杏MAP导航

Tafuta

2025.01.13 Askofu Mkuu Gallagher wakati wa Misa katika Jamhuri ya Congo Brazaville. 2025.01.13 Askofu Mkuu Gallagher wakati wa Misa katika Jamhuri ya Congo Brazaville. 

Ask.Mkuu Gallagher nchini Congo:Papa anaipenda nchi hii,jengeni jamii yenye haki na umoja

Katibu wa Mahusiano na Mataifa na Ushikiano wa Mashirika ya Kimataifa akiwa nchini Brazzaville,tangu tangu 11-14 Januari 2025 aliadhimisha Ibada ya Misa ya Jubilei ya Harakati za kikanisa.Aliwapa salamu za Papa Francisko kuwa:"Baba Mtakatifu yuko karibu nanyi wakati roho zenu za ustahimilivu zinapojaribiwa na majanga ya asili na hali ngumu katika maisha na jamii."Mwaliko wa Jubileei ni kutonyang'anywa matumaini. Askofu Mkuu alikutana na Rais,Waziri wa Nchi za Nje na uzinduzi wa kazi za Tume.

Na Salvatore Cernuzio na Angella Rwezaula– Vatican.

Katibu wa Vatican wa Mahausiano na Ushirikiano na Nchi na Mashirikia ya Kimataifa tangu tarehe 11  hadi 14 Januari 2025 amekuwa Barani Afriika huko Nchini Congo Brazaville katika fursa ya  Kuanzisha Kazi ya Tume Mchanganuo kwa ajili ya utekelezaji wa Mkataba wa Mfumo. Tume hiyo ni makubaliano yaliyotiwa saini mnamo 2017 na kuanza kutumika mnamo 2019, ambayo yanatambua hadhi ya kisheria ya Kanisa na taasisi zake, kulinda uhuru na uhuru wao. Akiwa huko kama ilivyokuwa imetaarifa awali pamoja na hili kumekuwa na matukio mbali mbali ya mikutano na sherehe mbali mbali. Awali ya yote, Askofu mkuu Paul Richard Gallagher aliwapa salamu na ukaribu wa Baba Mtakatifu Francisko kwa wakazi wa Jamhuri ya Congo, wanaojaribiwa na majanga ya asili, migogoro ya kikabila, na matatizo katika maisha na jamii.


Misa katika mraba

Akiwa katika mji mkuu Brazzaville Askofu Mkuu Galalagher alionana na Rais N'Guesso, Waziri Mkuu Collinet Makosso na Waziri wa Mambo ya Nje wa Congo – tarehe 12 Januari  aliadhimisha Misa ya Jubilei ya Harakati za kikanisa katika Uwanja wa Kanisa Kuu la Maria, uliowekwa wakfu kwa Kanisa la Moyo Mtakatifu wa Yesu.  Waliohudhuria ni Askofu Mkuu wa Brazzaville Bienvenu Manamika, Rais wa Baraza la Maaskofu, Balozi wa Vatican Askofu Mkuu Javier Herrera Corona, Maaskofu wa Congo na baadhi ya wajumbe wa serikali, pamoja na umati wa waamini, hasa wale wanaotoka katika hali halisi ya kikanisa, kwa kuuisha sherehe kwa muziki wa kiutamaduni, nyimbo na ngoma.

Salamu na shukrani za Papa

“Leo ninawaletea salamu na baraka za Papa Francisko, ambaye anafuatilia maisha ya watu wa Congo kwa umakini mkubwa. Papa anawapenda na yuko karibu na nanyi!” Kardinali Gallagher aliwaambia, mwanzoni mwa mahubiri yake. “Papa Francisko anawafikiria ninyi nyote, kaka na dada wapendwa wa jumuiya ya Kikatoliki ya Congo. Anajua vizuri matarajio yenu na matumaini yenu ya amani na udugu. Yuko karibu nanyi katika nyakati ngumu, roho yenu ya ustahimilivu mnapojaribiwa na mikasa ya asili na hali ngumu ya maishani na jamii.” Kutoka kwa Papa hadi kwa wakazi wote na kwa Kanisa la Congo pia "asante", alisisitiza Askofu Mkuu Gallagher akuwa  "kwa ushuhuda mnaotoa kwa ajili ya Injili na kwa ajili ya ujenzi wa jamii ya haki zaidi na ya kindugu, pamoja na matumaini. kwamba "Mwaka wa Jubilei na uimarishe imani yenu na kuangazia njia ya Kanisa zima la Congo kuelekea utakatifu."

