemteua Kardinali wa India George Jacob Koovakad kuwa Mwenyekiti Mpya wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Majadiliajo ya kidini. Kardinali huyo anamrithi Kardinali Miguel Ángel Ayuso Guixot, aliyeaga dunia mnamo Novemba 2024. Kardinali pia atabaki na nafasi ya kuwa mratibu wa safari za kitume katika Sekretarieti ya Vatican

Wasifu wake

Kardinali Koovakad mwenye umri wa miaka 51 alizaliwa huko Chethipuzha, India, tarehe 11 Agosti 1973. Akapewa daraja la Upadre tarehe 24 Julai 2004. Mnamo 2006, alihitimu katika  Chuo Kikuu cha Kipapa cha Kanisa   na kujiunga katika huduma ya kidiplomasia ya Vatican na kutumwa katika Balozi mbali mbali za Vatican, kuanzia na Algeria kama katibu. Kisha alihudumu tangu 2009 katika Ofisi ya Balozi wa Vatican  nchini Korea, 2012, nchini Iran, 2015  huko Costa Rica kama mshauri mnamo mwaka 2018 na Ubalozi wa Vatican nchini Venezuela. Tangu 2020, amefanya kazi katika Sekretarieti ya Vatican katika kitengo cha Masuala ya Jumla.

Mnamo 2021, Papa Francisko alimkabidhi Uratibu wa ziara za kitume. Mnamo tarehe 25 Oktoba 2024, aliteuliwa kuwa Askofu Mkuu wa Nisibis wa Wakaldayo, akipokea daraja la uaskofu mnamo tarehe 24 Novemba huko Changanacherry  na kuwa Askofu Mkuu wa Ernakulam-Angamaly wa Syro-Malabars, Raphael Thattil. Aliundwa kuwa Kardinali katika Baraza la Makardinali tarehe  7 Desemba 2024, kwa ushemasi  wa Parokia ya  Mtakatifu Antony wa Padua lililoko Appia, Roma.

Papa amemteua Mwenyekiti mpya wa majadiliano ya kidini
24 Januari 2025, 16:14