Kardinali Parolin atembelea Paris na kukutana na Waziri Mkuu Bayrou
Vatican News
Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican yuko nchini Ufaransa ili kushiriki Kongamano la Quai d'Orsay huko Paris lililotolewa kwa ajili ya kumbukizi ya ubadilishanaji wa barua uliofanyika miaka mia moja iliyopita (11 - 17 Januari 1924) kati ya kipindi cha utume wa Balozi wa Vatican nchini Ufaransa, Monsinyo Bonaventura Cerretti, ambaye angekuwa Kardinali baadaye mwaka uliofuata 1925,na Waziri Mkuu, Raymond Poincaré, Rais wa zamani wa Jamhuri hiyo.
Baraza la nchi ya Ufaransa linayachukulia maandishi hayo kama makubaliano ya kimataifa yanayofangamanisha Ufaransa na Vatican na kuruhusu kuanzishwa kwa chama cha majimbo katika kila Jimbo na hivyo kurekebisha ombwe la kisheria lililoanzishwa na sheria ya 1905 ya kutenganisha Makanisa na Serikali. Maendeleo ya kisheria yaliyofuata hayajabadilisha utiifu wao wa sheria ya 1905, kama ilivyothibitishwa na Waziri Mkuu Elisabeth Borne mnamo Machi 2023.
Kardinali Parolin anasindikizwa kwenye mkutano huo Alhamisi tarehe 16 Januari 2025, na Balozi wa Vatican Celestino Migliore, pia alikuwepo rais wa Baraza la Maaskofu wa Ufaransa, Askofu Mkuu Éric de Moulins-Beaufort, Askofu Mkuu wa Reims. Alhamisi saa 12.30 jioni, kutakuwa na mkutano kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na Waziri Mkuu wa Ufaransa, François Bayrou, ambao utafanyika katika Hoteli ya Matignon. Tovuti ya Serikali ilibainisha kuwa pamoja na Mkutano wa kitaasisi, kisha Kardinali atakwenda katika makao makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani, ambayo mkuu wake, Bruno Retailleau, ataadhimsha pia mia na hatimaye, mkutano umepangwa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Waziri Jean-Noël Barrot kuhusu masuala ya kimataifa yenye maslahi ya pamoja.