杏MAP导航

Tafuta

2024.05.12 Kardinali Stephen Brislin. 2024.05.12 Kardinali Stephen Brislin.  (Alessia Giuliani / CPP )

Papa amemteua Kard.Brislin kuwa Askofu Mkuu wa Johannesburg

Papa Francisko amekubali king’atuka kwa Askofu Mkuu wa Johannesburg,nchini Afrika Kusini Askofu Mkuu Buti Joseph na wakati huo huo akamteua Kardinali Stephen Brislin,kuwa mkuu wa Kanisa hilo ambapo hadi uteuzi huo alikuwa Askofu Mkuu wa Kanisa Kuu katiliki la Cape Town nchini Afrika Kusini.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Jumatatu tarehe 28 Oktoba 2024, Mama Kanisa akiwa anakumbuka watakatifu Yuda Taddei na Mtakatifu Simoni, Baba Mtakatifu Francisko amekubali, kung’atuka kwa shughuli za kichungaji za Jimbo Kuu la Johannesburg Afrika Kusini iliyowakilishwa na Askofu Mkuu Buti Joseph Tlhagale, O.M.I. na wakati huo huo akamteua aliyekuwa Askofu Mkuu wa Kanika katoliki  la  Johannesburg nchini Afrika Kusini,  Kardinali Stephen Brislin, ambaye hadi uteuzi huo alikuwa Askofu Mkuu wa  Cape Town.

Kardinali Brislin, Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki la Cape Town, Kaapstad(Afrika Kusini), alizaliwa huko Welkom mnamo 24 Septemba 1956. Alihitimu  masomo yake ya awali katika Mtakatifu Inés na CBC, Welko. Alijiunga na Seminari ambako alisoma Falsafa katika  Cguo cha Mtakatifu Yohane Vianney, Pretoria na Taalimungu katika Taasisi ya Utume huko London. Tarehe 17 Oktoba 2006, Papa Benedikto XVI alimteua kuwa Askofu wa Kroonstad, Afrika Kusini na kusimikwa rasmi tarehe 28 Januari 2007.

Tangu Agosti 2024 amekuwa Rais wa SACBC

Kunako tarehe 18 Desemba 2009 alichaguliwa kuwa Askofu Mkuu wa Cape Town, na kusimikwa rasimi tarehe 7 Februari 2010, kwenye maadhimisho ya Mama Yetu wa Ndege kuelekea Misri, ambayo sikukuu ya mlinzi wa Jimbo Kuu la Cape Town. Kuanzia 2013 hadi 2019 alikuwa Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Afrika Kusini. Ameundwa na kutangazwa kuwa Kardinali na Papa Francisko katika Mkutano wa Baraza la Makardinali  tarehe 30 Septemba 2023, kwa kupewa Kanisa la Kirumi la Mtakatifu  Maria Domenica Mazzarello. Na tangu Agosti 2024  aliteuliwa tena kuwa Rais wa Baraza la Maaskofu Afrika Kusini (SACBC).

Papa na Uteuzi
28 Oktoba 2024, 16:44