Kard.Re aongoza mazishi ya Kardinali Angelo Amato:alikuwa mtu wa imani!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Katika Ibada ya Misa Takatifu iliyofanyika kwenye Madhabahu ya Kiti cha Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, alasiri tarehe 2 Januari 2025 na ambapo, Baba Mtakatifu Francisko alijumuika ili kuongoza ibada ya Buriani (Commendatio,) ikiwa ni mapendekezo ya mwisho kwa Mwenyezi Mungu kukaribisha roho ya marehemu mahali pema peponi na Ushirika wa Watakatifu, na vile vile (Valedictio) ambayo ni kuaga mwili kabla ya mazishi. Katika misa iliyoudhuriwa na Makardinali, maaskofu, mapadre na waamini, Watu wa Mungu iliongozwa na Kardinali Giovanni Battista Re, Mkuu wa Baraza la Makardinali kwa ajili ya Kardinali Angelo Amato aliyeaga dunia tarehe 31 Desemba 2024 akiwa na umri wa miaka 86. Katika mahubiri yake Kardinali Re alitoa sifa nyingi za marehemu kwamba alikuwa ni “Mtu tajiri wa imani na ubinadamu, aliye wazi kwa mazungumzo na aliyejaliwa uchanya wa asili kuelekea maisha na hali yake. Sifa ambazo pamoja na hekima na nguvu zilitambua maono ya Papa Yohane Paulo II ya kuanzishwa upya kwa Chuo cha Kipapa cha Taalimungu ambapo mabadilishano kati ya taalimungu na falsafa yaliwekwa katikati,” alisisitiza.
Mafunzo na ibada kwa Mama Maria
Katika mahubiri hayo Mkuu wa Baraza la Makardinali alirejea maisha ya Kardinali, aliyezaliwa Molfetta mwaka 1938 kwa familia ya wajenzi wa meli. Lakini ni “Kazi iliyowekwa kando akivutiwa na sura ya Don Bosco, na kujiunga na Shirika la Kisalesian huko Torre Annunziata. Baada ya taaluma yake ya kwanza ya kidini na kuwekwa wakfu wa kipadre, Kardinali Amato aligawanya masomo yake kati ya Roma na Chuo Kikuu cha Thesaloniki, nchini Ugiriki.” Baadaye alikuwa Mkuu wa Kitivo cha Taalimungu cha Chuo Kikuu cha Kipapa cha Salesian, ambacho pia angekuwa makamu wa mkurugenzi mwaka 1997, kwa mtindo wake wa kufundisha” alikumbuka Kardinali Re kuwa “kulikuwa na usawa kati ya Mafundisho ya Kristo(Christology) na ya Maria(Mariology,) iliyoamriwa na ibada fulani kwa Mama ambapo Kardinali "alizungumza kwa hiari".
Nguvu na hekima ya kupata tena Chuo cha Kipapa cha Taalimungu
Dhamira yake ya kitaaluma ilimfanya kuwa na wasifu uliochaguliwa na Yohane Paulo II kwa ajili ya "kuanzisha upya" Chuo cha Kipapa cha Taalimungu mnamo mwaka 1999, akimteua kuwa katibu. Mkuu wa Baraza la Makardinali alisisitiza kuwa “Hata katika wakati huo Kardinali Amato, alikuwa na uwezo wa wa kufanya taaluma za asili tofauti kuwasiliana na kila mmoja. "Sufficit gratia mea" yaani “Neema yako yatosha”, ni kauli mbiu iliyochaguliwa ya kiaskofu, ambayo, alikumbuka, alibaki "mwaminifu katika matendo yake" hasa katika miaka ya mwisho ya maisha yake, "akiwa na mateso". Aliyeteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Kuwatangaza Watakatifu na Papa Benedikto XVI mnamo Julai 2008, Ratzinger mwenyewe alimuunda kuwa kardinali mnamo 2010.
Matumaini kamili yasiyokufa
Kardinali Amato alisimama kidete kwa ajili ya maandalizi yake makubwa ya kitaalimungu na uimara wa mafundisho," alisema Kardinali Re. "Roho yake ya kweli" ilitekelezwa kama Don Bosco kisha ikaamsha heshima na huruma" kwa wale waliomjua. Kwa mwamini, kifo ni kifungu kutoka katika kuwepo kwa maumivu na majaribio hadi maisha kamili na ya kudumu ya furaha ya Mungu",alisisitiza Kardina Re na huko, akionesha jinsi ambavyo katika mtazamo huu kunaweza kuwa na nafasi tu ya tumaini. Matumaini hayo ni sawa yaliyojaa na ambayo hayafi kwa Kardinali Amato ambayo alikiri mwenyewe wakati wa hija yake duniani.”