杏MAP导航

Tafuta

2024.10.28 Padre Antonio Spadaro na Papa Francisko. 2024.10.28 Padre Antonio Spadaro na Papa Francisko.  (Vatican Media)

Spadaro:Dilexit nos mdundo wa huruma kati ya vurugu na algorithm

Katibu wa Baraza la Kipapa la Utamaduni na Elimu anasisitiza kwamba katika Waraka wa hivi karibuni,Papa anaonesha maadili ya kimsingi kwa ulimwengu ulio na mizozo na kutokuwa na hisia: leo kipimo cha ‘ujanja’cha uwepo kinatawala.Kwa hiyo Papa anatualika kugundua upya kituo cha kuunganisha kinachotoa maana kwa kile tunachopitia moyoni na kujisikia kupendwa na Mungu.

Na Alessandro Di Bussolo na Angella Rwezaula- Vatican News.

Papa Francisko daima amejisikia kama 'mwenye dhambi aliyeokolewa kwa upendo wa Bwana' na katika Waraka wa Dilexit nos anatualika kugundua tena huruma yake, na kuelewa jinsi Bwana anavyozungumza nasi kupitia hisia za ndani.” Kwa hiyo, Padre Mjesuit wa Sicilia Antonio Spadaro, mkurugenzi wa zamani wa Gazeti ‘La Civiltà Cattolica’ kuanzia mwaka 2011 hadi 2023 na leo ni Katibu msaidizi wa Baraza la Kipapa la Utamaduni na Elimu, ameviambia tena vyombo vya habari vya Vatican kuhusu Waraka wa Kipapa wa hivi karibuni uliochapishwa tarehe 24 Oktoba 2024 kuhusu 'upendo wa Moyo wa Yesu. Hati  kama “kielelezo cha hali ya kiroho ya Papa Francisko na ufunguo wa kuelewa juu ya  upapa wake mzima. Padre Spadaro alikumbuka kuwa "alipitisha" kwa Papa maandiko juu ya Moyo Mtakatifu ambayo rafiki yake Padre Diego Fares, "mtoto wa kiroho" wa Jorge Mario Bergoglio(Papa Francisko) alikuwa akiandika kabla ya kifo chake, na ambayo iliongoza sura ya kwanza. Na kwamba kwa Waraka huu Papa anaomba ulimwengu, "ambao unapoteza moyo" na usikivu wote wa kibinadamu, kurejesha maadili yake ya msingi.

Padre Spadaro, unafikiri pia kwamba Waraka wa Dilexit nos ni hati muhimu ya Upapa na ufunguo wa kuelewa mafundisho yote ya Papa Francisko?

Waraka huu unazingatia hali ya kiroho ya Papa Francisko. Kwa hiyo, kwa namna fulani, tunaweza kusema kwa hakika kwamba ni ufunguo wa kuelewa upapa wote, kwa sababu ni ufunguo wa kuelewa utu wa kiroho wa Fransisko. Lakini tusisahau kwamba hatua muhimu sana ya upapa wake ilikuwa Mwaka wa Huruma. Kwa hiyo mada ya huruma, yaanI  ya moyo unaokaribiana, kama jirani, ayependa kwa undani, hisia, za ndani”, kama Mtakatifu Ignatius alivyosema, pia ni kitovu cha Utawala wa Papa Fransisko, ambavyo unasonga mbele kwa utambuzi. Utambuzi ni kujaribu kuelewa jinsi Bwana anavyozungumza kupitia hisia za ndani ambazo zimeelekezwa kwa moyo waziwazi. Kisha ningesema kwamba kwa hakika Waraka huu, lakini pia waraka wa Kitume wa Gaudete ed Esultate, ni kielelezo cha hali ya kiroho ya Papa Fransisko na kutoa nuru ya upapa nzima.

Katika kifungu hiki, ni lini na wapi tunaweza kupata uzoefu wa kiroho wa Jorge Mario Bergoglio na kukutana kwake binafsi na Kristo na upendo wake ‘kwa wote, kwa wote?

