杏MAP导航

Tafuta

2024.09.22 Kardinali Mario Zenari - Parokia ya Mtakatifu Maria wa Neema, Fornaci, Roma 2024.09.22 Kardinali Mario Zenari - Parokia ya Mtakatifu Maria wa Neema, Fornaci, Roma 

Zenari:Mabomu ya umasikini yanaua tumaini

Balozi wa Vatican nchini Siria,Kardinali Mario Zenari,katika mahubiri yake tarehe 22 Septemba 2024 alishirikisha mateso ya watu wa kisiria, katika Parokia ya Mtakatifu Maria wa Neema huko Fornaci,Roma ambalo pia ni shemasi wa Kanisa hilo.

Na Massimiliano Menichetti - Vatican

Siria inayoteswa, kama Papa Francisko anavyosisitiza mara nyingi, sasa imesahaulika na imeanguka kutoka katika rada ya habari. Shuhuda wa mwanga wa Kristo na matumaini yanayofifia katika nchi hiyo ni mjumbe wa kitume huko Damasco, Kardinali Mario Zenari, Balozi wa Vatican nchini Siria ambaye  Dominika tarehe 22 Septemba 2024  aliongoza Ibada ya Misa Takatifu  katika Parokia ya Roma ya Mtakatifu Maria wa Neema huko Fornaci, ambapo pia ni Shemasi wa Kanisa hilo, kama ambayo kila Kardinali hupewa  Kanisa la Kirumi. Katika mahubiri yake na katika kukutana na waamini wa parokia baada ya sherehe hiyo alishirikisha mateso ya watu wa Siria ambao sasa wameingia katika mwaka wa kumi na nne wa vita na "wamechoka na kujitahidi katika kuona mwanga wa siku zijazo". Vita hivyo vimeua watu 500 elfu zaidi ya milioni 7 wamekimbia makazi yao na zaidi ya milioni 5 wamekimbilia nchi zingine. Kulingana na Umoja wa Mataifa, watu milioni 16.7 wanahitaji msaada wa kibinadamu na karibu milioni 13 wana uhaba mkubwa wa chakula.

Kardinali Zenari, Balozi wa Vatican nchini Siria
Kardinali Zenari, Balozi wa Vatican nchini Siria

Kardinali Zenari alizungumza juu ya misalaba mingi, "midogo na mikubwa", ambayo kila mtu hubeba katika maisha yake na msaada ambao Kristo hutoa, kisha akawaonesha wale walioko Shamu. Alirejea akiwa na kumbukumbu yake ya miaka ya nyuma, kwa taswira iliyowekwa akilini mwake ya Wasiria zaidi ya milioni moja ambao walikuwa wamejipanga kuepuka vurugu, chini ya mvua na theluji, wakiwa wamebeba kile walichoweza kama vile “Njia ya Msalaba”kwa kilometa kwa muda mrefu." Kisha taswira nyingine, ile ya Ijumaa Kuu ambapo mabomu yaliangukia mji wa Homs na ambapo Msakristi alimuuliza padre, Michele, mahali ambapo liturujia ingepaswa kutayarishwa, katika mazingira ambayo kila kitu kiliharibiwa na makanisa kuharibiwa. “Padre Michele aliamuru kuchukua kamba ndefu na kuiweka pande zote za vitongoji vilivyoharibiwa na vita na kuweka maandishi ya Kalvario katikati ya eneo. Kardinali alisisitiza: “Leo  hii kamba ni ndefu zaidi na imeenea kwa kilomita na kilomita na inakumbatia Mashariki ya Kati nzima.” Aidha alisema: "Niliona uharibifu mwingi, vifo, watoto waliokatwa viungo, mateso mengi katika miaka ya mapigano makali. Sasa bomu la umaskini limelipuka jambo ambalo haliacha matumaini kwa wakazi."

Kardinali Zenali, Balozi wa Kitume chini Siria.
Kardinali Zenali, Balozi wa Kitume chini Siria.

Kardinali alithibitisha kwamba vikwazo vilivyotekelezwa dhidi ya utawala wa Siria vina madhara makubwa sana kwa idadi ya watu: "Wakati wa vita kulikuwa na mwanga, sasa hakuna umeme na giza linaifunika nchi." Kuna ukosefu wa dawa, chakula, vitu vya matumizi ya kila siku, benki haziwekezi, fedha zimesimama, kama ilivyo kwa  upande wa elimu. Idadi ya watu inaendelea kukimbia, umaskini umekithiri. Kardinali Zenari alieleza “Leo Daktari anapata euro 20 kwa mwezi.” Ni kujifunza inapoweza na kufikiria kuhama." Katika hali hii, Kanisa liko mstari wa mbele katika kutoa misaada, kufariji na kuanzisha kila hatua, zikiwemo za kidiplomasia, ili kurudisha nyuma anguko hili la shimo la kina. Kulingana na Umoja wa Mataifa, karibu watu 500 huondoka nchini kila siku. Kilio cha Balozi wa  Damasco hakiwezi kubaki kiziwi katika sayari iliyoharibiwa na migogoro. Ujenzi wa ulimwengu wa kidugu, msaada, na amani, wenye uwezo wa kuanzisha miradi mbali mbali ya kisiasa na mtu katikati inawezekana, sio tu ya kufikiria na inatekelezwa kwa dhamira ya wengi. Hatuwezi kusahau Siria, hatuwezi kuangalia upande mwingine ikiwa wahamiaji wanakufa baharini, hatuwezi kukubali udikteta na migogoro. Kila mtu, katika kila eneo, ameitwa kujenga njia za mazungumzo, kukutana na amani.

Kardinali Zenari,Balozi wa Vatican nchini Siria atoa ushuhuda wa Nchi hiyo
24 Septemba 2024, 10:22