杏MAP导航

Tafuta

Katibu wa Vatican akiwa katika Mkutano  wa 79 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa,New York Marekani kuhusu "siku zijazo." Katibu wa Vatican akiwa katika Mkutano wa 79 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa,New York Marekani kuhusu "siku zijazo."  (ANSA)

Vatican,Kard.Parolin:Afya sio anasa!Ulimwengu unaowatupilia mbali wagonjwa!

Kama Papa alivyosema ikiwa hatutajitolea kukabiliana na ukosefu wa usawa katika huduma za afya,tunakubali ukweli wa uchungu kwamba sio maisha yote ni sawa na afya hailindwi kwa kila mtu kwa njia sawa.Ni katika Hotuba ya Katibu wa Vatican,katika Mkutano wa Ngazi za Juu kuhusu ukinzani wa viua viini(antimicrobial)uliofanyika tarehe 26 Septemba 2024 huko New York,Marekani.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kardinali Pietro Parolin,  Katibu wa Vatican akiwa huko New York Marekani kushiriki Kikao cha 79 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa tangu tarehe 22 Septemba, Alhamisi tarehe 26 Septemba  2024alitoa tamko lake katika Mkuno wa Ngazi za Juu kuhusu upinzani dhidi ya vijidudu (AMR). Katika tamko lake alisema kuwa &苍产蝉辫;“Vatican inakaribisha kufanyika kwa Mkutano wa Ngazi ya Juu kuhusu ukinzani wa viua viini(antimicrobial). Azimio lililopitishwa tarehe 26 Septemba 2024 linaonesha ahadi za kisiasa ambazo lazima zifuatwe na hatua za wakati katika  ngazi zote za kupambana na upinzani dhidi ya vijidudu (AMR) na kuzuia matokeo yake yanayoweza kuwa mabaya. “ Kardinali aidha alisema kuwa “Mwitikio kwa AMR lazima uhusishe sekta nyingi, sio dawa tu bali pia zile zinazohusisha wanyama na mazingira. Hii inaakisi kile ambacho Papa Francisko alikiita “ikolojia fungamani”, ambayo “haiwezi kutenganishwa na manufaa ya wote” na inahitaji utunzaji unaowajibika wa mazingira na utunzaji wa viumbe hai wote.”

Wanadamu ni mashuhuri kati ya viumbe hai

Vatican inasisitiza kwamba “Wanadamu ni mashuhuri kati ya viumbe hai na kwa hivyo ustawi wa mwanadamu lazima uwe lengo kuu la juhudi zote za kupambana na AMR. Kuzuia magonjwa ya kuambukiza ni muhimu katika kukabiliana na AMR. Hii inalazimu utengenezaji wa chanjo na uendelezaji wa mazoea ya usafi. Jamii nyingi maskini hazina huduma ya maji, usafi wa mazingira na usafi (WASH) katika vituo vya huduma za afya.”&苍产蝉辫; Hata hivyo, kuna juhudi nyingi muhimu katika maeneo haya ambazo zinapaswa kuungwa mkono. Mnamo 2020 Baraza la Kipapa la Kuhamaisha Maendeleo Fungamanai ya Binadamu ilizindua mpango ambao tayari umewezesha uboreshaji wa hali ya WASH katika vituo vya afya vya Kikatoliki Afrika yote, Asia na Carribien. Kama Papa Francisko alivyosema ikiwa hatutajitolea kukabiliana na ukosefu wa usawa katika huduma za afya, “tunakubali ukweli wa uchungu kwamba sio maisha yote ni sawa na afya hailindwi kwa kila mtu kwa njia sawa.”

Wagonjwa maskini hawawezi kutengwa na matibabu ya lazima

Kardinali Parolini aidha alisema kuwa “Wagonjwa maskini hawawezi kutengwa na matibabu ya lazima, ya kutosha na ya bei nafuu, au kutarajiwa kufanya mazoezi ya usafi bila maji safi - matatizo ambayo pia huchangia upinzani wa(antimicrobial) upinzani dhidi ya vijidudu (AMR). Kwa njia hiyo, ili kupambana vilivyo na AMR, umaskini na matokeo yake, ikiwa ni pamoja na ukosefu wa huduma za afya na hali duni ya maisha, lazima kushughulikiwa. Kazi kubwa inasalia kufanywa ili kukabiliana na AMR, na kukuza sera na rasilimali zinazohitajika ili kuhakikisha “haki ya kimsingi ya kila mtu ya kupata huduma za afya za kimsingi na zinazostahili. Afya sio anasa! Ulimwengu unaowatupilia mbali wagonjwa, ambao hauwasaidii wale wasioweza kumudu matunzo, ni ulimwengu wa kijinga usio na wakati ujao.”

27 Septemba 2024, 14:12