杏MAP导航

Tafuta

2023.10.20 Sinodi ya Maaskofu inaendelea hadi 29 Oktoba 2023. 2023.10.20 Sinodi ya Maaskofu inaendelea hadi 29 Oktoba 2023.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Sinodi yatoa wito kwa wasafirishaji wa silaha kugundua tena hisia za kibinadamu

Wakati wa mkutano wa Oktoba 20 na waandishi wa habari kuhusu maendeleo ya sinodi,wajibu wa maaskofu na uwajibikaji wa walei katika Kanisa, mamlaka yenye uzoefu kama huduma ilijadiliwa:“Askofu ndiye analo neno la mwisho, lakini si pekee wa kusema.Sinodi "inaweza kusaidia kuzuia unyanyasaji kwa sababu inahusishwa na kusikiliza na mazungumzo."

Vatican News.

Mamlaka, ambayo katika Kanisa ni huduma”ambayo inatekelezwa bila viatu, na suala la unyanyasaji lilikuwa miongoni mwa mada zilizozungumziwa wakati wa Kusanyiko Kuu la Kumi na Tatu  na kwa washiriki (341 walikuwapo) na la Kumi na Nne ( walikuwa 343), lililofanyika Alhamisi alasiri 19 Oktoba  na Ijumaa asubuhi, 20 Oktoba  kila mara kulingana na hali sawa ya uingiliaji kati wa vikundi vidogo vya mduara ikifuatiwa na uingiliaji wa mtu binafsi. Ndivyo ilivyoripotiwa mnamo Ijumaa alasiri tarehe 20 Oktoba kwa waandishi wa habari katika Ofisi za Vyombo vya habari Vatican.

Mamlaka si kutawala bali ni huduma

Akirejea uingiliaji kati alasiri 20 Oktoba kwenye sehemu B3 ya Instrumentum laboris (Kitendea kazi – ambayo ina kichwa: ‘Ushiriki, wajibu na mamlaka’, rais wa Tume ya Habari ya sinodi , Dk. Paolo Ruffini, na Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano alieleza kwamba dhamira ya Kanisa ya kuepuka utawala wa kimabavu ilikuwa imezungumzwa  tena. Mamlaka si kutawala bali ni huduma, usemi ambao umeundwa katika: mamlaka unatekelezwa bila viatu. Kwa hiyo yule “aliye na mamlaka”, kwa mujibu wa vikundi vidogo vidogo walibainisha ni“lazima asidhibiti kila kitu bali awe na uwezo wa kushirikishana”; kwa upande wa Askofu walibainisha kwamba, ana neno la mwisho lakini hana neno  pekee yake.’ Miongoni mwa mada zilizojadiliwa, ni “nafasi ya wachungaji katika kuwahudumia maskini”, pia kwa mtindo wa sala iliyoongozwa Alhamisi 19 Oktoba usiku na Papa Francisko katika Uwanja wa Mtakatifu Petro kwa ajili ya wahamiaji na wakimbizi. Ni lazima tuzingatie "kilio cha wale wanaoteseka mitaani", tulibainisha katika hatua'. Zaidi ya hayo, kwa mujibu wa Dk. Paolo Ruffini aliliripoti kuwa, "maaskofu lazima waitishe uongofu wa moyo ili hisia za ubinadamu zifufuliwe kati ya wale ambao, kupitia ulanguzi wa silaha, wanachangia "vita ya tatu ya ulimwengu" ambayo husababisha mamilioni kuteseka.

