Papa katika CO28,mpango rasmi wa ziara ya Dubai umechapishwa!
Vatican News
Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican imechapisha tarehe 9 Novemba 2023 ratiba rasmi ya ziara fupi ya Baba Mtakatifu Francisko huko Dubai, kuanzia tarehe Mosi hadi 3 Desemba 2023, wakati wa Mkutano wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi au (COP28). Katika Mkutano huo, Papa atakuwa na hotuba moja tu, salamu na mikutano ya kibinafsi katika Nchi mbili. Kwa hiyo Baba Mtakatifu anatarajia kuondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Fiumicino, Roma siku ya Ijumaa tarehe 1 Desemba, saa 5.30, kuelekea Dubai. Na atatua katika jiji la Emirati saa 2.25 usiku katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa hadi Uwanja wa Ndege wa Dubai/ kituo cha Dunia, ambapo Papa atakaribishwa.
Hotuba ya COP28
Kiini cha ziara yake nzima kitakuwa siku ya Jumamosi tarehe 2 Disemba 2023 ambapo Papa Francisko atazungumza kwenye Mkutano wa COP28, kabla ya Wakuu wa Mataifa mbalimbali kukusanyika katika mji wa Expo. Papa atawasili saa 4.00 asubuhi na kutoa hotuba yake. Majira ya saa 4.30, kwa mujibu wa ratiba tunasoma kuwa, mikutano ya kibinafsi ya nchi mbili imepangwa, ambayo itaendelea katika kikao cha mchana kuanzia saa 9.30 alasiri.
Uzinduzi wa Banda la Imani
Siku ya Dominika tarehe 3 Desemba 2023, saa 3.00 asubuhi Papa Francisko atazindua "Banda la Imani" katika Jiji la Expo, ambalo lina malengo makuu sita ya COP28: kuhamasisha nguvu za dini na viongozi wa kidini kama mawakala wa mabadiliko kwa hatua ya tabianchi; kuakisi hatua madhubuti za taasisi za kidini na jumuiya ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa kutumia viashirio vinavyoweza kupimika na utaratibu wa ufuatiliaji; kukuza muungano wa kimataifa wa viongozi wa imani wanaofanya kazi pamoja kwa ajili ya hatua za tabianchi; kuhimiza viongozi wa kidini kushiriki katika majadiliano ya kisiasa na kuhamasisha hali ya tabianchi miongoni mwa wajumbe wa kisiasa; kufikia upatanisho wa kihistoria nyuma ya wito wa hatua ya tabianchi; kuunganisha na kuongeza hatua ya pamoja ya watendaji wa kidini waliopo kwenye COP 28. Katika hilo salamu kutoka kwa Papa zinatarajiwa katika hafla hiyo.
Kurudi Roma
Saa 4.15 Baba Mtakatifu Francisko atahamishiwa kueleka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dubai/Kituo cha Dunia kwa ajili ya afla za kuaga. Kuondoka kuja Roma kumepangwa sa 4.45 asubuhi; wakati kuwasili, tena katika Uwanja wa Kimataifa Fiumicino Roma, unatarajiwa saa 8.40 alasiri.