Padre Radcliffe:Mungu anaonekana na kiu katikati yetu!
Na Angella Rwezaula, Vatican.
Katika mkutano mkuu wa 4 kwa Washiriki wa Sinodi inayoendelea mjini Vatican katika Ukumbi wa Paulo VI, Jumatatu tarehe 9 Oktoba 2023 tafakari ya Padre Timothy Radcliffe OP imeongozwa na kifungu cha Injili kuhusu Msamaria katika kisima (Yh 4,7-30. Padre Radcliffe amesema kuwa leo tunaanza kutafakari kifungu cha B. I cha ’Instrumentum Laboris, kinachohusu “Ushirika unaomeremeta.” Mada iliyoibuka mara kwa mara katika mikutano yao kwa Juma lililopita ilikuwa ni mafunzo. Kwa hiyo je ni jinsi gani wote wanaweza kufunzwa katika ushirika ambao unafurika katika utume? Katika sura ya 4 ya Injili ya Yohane anazungumza kuhusu mkutano wa Yesu na mwanamke kisimani.
Mwanzo wa sura hiyo alikuwa peke yake, ambapo inaonesha picha ya upweke. Mwishoni yeye anabadilika kwa mara ya kwanza ya kuwa muhubiri wa Injili, na kama ilivyokuwa mhubiri wa kwanza wa ufufuko atakuwa mwanamke, Maria Magdala, Mtume wa Mitume: Kwa hiyo Wanawake wawili wanazindua awali ya yote kuhubiri habari njema kuwa Mungu alifika kwetu, na baadaye ufufuko. Ni jinsi gani Yesu anaweza kushinda upweke? Mkutano unafunguliwa na maneno mafupi matatu kwa lugha ya kigiriki: “Ninaomba maji ya kunywa”. Kwake Yesu ana kiu lakini siyo ya maji tu. Injili yote ya Yohane imezungukia juu ya kiu ya Yesu. Ishara ya kwanza, aliyoitoa ya divai kwa waalikwa wenye kiu katika Harusi ya Kana. Ni karibu na maneno yake ya mwisho wakati akiwa msalabani ni “Nina kiu”.
Baadaye akasema: “kila kitu kimetimia” na akafa. Mungu anaonekana kati yetu kama yeye aliye na kiu zaidi ya yote kwa ajili ya kila mmoja wetu. Padre Radriclieffe alisema , Geoffrey Preston OP Mwalimu wake alipokuwa mwanafunzi, aliandika hivi: “Wokovu ni kuhusu Mungu kututamani na kuteswa na kiu kwa ajili yetu; Mungu anatutaka zaidi ya vile tunavyoweza kumtaka.” Julian wa Norwich, mtaalamu wa fumbo wa karne ya kumi na nne, alisema, “Tamaa na kiu ya kiroho kwa ajili ya Kristo hudumu na itadumu hadi siku ya hukumu.” Kwa hiyo Mungu alikuwa na kiu sana kwa mwanamke huyo aliyekuwa na dhambi hata akawa mwanadamu. Alishirikishana, naye kile ambacho ni cha thamani zaidi, jina la Mungu: "MIMI NDIYE, anayesema nawe". Ni kana kwamba Umwilisho ulifanyika kwa ajili yake hasa. Yeye pia alijifunza kuwa na kiu.
Kwanza kabisa kwa maji, ili asije kisimani kila siku. Kisha aligundua kiu kikubwa zaidi. Hadi sasa ilipita kutoka kwa mwanadamu hadi kwa mwanadamu. Na kwa hiyo aligundua ile ambayo alikuwa akiitaka siku zote bila kujua. Kama Romano Mwimbaji alivyosema, mara nyingi maisha ya watu ya kujamiiana yasiyo ya kawaida ni kupapasa baada ya kiu yao kuu, ile ya Mungu. Lakini Bwana hutungoja kwa subira kwenye visima vyetu, akitualika tuwe na kiu zaidi. Kwa hiyo kinachotutenga sisi sote ni kunaswa na tamaa ndogo ndogo, katika kuridhika kidogo, kama kuwapiga wapinzani wetu au kuwa na hadhi, kuvaa kofia maalum! Kulingana na mapokeo ya mdomo, Mtakatifu Thomas Aquinas alipoulizwa na dada yake Theodora jinsi ya kuwa mtakatifu, alijibu kwa neno moja: Velle! Uitake! Yesu mara kwa mara anawauliza watu wanaomkaribia hivi: “Je, wataka, ?”; "Ninaweza kukusaidia vipi?"
Bwana anataka kutupatia utimilifu wa upendo. Je, tunautaka?Kwa hivyo mafunzo yetu katika sinodi yanamaanisha kujifunza kuwa watu wenye shauku, waliojazwa na hamu kubwa. Pedro Arrupe, jemadari mkuu wa ajabu wa Wajesuit, aliandika hivi: “Hakuna jambo linalofaa zaidi kuliko kumpata Mungu, yaani, kupendana kabisa na kwa uhakika. Unachopenda, kinachovutia mawazo yako, kitaathiri kila kitu. Kitaamua nini kinakuondoa kitandani asubuhi, nini cha kufanya jioni, na jinsi gani unavyotumia mwisho wa Jumba lako, kile unachosoma, unayemjua, ni nini kinachovunja moyo wako, na kile kinachokushangaza kwa furaha na shukrani. Kuingia katika upendo, kukaa katika upendo na kila kitu kitaamua." Mtu mwenye shauku, Mtakatifu Augustino, alipaza sauti kuwa: "Nimekuonja na sasa nina njaa na kiu kwa ajili yako; ulinigusa nami nikawaka moto kwa ajili ya amani yako." Kwa hivyo, mafunzo katika ushirika unaomeremeta" humaanisha kujifunza kiu na njaa kwa undani zaidi. Tuacha tuanze na matamanio yetu ya kawaida.
Padre Redicliffe ametoa ushuhuda kuwa: Nilipokuwa mgonjwa wa saratani hospitalini, sikuruhusiwa kunywa chochote kwa muda wa majuma matatu hivi. Nilijawa na kiu kali. Hakuna kilichowahi kuonja vizuri kama glasi hiyo ya kwanza ya maji, hata kuwa bora kuliko glasi ya whisky! Lakini polepole niligundua kwamba kulikuwa na kiu kikubwa zaidi: “Ee Mungu, wewe ni Mungu wangu, ninakutamani, kama nchi kavu na iliyochoka isiyo na maji” (Zaburi 62). Kinachotutenga sisi sote ni kunaswa na tamaa ndogo ndogo, katika kuridhika kidogo, kama kuwapiga wapinzani wetu au kuwa na hadhi, kuvaa kofia maalum! Kulingana na mapokeo ya mafunzo ya Mtakatifu, Thomas Aquinas alipoulizwa na dada yake Theodora jinsi ya kuwa mtakatifu, alijibu kwa neno moja: Velle! Uitake! Yesu huwauliza hivi watu wanaomkaribia: “Je, wataka, wataka?”; "Naweza kukusaidia vipi?" Bwana anataka kutupa utimilifu wa upendo. Je, tunaitaka?