Papa Fransisko daima hujisikia kama mwenye dhambi aliyeokolewa na upendo wa Bwana. Nakumbuka, tangu mahojiano ya kwanza niliyofanya naye mwaka 2013, muda mfupi baada ya uchaguzi, alijifafanua hivi. Hivyo kipaumbele kinatolewa kwa upendo wa Bwana. Uongofu ni tunda la upendo huu. Ikiwa hakuna mawasiliano ya moja kwa moja, mtazamo wa upendo, ujuzi wa ndani wa Bwana wa kumpenda zaidi na kumfuata, kama Mtakatifu Ignatius alivyosema, hawezi hata kuwa na uongofu wa kweli. Kwa hivyo, kuandika Waraka  juu ya moyo ina maana kwamba kuingia katika moyo wa Kristo huturuhusu kuhisi kupendwa na moyo wa kibinadamu uliojaa mapenzi, hisia kama zetu. Hali ya kiroho ya Papa Fransisko, kwa maana hiyo, iko mbali sana na sura zisizo na mwili na zenye msimamo mkali. Anaamini kwamba hali ya kiroho inahusisha sana nafsi ya mwanadamu, hisia na mwelekeo wa kimwili wa mwanadamu.

Kwa hivyo, “Dilexit nos” ni onesho kwamba Papa Bergoglio sio fundisho linalolenga kijamii tu, kama wengine walivyoelewa?

Ningesema kwa ujumla kwamba mafundisho ya Papa Francisko hayalengi kitu chochote. Hakika imani ambayo haifasiri matendo imekufa, haina maana. Kwa hiyo ni wazi kwamba mwelekeo wa kijamii, mafundisho ya kijamii ya Papa Fransisko ni matunda ya moja kwa moja ya hali yake ya kiroho na pia ya kiroho ya Moyo wa Kristo. Baada ya yote, Papa Francis anasema waziwazi katika Waraka huu kuwa: ni lazima tuwe na huruma kwa dunia iliyojeruhiwa. Katika andiko hilo anaonesha Yesu akinyoosha mkono na kuponya. Na kwa namna fulani anaunganisha mafundisho yake ya awali na sura hii, kwa sababu katika Ndugu vifungo vyote vya kidugu vinawezekana kwa sababu tunakunywa, alisema Papa, kutokana na upendo wa Bwana. Ni shukrani kwa upendo huu kwamba tunaweza kuanzisha vifungo vya udugu, lakini pia kutunza nyumba yetu ya kawaida pamoja. Kwa hivyo asingefanya tofauti hii kati ya majisterio ya kijamii na majisterio ya kiroho. Hakika moyo ndio kitovu cha mambo ya kiroho na kijamii.

Ni muhimu kwamba, kwa sura ya kwanza, Papa anaandika kwamba aliongozwa na maandishi ambayo hayajachapishwa ya “Mtoto wake wa kiroho” Padre Diego Fares, ambaye alifariki mwaka 2022, ambaye alikuwa mwandishi wa Gazeti la 'La Civiltà Cattolica' chini ya uongozi wake. Je, una kumbukumbu gani za kujitolea kwake kwa Moyo Mtakatifu?

Diego alikuwa rafiki mpendwa sana, mwandishi mkuu wa La Civiltà Cattolica, ambaye alikuja hapa Roma baada tu ya kuchaguliwa kwa Papa Francisko, akiwa tayari kuacha kazi aliyokuwa akiifanya. Kazi yake huko Argentina ilikuwa mbili: kwa upande mmoja alifundisha falsafa katika Chuo kikuu, kwa upande mwingine alitunza malazi ya wagonjwa mahututi na watu wasio na makazi. Kwa hiyo maisha yake “yalikumbatiwa” na shughuli hizi mbili na sauti yake ya kiroho iliwekwa alama kwa utambuzi wa hisia za ndani, kwa hiyo ilikuwa na mizizi ndani ya moyo wa Kristo. Katika miezi ya mwisho ya maisha yake alitaka kuandika andiko juu ya moyo wa Kristo, ambalo alikuwa akilifanyia kazi. Nakala nzuri sana ambayo nilimpatia Papa, ambaye pia alijua kazi hii nzuri ambayo Diego alikuwa akifanya. Na Papa alitaka kuimarisha, kwa sababu alisikia katika maneno hayo ya Diego mwangwi wa kile ambacho yeye mwenyewe alihisi. Pia nataka kusema kwamba Diego aliingia katika Jumuiya ya Yesu wakati Papa Francisko alipokuwa Mkuu wa Kanda ya  Wajesuit nchini Argentina (mwaka 1975, ed.). Kwa hiyo ujuzi wao ulikuwa wa kina sana na ulidumu kwa miongo kadhaa.