Wajibu wa pamoja katika Kanisa

Wajibu wa pamoja ni mojawapo ya maneno ambayo yamesikika mara nyingi katika uingiliaji kati, na imeeleweka kama ushirikishwaji na uratibu wa misaada, kwa mujibu wa Dk. Paolo Ruffini. Katika suala hilo, umuhimu wa kukuza takwimu, ujuzi na juu ya yote dhamira ya walei ilisisitizwa katika kazi hiyo. Mkuu wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano alitaka pia kufafanua swali la idadi ya washiriki katika Sinodi kuwa : kuna 365 pamoja na Papa. Akikumbusha mbinu tofauti za ushiriki, ambapo Dk. Paolo Ruffini alibainisha kuwa kwa jumla, karibu watu mia moja zaidi wanahusika  na  ambayo inafanya idadi hiyo kufikia 464 - lakini uwepo wao hauhesabiwi katika mawasiliano rasmi. Pia alifafanua kuwa Sekretarieti kuu inatoa kipaumbele kwa wale ambao bado hawajazungumza. Kwa mujibu wa Sheila Pires, Katibu wa Tume ya Habari, baadaye alisema kwamba baadhi ya wajumbe wa Mkutano huo walikuwa wakionya dhidi ya ukasisi, hata miongoni mwa walei, kwa sababu “umesababisha matumizi mabaya ya madaraka, dhamiri, kiuchumi na kingono. Dhuluma hizi, alisisitiza, zimesababisha Kanisa kupoteza uaminifu, kiasi kwamba utaratibu wa kudhibiti ni muhimu. Sheila Pires Sinodi, alisema, “hii inaweza kusaidia kuzuia unyanyasaji kwa sababu ni mchakato unaohusiana na kusikiliza na mazungumzo.”

Marekebisho ya lazima katika Kanisa

Kuhusu mageuzi, kulikuwa na mjadala wa mabadiliko muhimu ili kufikia uwazi zaidi wa miundo ya kifedha na kiuchumi, marekebisho ya sheria ya kanuni na pia ya ‘majina’ fulani ambayo yamekuwa ya kutofautisha. Kuhusu sinodi, uharaka wa kuimarishwa kwa miundo iliyopo tayari- kama vile mabaraza ya wachungaji - ilisisitizwa, kwa uangalifu ili kutokubali ubadhirifu wa washiriki wa Mkutano. Hatimaye, Sheila Pires alidokeza umuhimu wa kusimama kidete  pamoja na vijana katika mazingira ya kidijitali, mahali pa kweli pa utume  wa  kuwaleta pamoja wale walio pembezoni. Kiukweli, ni juu ya kukutana na vijana hawa mahali walipo tayari, ambayo ni kusema katika mitandao tofauti ya kijamii,alihitimisha.

Askofu Gru?as: malezi na uongofu

Askofu Mkuu wa Vilnius, Rais wa Baraza la Mabaraza ya Maaskofu wa Ulaya na Baraza la Maaskofu wa Lithuania, alichukua nafasi ya kwanza kujadili mkutano wa bara mnamo Februari huko Prague. Kulingana na Askofu Mkuu  Gintaras Gru?as, alisema  ni “fursa chanya sana ya mazungumzo na kushiriki kiroho”, shukrani ambayo wachungaji kutoka nchi 45 tofauti waliweza kuzungumza na kukabiliana pamoja kutoka kwa mitazamo tofauti. Kisha akiibua kazi ya sinodi, Askofu Mkuu Gru?as alisisitiza kiini cha mada ya malezi kama “njia ya kuwa Kanisa, ya kuishi pamoja, ya kupata ushirika.” Uzoefu wa sinodi yenyewe unafanya haya yote: “licha ya uchovu wa siku hizi,” alisema, “tuna nguvu kubwa kwa sababu, ingawa tunatoka nchi mbalimbali, tunatambua kwamba tuna mambo mengi kwa pamoja: zaidi ya yote, tunapata nguvu nyingi, lakini tunapata nguvu nyingi katika imani”. Jambo jingine muhimu lililosisitizwa na maaskofu ni uwongofu wa moyo, nia ya “kukua kama Kanisa” kutoka katika shauku ya  “kubadili mawazo”.

Sr. Fadoul: kati ya mateso na matumaini

Sr. Houda Fadoul, mwenye asili ya Siria, ambaye mwaka 1993 alijiunga na jumuiya ya watawa ya ibada ya Wasiria-Katoliki ya Deir Mar Moussa iliyoanzishwa na Padre Paolo Dall'Oglio, kisha alizungumza. Mtawa - ambaye anashiriki katika kazi kama shahidi wa mchakato wa sinodi kwa Makanisa ya Mashariki na Mashariki ya Kati, alizungumza juu ya uzoefu wake wa kibinafsi na wa kikanisa, uliowekwa alama na matukio makubwa kama vile vita, janga, tetemeko la ardhi. Jimbo lake pia lilikaa bila askofu kwa miaka mitatu na padre mpya, ambaye amewasili hivi karibuni, alijaribu ‘kurekebisha’ kwa kuwashirikisha vijana hasa na pia kumwalika Askofu mtaalam wa Lebanon kukutana na sehemu tofauti za jumuiya.  Kuhusu sinodi, mtawa huyo  aliibua "wakati mzuri sana wa kubadilishana" ambao unakuza mvutano kuelekea umoja na kushiriki kunapendekezwa katika sala. Kila mada, kiukweli, inakaribia kwa njia ya "kutembea pamoja": kuna mahali pa kuanzia, njia, lengo la kufikia.

