Katika Jubilei,Lugha za Ishara za Vyombo vya Habari vya Vatican zinaongezeka
Vatican News
Hatua mpya muhimu ya Mpango wa “Nessuno Escluso,” yaani, “pasiwepo aliyetengwa,” katika fursa ya Jubilei ya Ulimwengu wa Mawasiliano, huduma ya Vyombo vya Habari vya Vatican inazindua Lugha ya Ishara kwa Kifaransa na Lugha ya Ishara ya Kihispania. Kwa hiyo kuanzia Dominika tarehe 26 Januari, 2025 ambayo ni Dominika ya Neno la Mungu na siku ya mwisho ya Jubilei ya Wawasilianaji, katika Sala ya Malaika wa Bwana na Katekesi, vitakuwa vinatafsiriwa moja kwa moja kwa Lugha ya Ishara ya Kiitaliano(LIS), Kihispania (LSE) na Kifaransa (LSF) , kwenye chaneli ya YouTube ya Vatican News na inapohitajika katika Lugha ya Ishara ya Kiingereza cha Kimarekani(ASL) pia kwenye YouTube.
Manukuu ya moja kwa moja ya maneno ya Papa pia yatatunzwa katika Kiitaliano wakati wa Jubilei. Huduma hiyo katika lugha mbili mpya za ishara ziliwezekana kutokana na usaidizi wa kifedha wa Mfuko wa Conrad N. Hilton na inalenga kuwa ishara madhubuti ya kuishi Jubilei kwa njia inayojumuisha ili kila mtu ahusike na kusiwe na mtu yeyote anayetengwa. Pamoja na utiririshaji wa moja kwa moja katika lugha ya ishara, ulioanza na lugha ya Kiitaliano na Kiingereza cha kimarekani mnamo 2021, Mpango wa “Nessuno Escluso” yaani “Pasiweyo anayetengwa,” pia inatoa programu ya“Vatican for All information”, yaani “Vatican kwa taarifa zote” uliyoundwa na Baraza la Kipapa la Mawasiliano kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa mawasiliano na wanaoona.
App au Programu, inayoweza kupakuliwa bila malipo kwenye Google Play na Apple Store, inaruhusu ufikiaji wa maudhui ya habari kuhusu matukio ya kipapa na Vatican. Pia hukuruhusu kusasishwa mara moja kuhusu maisha ya Kanisa ulimwenguni. Mpango wa "Nessuno Escluso" ulizinduliwa katika hafla ya Pasaka 2021 kwa kufunguliwa kwa chaneli ya moja kwa moja ya kutafsiri katika Lugha ya Ishara ya Kiitaliano na moja iliyoahirishwa kwa tafsiri ya ASL (Lugha ya Ishara ya Marekani) Mpango huu unaratibiwa na Sista Veronica Donatello, mshauri wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano na Mkuu wa Huduma ya Kitaifa ya Baraza la Maaskofu wa Italia kwa ajili ya Huduma ya Kichungaji kwa Watu Wenye Ulemavu.
Mpango huu unawezekana kutokana na ushirikiano na msaada wa kifedha wa Taasisis ya Pio kwa ajili ya Ulemavu wa Mcho cha Milano CBM Italia, Misheni za Kikristo kwa ajilli ya Vipofu Duniani, Marafiki wa Radio Vatican (,Freunde von Radio Vatikan) katika Kituo cha Viziwi cha Mtakatifu Francis Borgia huko Chicago, Illinois, Marekani, mwanachama wa Mfuko wa Conrad N. Hilton.