Unafikiri ni kwa nini Papa Francisko alichagua wakati huu kuweka wakfu Waraka  kwa Moyo Mtakatifu wa Yesu? Labda kwa sababu ana wasiwasi, kama aandikavyo, kwamba "dini isiyo na kumbukumbu ya uhusiano wa kibinafsi na Mungu wa upendo" inasonga mbele na kwamba Ukristo unasahau “upole wa imani, furaha ya kujitolea kwa huduma, ari ya utume wa mtu na kwa kila mtu”?

Kwa upande mmoja, ninaamini sababu muhimu ni mtazamo kwamba jamii inapoteza moyo wake. Alisema, wakati fulani katika Waraka, kwamba "kuona bibi wakilia, bila hii kuwa isiyovumilika, ni ishara ya ulimwengu usio na moyo.” Anarejea vita, askari waliokufa, ukweli kwamba ulimwengu hivi sasa umegawanyika na una jeraha kubwa wazi. Na hii ni kutokana na kutokuwa na hisia, na ukosefu wa nia ya kutafuta ufumbuzi wa matatizo yanayotokea. Hivyo jamii inayopoteza moyo inahitaji kukumbushwa tunu zake msingi. Sababu ya pili ndiyo, nadhani ni kile ulichokuwa unasema, yaani, tunakuwa watumwa kutafuta soko, kwa mwelekeo wa "smart" wa kuwepo, kwa hiyo kwa ufanisi, kwa pande zote mbili badala ya zaidi ya silika, bure kabisa, bila breki. Tumepoteza kitovu cha kuunganisha kinachotoa maana kwa kile tunachopitia, yaani, moyo. Kwa hivyo wito huu ni wa kina na unajibu hitaji la nyakati zetu.

Hatimaye, katika waraka huo kuna ombi la kutokejeli usemi wa bidii wa watu wa Mungu ambao, katika ibada zao maarufu, wanatafuta kumfariji Kristo. Je, huruma kwa watu ina nafasi gani katika majisterio ya Papa Francisko?

Ni muhimu sana, kwa sababu imani rahisi, maarufu, inaoneshwa kwa njia ya ibada na picha. Moja ya sababu kwa nini Ukristo unaweza kuwa katika mgogoro ni kwa nini hauwezi tena kupata maneno na picha ya kusema yenyewe, kujieleza. Kwa hiyo ibada maarufu ya watu ni chanzo chenye dhahabu, tunaweza kusema, wa picha, wa maneno ya kujieleza, na hatimaye unahusishwa sana na hisia za kibinadamu zaidi. Kwa hiyo ni hali ya kiroho, ya watu, iliyounganishwa sana na historia na unyeti wa kibinadamu. Hisia ambazo ni za kiakili sana, za busara, zinahatarisha kumtenga mwanadamu kutoka katika ukweli wake mwenyewe. Imani inahatarisha kupotea kati ya mambo mengine kwa wajuzi wachache na kwa wasomi. Badala yake, ni kwa watu rahisi ndipo moyo mchangamfu wa imani hupatikana.

Padre Spadaro anaeleza Juu ya Waraka Mpya wa Kipapa:Moyo wa Upendo
29 Oktoba 2024, 11:23