杏MAP导航

Tafuta

2024.11.13 Ziara ya Askofu Mkuu Richard Gallagher katika Chuo Kikuu Katoliki, kwenye Kitivo cha Mafunzo ya Taalimungu(KUL),kitengo cha Wafungwa huko Lublin nchini Poland.d. 2024.11.13 Ziara ya Askofu Mkuu Richard Gallagher katika Chuo Kikuu Katoliki, kwenye Kitivo cha Mafunzo ya Taalimungu(KUL),kitengo cha Wafungwa huko Lublin nchini Poland.d.  (Tomasz Koryszko/KUL)

Gallagher akutana na wanafunzi wa taalimungu katika Chuo Kikuu cha Lublin

Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya kimataifa akiwa nchini Poland alizungumza na wafungwa wanaohudhuria masomo katika Kitivo cha "Taalimungu ya Familia" iliyobobea katika utunzaji wa watu wenye ulemavu.

Vatican News

Wakati wa ziara yake nchini Poland, katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Yohane  Paulo II huko Lublin (KUL),Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa vatican wa Mahusiano na Nchi na Mashirika ya Kimataifa, Jumatano tarehe 13 Novemba 2023 alitembelea kituo cha Wafungwa  huko Lublin na kuzungumza na wafungwa wanaosoma katika  Chuo Kikukuu Katoliki (KUL) (Kitivo cha Taalimungu ya Familia iliyobobea katika Chuo Hicho), utunzaji wa watu wenye ulemavu).  Askofu Mkuu alisema kuwa: "Sisi Wakristo tunaamini kwamba Mungu daima humwangalia mwanadamu kwa jicho la ukarimu, huona mema ndani yake. Hapa, kwa kushangaza, shukrani kwa elimu na malezi ya imani, mtapewa fursa kubwa."

Papa Francisko, kwanza alitunuku nishani ya Njiwa Mweupe

Kanali Anna Ausz, mkurugenzi wa Kituo cha  Wafungwa, ambaye anasimamia utekelezaji wa masomo, pamoja na Padre  Gregory Drausl, anayehudumia kikanisa cha gereza, walimkabidhi  Askofu Mkuu huyo nishani ya Njiwa Mweupe kwa ajili ya Papa Francisko.  Papa ndiye wa kwanza kupokea nishani hii ya Njiwa Mweupe kwa kutambua ulezi wake kwa wafungwa. Ishara ya medali inarejea njiwa wa kibiblia aliyeachiliwa kutoka katika Safina ya Nuhu, ambaye, akiwa amebeba tawi la mzeituni, alitangaza mwisho wa adhabu ya gharika. Shughuli za wafanyakazi wa Kituo cha Mahabusu, zinazohusisha Kanisa na Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Lublin, huleta hukamavu  kwa maisha mazuri mara moja.

Wafungwa wanamwandikia Papa

Wafungwa hao walimpatia  Askofu Mkuu Gallagher barua kwa ajili ya Papa iliyotiwa saini na wafungwa kadhaa na makatekista wa Harakati ya Neocatechumenali, ambayo imekuwa ikihubiri katika kituo cha Wafungwa  cha Lublin tangu Mei mwaka 2023, na tayari wanaongoza Jumuiya nne. Wengi wa wanafunzi wanaoshiriki katika mkutano hufuata malezi ya kiroho ya Njia ya Neokatekumenali. "Tunahisi kwamba Kanisa linatutunza, kupitia uinjilishaji na uwezekano wa elimu. Tunaona kwamba hatujafutwa, kwamba kuna mustakabali mwema mbele yetu", alitangaza mkuu wa Jumuiya ya kwanza, akitoa zawadi iliyopambwa sana ya  barua, pamoja na picha za nyingine iliyotengenezwa na ya kiliturujia.

Kituo cha Utafiti cha  mafunzo hara kwa wafungwa katika Chuo Kikuu(KUL)

Askofu Mkuu  Gallagher alipotembelea vyumba vya madarasa ambako masomo hayo yanafanyika;  moja lilikuwa limetoka kupata funzo la  ushirikiano na mashirika yasiyo ya kiserikali, lingine lilikuwa linaanza somo la maadili. Miros?aw Kalinowski, mkuu wa Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Lublin, kisha akisindikizana na Padre hadi kwenye chumba kikuu cha pamoja cha Kituo cha Gereza ambapo sherehe zinazohusiana na chuo kikuu pia hufanyika, kama vile uzinduzi wa hivi karibuni wa mwaka wa masomo.  Karibu na chumba cha kawaida pia kuna Kikanisa kidogo chenye picha kubwa  , iliyochorwa na wafungwa na mwanafunzi wa Kitivyo hicho, inayoonesha Kristo na Mitume na "Wanawake kwenye Kaburi Tupu". Tangu 2013, wafungwa kadhaa wamemaliza masomo yao katika Chuo hicho (KUL) na zaidi ya 80% ya wahitimu hawajafanya uhalifu baada ya kutoka gerezani.