Askofu Mkuu wa Tokyo: kwa macho ya Caritas

Askofu Mkuu  Tarcisio Isao Kikuchi - mmisionari wa Verbite, askofu mkuu wa Tokyo, rais wa Caritas internationalis, rais wa Baraza la Maaskofu wa Japan, katibu mkuu wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Asia,  alisisitiza jinsi ilivyo vigumu kwa Wajapan kuzungumza katika kundi, kwa sababu wanapendelea, kulingana na mtindo wao wenyewe, ukimya. Hii ndiyo sababu, alibainisha, “mjadala tunaofanya siku hizi ni muhimu sana. Katika makusanyiko ya bara, tulikuwa tayari tumeanza kutumia hali ya vikundi vidogo, kuzunguka meza, na mikutano iliyoandaliwa huko Asia ambayo ilitutayarisha vyema zaidi kwa ajili ya Sinodi.” Kwa kushiriki katika vikundi vidogo vitano, alikumbuka Askofu Mkuu, “nilipata fursa ya kuona tofauti katika umoja wa Kanisa, bila kusahau kwamba uwepo wake ni wa ulimwengu wote. Lugha inayotumiwa katika mikutano, alisisitiza, “kiukweli  ni ile ya taalimungu ya ulimwengu wote, hata ikiwa suluhisho moja haliwezi kuwa halali kwa wote. Hii ni kwa sababu huko Asia kuna lugha nyingi sana na ukweli mwingi: hatuwezi kuchagua suluhisho moja la kutembea pamoja, kwa sababu sinodi pia inamaanisha heshima kwa tamaduni za wenyeji. Kisha alizungumza kuhusu huduma yake kama rais wa Caritas Internationalis, akisisitiza kwamba “kila Caritas ni ya msingi katika safari ya sinodi ya Kanisa.” Mashirika yote, alisisitiza, yana utambulisho wao wa Kikatoliki, yanashirikiana kikamilifu na washirika mbalimbali na pia yana thamani ya kiekumeni na ya kidini. ‘Sinodi hiyo inaonekana katika mataifa tofauti ya wale wanaoongoza shirika hili na wale wanaofanya kazi mashinani, katika sehemu zote za dunia,’ alimalizia.

Sr. Barron: Sinodi ya Asili ya Kiafrika

Sr  Mary Teresa Barron wa Ireland, Mkuu Shirika la  Masista wa Mama Yetu wa Mitume, rais wa Umoja wa Mama wakuu Kimataifa, alianzisha uingiliaji kati wake kwa kuibua msemo wa Kiingereza: “Hakuna mtu anayesoma kitabu kama hicho sawa mwingine.”  Kwa hiyo “Tafakari juu ya Sinodi,” aliamini, “iliniongoza kuona na kupata uzoefu wa mambo kulingana na uzoefu wangu kama mtawa, niliyekomaa katika Afrika Mashariki katika parokia ya vijijini, ambako niliishi uzoefu wa kwanza wa Kanisa la Sinodi, kama “kijana. Kanisa lenye mapadre wawili kwa vijiji 35 na katekista mmoja kwa eneo kubwa la nusu ya Ireland.” Sinodi inayopatikana katika vikundi vidogo, alieleza , ni sawa na ile iliyozoeleka huko Afrika “katika jumuiya, pamoja na waamini walei, kila Dominika nje ya vibanda vya udongo, tuliketi katika mduara kufanya maamuzi pamoja”, hata na watu ambao “hawakuwa na elimu na tulishirikishana imani kutoka ndani ya mioyo yetu. Lakini kila sauti ilikuwa na uzito sawa.” Sr. Barron kisha alipendekeza “kusikiliza zaidi makanisa machanga ambapo ushiriki wa chinichini ni mkubwa” na pia alithibitisha kwamba maisha ya kitawa ndani ya  Shirika lake yanategemea sinodi.

