杏MAP导航

Tafuta

Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregoriana Roma. Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregoriana Roma.  (Foto ? Institute of Anthropology - IADC))

Papa atatembelea Chuo Kikuu cha Kipapa Gregoriana Novemba 5 kwa ajili ya Dies Academicus

Mkutano wa Papa katika Chuo Kikuu cha Kipapa utatambulishwa kwa salamu kutoka kwa Padre Arturo Sosa,mkuu wa Shirika la Yesu na makamu mkuu wa Chuo Kikuu hicho na kutoka Gambera Padre Mark A.Lewis.

Vatican News

Jumanne  asubuhi tarehe 5 Novemba 2024, katika fursa ya “Dies Academicus” - (ufunguzi wa Mwaka wa Kitaaluma wa Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregoriana, kitakuwa na furaha ya kumkaribisha Baba Mtakatifu Francisko ili kusikiliza maneno yake. Mkutano huo utatambulishwa kwa salamu kutoka kwa Padre Arturo Sosa S.J.,mkuu wa Jumuiya ya Yesu (Wajesuit) na makamu Chansela wa Chuo hicho  Gregoriana, na Padre  Mark A. Lewis S.J. Gambera  wakati  Programu hiyo itahitimishwa kwa kutoa tuzo za masomo kwa misheni  tatu za Chuo Kikuu.

Vyuo vikuu vikongwe zaidi kati ya vyuo vikuu vya kipapa

Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregorian ndicho chuo kikuu kongwe zaidi kati ya vyuo vikuu vya Kipapa. Asili yake inaanzia kwenye mpango wa moja kwa moja wa Mtakatifu Ignatius wa Loyola, mwanzilishi wa Jumuiya ya Yesu, ambaye katika mwaka wa 1551 aliweka misingi ya Chuo cha Kirumi, kinachojulikana pia kama Universitas omnium Nationum, katika huduma ya Kanisa la Ulimwengu. Kunako Mwaka 1873 Papa Pio IX aliamuru kwamba chuo kikuu kichukue rasmi jina jipya la Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregoriana. Mnamo 1930 makao makuu mapya na ya sasa yaliyopo katika Uwamja wa Pilotta yalizinduliwa. Kuanzia tarehe 19 Mei 2024, taasisi nyingine mbili zilizokabidhiwa kwa Shirika la Yesu - Taasisi ya Kipapa ya Kibiblia na Taasisi ya Kipapa ya Mashariki - zimejumuishwa kwa hakika katika Chuo Kikuu hicho cha Gregoriana, kama ilivyoombwa na Papa Francisko. Taasisi ya Kipapa ya Biblia, iliyoanzishwa mwaka 1909 na Papa Pio,  Taasisi ya Kipapa ya Mashariki iliyoanzishwa mwaka 1917 na Baba Mtakatifu Benedikto XV, ni taasisi ya juu zaidi ya utafiti na masomo ya Mashariki ya Kikristo yenye utume mahususi wa huduma kwa Makanisa ya Mashariki.

Gambera: ziara hiyo inaadhimisha hatua muhimu katika historia yetu

Kwa mujibu wa Gambera Padre Mark Lewis S.J. alieleza kuwa: “Ziara hii ya Papa Francisko inaadhimisha hatua muhimu katika historia yetu. Misheni tatu za Chuo Kikuu - kwa kuingizwa ya Bibilia na Mashariki kama misheni ya asili ya Gregoriana inaunda ushirika mpya na kutufungua kwa upeo mpya. Tuna furaha kumkaribisha Baba Mtakatifu katika wakati huu wa kihistoria.”

Karibu wanafunzi elfu 3

Hadi sasa, Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregoriana kina wanafunzi 2952 wa mataifa 121. Kupitia vitengo vyake kumi na sita vya kitaaluma - vinavyojikita katika taaluma kama vile taalimungu, falsafa, sayansi ya kikanisa ya mashariki, sheria za kanoni, masomo ya Mashariki ya Karibu ya kale, akiolojia ya Biblia, sayansi ya kijamii, historia na urithi wa kiutamaduni wa Kanisa, saikolojia, anthropolojia na ulinzi, masomo ya Kiyahudi, na masomo ya kidini, chuo Kikuu cha Gregoriana kinatoa pendekezo pana na tajiri la kitaaluma ambalo linajumuisha tamaduni ya Kanisa la Kilatini na yale ya Makanisa ya Mashariki.

Papa atatembelea Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregoriana,jijini Roma
01 Novemba 2024, 15:33