Diplomasia ya Vatican

Utatuzi wa migogoro – kuanzia  Ukraine hadi Mashariki ya Kati, kutoka Caucasus hadi Myanmar, kutoka Ethiopia hadi Yemen - na kujenga amani; kukuza na kulinda haki za binadamu; uhuru wa kidini; utunzaji wa nyumba ya kawaida; kulinganisha "utamaduni wa kutupa"; uhamiaji; upatikanaji wa huduma za afya. Na tena: ulinzi wa sera za haki za kiuchumi; mapambano dhidi ya biashara haramu ya binadamu; kukuza udugu na ushirikiano wa pande nyingi.  Kanisa kama "hospitali  katikati ya  uwanja wa  vita", Vatican  ni "sehemu muhimu" ya mjadala juu ya mivutano ambayo jumuiya ya kimataifa inapaswa kukabiliana nayo na juu ya shughuli zinazofanyika katika jukwaa la kimataifa, kutumia nguvu laini " ambayo inaruhusu "kupata matokeo  hata mamlaka kuu ya ulimwengu mara nyingi ambazo hujitahidi kufikia yenyewe." Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican wa  Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa, alionesha kwa kina wito na asili, zana na mahusiano, shughuli na mbinu za utendaji za Diplomasia ya Vatican iliyodumu kwa miaka elfu moja inayojishughulisha na mahusiano na nchi 184 hivi sasa, na  sehemu kubwa ya taasisi zinazowakilisha utawala wa kimataifa. Alielezea hayo katika lectio magistralis  , mafunzo marefu sana katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Lublin (KUL) juu ya mada "Diplomasia ya Vatican  katika Ulimwengu wa Kisasa" wakati wa mkutano ulioandaliwa tarehe 12  Novemba 2024 , na Kitivo cha Masomo ya Diplomasia ya Chuo Kikuu. 

Jitihada za Vatican kama Hospitali katikati ya uwanja wa vita

Askofu Mkuu Gallagher awali ya yote  aliakisi  hali ya sasa ya shughuli ya kidiplomasia za Vatican  kuanzia historia, kisha hadi miongo ya kazi iliyowekwa kwa "kujenga madaraja, kutafuta mazungumzo na kila mtu, kwa kutumia unyenyekevu na uvumilivu hadi kiwango cha juu kufungua mafundo ambayo hayawezi kutenganishwa," ikijitahidi kurekebisha dalili hafifu za nia njema za pande zinazozozana ili kuanza mchakato wa amani. Lile la kipapa ni "diplomasia ya huruma", inayoeleweka kama "dhamira ya kweli ya kisiasa ya mshikamano, kwa nia ya kukuza wema wa wote". Si lengo la kufikirika, bali ni utekelezaji wa hatua madhubuti kama vile kufutwa kwa madeni ya nje na kukuza ushirikiano na sera za maendeleo au kuthamini utu wa binadamu, "hata katika hali ya uhalifu mkubwa" kama vile adhabu ya kifo.

Utekelezaji katika nyanja za kukuza na kulinda haki za binadamu

Sehemu nyingine ya utekelezaji ni kukuza na kulinda haki za binadamu, kwa hiyo haki ya kuishi na kutokiukwa kwa kila mtu, ulinzi wa utakatifu wa maisha ya binadamu kutoka mimba hadi kifo cha asili. Kwa kutetea haki hizi, Vatican sio tu inaweka kiwango cha maadili, lakini pia inaibua mijadala muhimu kwenye hatua ya kimataifa. Alisema Askofu Mkuu  Gallagher, akizikosoa nchi au kanda za nchi ambazo zinatafuta kuweka maono ya haki za binadamu, asili na utu ambayo hailingani na mafundisho ya Kanisa. Kwa bahati mbaya, katika baadhi ya matukio, utoaji wa misaada ya kimataifa ya kibinadamu na ufadhili wa maendeleo unatokana na nia ya nchi kupitisha itikadi hizi, alisisitiza.

Askofu Mkuu Gallagher nchini Poland

 

13 Novemba 2024, 18:45