Kila mtu ana nafasi yake katika Kanisa

Akijibu maswali ya waandishi wa habari, Sr  Fadoul alizungumzia mchango wa ushuhuda wa maisha ya kawaida kuhusu sinodi. Alikumbuka sana kwamba hakuwa amewaacha Wakristo wa Siria pamoja na jumuiya yake, kwa kuwasaidia katika sala, kwa kuwafanya wahisi mshikamano. Aliunga  mkono Sr  Barron, ambaye aliakisi ushiriki wa  Mama Wakuu wa Mashirika  katika mchakato wa sinodi. Kwa upande mwingine, aliongeza, maisha ya kuwekwa wakfu yanatambua umuhimu wa malezi ili kuelewa jinsi ya kuishi sinodi. Sr Barron alirejea juu ya mafunzo ya mtandaoni, ambayo ni muhimu katika kupanua kushiriki na kujenga jumuiya.’

Tafakari juu ya Ushemasi wa kike

Katika kujibu swali kuhusu ushemasi wa kike, Sr Barron alibainisha kuwa suala hilo liko kwenye ajenda ya utambuzi wa sinodi. Ni sifa ya uzuri wa Kanisa Katoliki kwamba kuna maoni tofauti, lakini wakati yanajadiliwa, aliongeza, haitakuwa sawa kuzungumza nje ya nafasi hiyo. Katika suala hili, Sr. Fadoul alisisitiza kwamba kila mtu lazima achukue nafasi yake katika Kanisa, wanaume na wanawake, kwa kujifunza kutumia karama za Bwana. Askofu Mkuu Gru?as aliongeza kuwa mjadala juu ya huduma mbalimbali katika Kanisa ni sehemu ya mazungumzo haya mapana sana ndani ya Sinodi. Kwa kawaida, alisisitiza, tunatafuta jibu kama ndiyo au hapana, nyeusi au nyeupe. Ni wazi kuwa kuna tofauti za maoni ambazo pia hutegemea muktadha wa kiutamaduni, kwa hivyo ni mapema sana kufanya uamuzi katika hatua hii.”

Sinodi inaendelea mjini Vatican

Tafakari ya Sinodi huko Ulaya na Asia

Askofu Mkuu Gru?as pia alionesha kwamba marais wa Mabaraza ya  maaskofu wametafakari juu ya idadi fulani ya miundo ambayo tayari ni sinodi katika sheria za kanoni na ambayo inaweza kutekelezwa kwa ufanisi sasa. Askofu Mkuu wa Tokyo alielezea kwamba wakati wa janga la uviko hapakuwa na fursa nyingi za kuleta watu pamoja ili kutembea kwa njia ya sinodi, na kwa hivyo njia ya mtandaoni  ilichaguliwa. Kisha alitoa wito wa kutafakari ukweli kwamba ikiwa kweli tunataka kuwashirikisha walei, lazima tuzingatie shughuli zao na familia zao. Akijibu swali la mwandishi wa habari wa Ufilipino kuhusu pendekezo lililomo katika hati ya bara la Asia juu ya ukarimu na ushirikishwaji katika Kanisa, Askofu Mkuu wa Tokyo alirudia kueleza kile kilichopendekezwa katika vikundi vidogo, ambayo ni desturi ya mashariki ya “kuvua viatu ili kuingia ndani nyumba” kama ishara ya kukaribishwa na ukarimu.”

Mchakato wa sinodi, muhimu zaidi kuliko maamuzi

Katika kujibu swali la mwisho juu ya maamuzi ya mwisho ya Mkutano wa Maaskofu,  Askofu Gru?as alisisitiza umoja wa Mkutano Mkuu "juu ya njia ya sinodi". Kwenye mada maalum, “Siamini kuwa katika hatua hii, au hata kabla ya 2024, kutakuwa na maamuzi ya mwisho”. Lakini ikiwa tutakua na kuishi katika sinodi, yatakuja, kwa sababu hatutafuti hitimisho la kweli, hakuna wazo la awali la nini Sinodi hii inapaswa kuwa. Ingawa kila mtu anataka maamuzi, mchakato ni muhimu zaidi kuliko maamuzi.” Hatimaye, Sr Fadoul aliongeza kwamba “kusikiliza, kushiriki na utambuzi ni maneno muhimu kwa Kanisa zima.”

 

21 Oktoba 2023, 15:36