Kard.Parolin mjini New York kwa Mkutano Mkuu wa 79 wa Umoja wa Mataifa
Vatican News
Kuanzia Dominika tarehe 22 Septemba hadi Jumatatu tarehe 30 Septemba 2024, Katibu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin, atakwenda New York kushiriki Kikao cha 79 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Hii ilijulikana kutoka katika chapisho la Umoja wa Mataifa huko New York, Marekani. Kardinali Parolin pia ataadhimisha Misa kwa ajili ya kumbukizi ya miaka 60 ya Ubalozi wa Vatican katika Umoja wa Mataifa.
Mkutano Mkuu wa 79 wa Umoja wa Mataifa utajikita katika kukuza masuluhisho ya pande nyingi kwa kuzingatia Mkataba wa Umoja wa Mataifa na kuongeza kasi ya juhudi za kutekeleza Ajenda ya 2030 ya Malengo ya Maendeleo Endelevu. Miongoni mwa vipaumbele ni uungaji mkono wa amani na usalama wa kimataifa, kukuza maendeleo endelevu, mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, upotevu wa viumbe hai na uchafuzi wa mazingira.