Ushuhuda wa Kadinali Biayenda

Akizungumzia watakatifu, Askofu Mkuu   alikumbuka kwamba huko Congo kuna mashahidi wengi wa imani, hasa wale ambao wamejitoa wenyewe kwa Mungu kwa heshima ya uhuru wao na akili zao, kwa nguvu zao zote na kamama zao za kinabii, katika zawadi ya maisha yao. Kisha akakumbusha "mtu, wa mafundisho ya amani na ushuhuda wa kiinjili wa Kardinali wa Congo Emile Biayenda, mtumishi wa Mungu, mwathirika wa mapigano ya kikabila, kutekwa nyara na kisha kuuawa usiku kati ya tarehe 22 na 23 Machi 1977 akiwa na umri wa miaka 50.  Alikuwa ameundwa kuwa Kardinali na Papa Paulo VI, na wakati huo huo, na Mtakatifu Yohane Paulo Pili ndiye aliyetaka  kuanzisha Mchakato wa  kutangazwa kuwa Mtakatifu. Mabaki ya Biayenda yamehifadhiwa katika Kanisa Kuu la Brazzaville na ziara ya kutembelea kaburi la Kadinali huyo ilikuwa ndicho kituo cha kwanza cha Askofu Mkuu Gallagher alipowasili katika ardhi ya Congo. Katika mahubiri yake, Askofu mkuu aliomba kwa maombezi ya Mtumishi wa Mungu “ili tuweze kutambua uwepo wa Mungu katika jamii yetu, tuifanye upya, tuibadilishe, tuifanye kuwa ya haki zaidi, iliyo wazi na yenye umoja."

Jubile, wakati wa uongofu

Ni mwaliko ule ule ambao tayari alikwisha kuutoa mwanzoni mwa Liturujia, ambao ulilenga kabisa mada za matumaini, furaha na utume wa Kikristo, katika muktadha wa Jubilei, kwamba ni “wakati wa baraka wa huruma ya Bwana, ni wakati wa baraka wa kuongoka na kubadilika, vile vile ni wakati wa matumaini." Mwaka Mtakatifu ni mwaliko mzito wa kuamka kutoka katika usingizi wa mazoea, mwaliko wa kuikomboa mioyo yetu kutoka katik kila kitu kinachotuzuia kwa kweli kungojea ujio wa Bwana katika maisha yetu na kumtambua kuwa yuko kati yetu, "alisema Askofu Mkuu Gallagher. Kisha alihimiza "kuanza tena kwa nguvu mpya njia ya uinjilishaji na, tena, kuheshimu uumbaji, kuweka vifungo vya udugu na wote, kutenda haki, kuonesha upendo, kusaidia walio dhaifu na maskini zaidi."

Askofu Mkuu Gallagher wakati wa Ibada ya Misa
Askofu Mkuu Gallagher wakati wa Ibada ya Misa

Mjumbe wa Papa alisema “Hapa, Congo, Kanisa limepitia nyakati za shauku kubwa ya uinjilishaji, kwa elimu ya vizazi vipya katika mwanga wa Injili, zaidi ya yote, shukrani kwa ushuhuda wa upendo wa watu wengi ambao wamejiweka katika huduma ya wengine,  hasa wale walio dhaifu na wadogo zaidi, pamoja na mipango mingi ya mshikamano.” Mwishoni mwa mahubiri yake  wazo maalum kwa vijana, ambao alirudia maneno ya  Papa ambayo mara nyingi huwa akiweleza kuwa wavulana na wasichana: "Msijiruhusu kuibiwa na tumaini!". Na kwa hiyo “Tusinyang’anywe tumaini!” alisisitiza Gallagher,  bali “tuyainue macho yetu kwa Bwana! Tusikubali kukatishwa tamaa na magumu ya kila siku! Tusikate tamaa kuhusu siku zijazo; tunatembea licha ya vikwazo na matukio ambayo yanaweza kutuhuzunisha."

Wakati wa misa
Wakati wa misa

Misa hiyo ilifuatiwa na mkutano na Baraza la Maaskofu wa Congo. Askofu Mkuu aidha Gallagher alimtembelea Rais wa Jamhuri, Denis Sassou N’Guesso, na kisha Waziri Mkuu, Anatole Collinet Makosso kama ratiba ilivyokuwa imepangwa. Pia alikutana na mwenzake Jean-Claude Gakosso, Waziri wa Mambo ya Nje, ambapo pia kiini cha  safari tarehe 14 Januari imefanyika hafla ya uzinduzi wa kazi za Tume ya Pamoja ya utekelezaji wa Makubaliano ya Mfumo. Kisha Askofu Mkuu Gallagher alikutana na Waziri wa Ushirikiano wa Kimataifa na Uendelezaji wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, Denis Christel Sassou N' Guesso, ambayo ilikuwa ni mipango ya mwisho kabla ya kurudi jijini Roma.

Askofu Mkuu Gallagher
14 Januari 2025, 17:34