杏MAP导航

Tafuta

Tarehe 30 Septemba ni kuundwa kwa Makardinali wapya 21 kutoka mabara yote.Tarehe 4 Oktoba Papa Francisko ataadhimisha misa  ya ufunguzi wa Sinodi pamoja na Makardinali wapya. Tarehe 30 Septemba ni kuundwa kwa Makardinali wapya 21 kutoka mabara yote.Tarehe 4 Oktoba Papa Francisko ataadhimisha misa ya ufunguzi wa Sinodi pamoja na Makardinali wapya. 

Papa:Septemba 30,kuundwa kwa makardinali wapya&Oktoba 4,misa ya ufunguzi wa Sinodi

Baba Mtakatifu anatarajia kuwaunda makardinali wapya 21 mnamo tarehe 30 Septemba wakati huohuo misa pamoja na Makardinali wapya itakuwa tarehe 4 Oktoba ikiwa ni ufunguzi wa Sinodi ya XVI ya Maaskofu.Yote hayo yatafanyika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican kwa ushiriki wa waamini pia.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Siku ya Jumamosi tarehe 30 Septemba 2023, saa 4.00 asubuhi, majira ya Ulaya, katika Uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, kwa umma, Baba Mtakatifu Francisko anatarajia kuwaunda Makardinali wapya 21 kwa kuwawekea mikono yake, kuvalishwa vikofia, utoaji wa pete kwa ajili utume wa huduma ya Kanisa na kuwakabidhi Kanisa mojawapo la Roma au Diakonia. Hayo yamethibitishwa tarehe 18 Septemba 2023 na taarifa ya Ofisi ya Maadhimisho ya Liturujia ya Kipapa na kubainisha kuwa, ziara za kuwatembelea  na kuwapongeza Makardinali wapya zitafanyika kuanzia saa 5.30 asubuhi hadi saa 7.30 mchana siku hiyo baada ya tukio la kuundwa kwa makardinali hao.

Maandalizi ya Kuundwa kwa makardinali wapya 21 mnamo tarehe 30 Septemba
Maandalizi ya Kuundwa kwa makardinali wapya 21 mnamo tarehe 30 Septemba

Wakati huo huo siku ya Jumatano tarehe 4 Oktoba 2023,  saa 3.00 asubuhi majira ya Ulaya, katika Uwanja wa Kanisa  Kuu la Mtakatifu Petro, Baba Mtakatifu Francisko anatarajia kuongoza maadhimisho ya Ekaristi Takatifu akiwa  pamoja na Makardinali wapya na Baraza la  Makardinali,  ambapo pia itakuwa ni fursa ya ufunguzi wa Mkutano mkuu wa kawaida wa Sinodi ya XVI ya Maaskofu kutoka ulimwenguni kote. Kwa mujibu wa maelekezo wafuatao wataweza kusherehekea pamoja na Baba Mtakatifu altareni: Makardinali wapya walioundwa, Baraza la Makardinali na Mapatriaki, Maaskofu wakuu, Maaskofu na Mapadre, washiriki wa Sinodi, Maaskofu wakuu wengine na maaskofu, makleri watakao kuwa na tiketi maalum.

Ikumbukwe Baba Mtakatifu Francisko mnamo Dominika tarehe 9 Julai 2023 aliwateuwa Makardinali wapya 21 miongoni mwa makardinali wateule ni Kardinali Mteule Protase Rugambwa, aliyezaliwa tarehe 31 Mei 1960 huko Bunena-Bukoba nchini Tanzania, akapata Daraja Takatifu ya Upadre mikononi mwa Mtakatifu Yohane Paulo II akiwa katika hija ya Kitume nchini Tanzania miaka 33 ilyopita mnamo tarehe 2 Septemba 1990 na kuwa Padre wa Jimbo Katoliki Rulenge-Ngara. Kuanzia mwaka 2002 hadi mwaka 2008  Kardinali Mteule alifanya utume wake kwenye Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu mjini Vatican. Baba Mtakatifu Benedikto XVI, mnamo tarehe 18 Januari 2008 alimteuwa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki Kigoma na tarehe 26 Juni 2012 akateuliwa kuwa Katibu Mwambata wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu na Rais wa Mashirika ya Kipapa ya Kimisionari,  wakati huo huo kumpandisha hadhi na kuwa Askofu mkuu.

Kardinali Mteule akiwa anakaribishwa Jimbo kuu
Kardinali Mteule akiwa anakaribishwa Jimbo kuu

Tarehe 9 Novemba 2017,  Baba Mtakatifu Francisko alimteuwa kuwa Katibu mkuu wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa watu. Alilitumikia Baraza  hilo kwa awamu mbili  ambapo kwa mujibu wa Katiba mpya ya Kitume ya “Predicate evangelium” yaani “Hubirini Injili” Juu ya Sekretarieti kuu la “Curia Romana” na  Huduma kwa Kanisa la Ulimwengu” alihitimisha muda wake. Na mnamo tarehe 13 Aprili 2023, Baba Mtakatifu Francisko alimteuwa kuwa Askofu Mkuu Mwandamizi  mwenye  haki ya kurithi Jimbo kuu  katoliki la Tabora, nchini Tanzania.

Moja ya mikutano na Papa ya kila wakti mjini Vatican
Moja ya mikutano na Papa ya kila wakti mjini Vatican

Makardinali wengine wateule ni  Askofu mkuu Robert Francis PREVOST, O.S.A., Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa; Askofu mkuu Claudio GUGEROTTI, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Makanisa ya Mashariki; Askofu mkuu Víctor Manuel FERNÁNDEZ, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa, Askofu mkuu Emil Paul TSCHERRIG, Balozi, Askofu mkuu Christophe Louis Yves Georges PIERRE, Balozi, Askofu mkuu Pierbattista PIZZABALLA, Patriaki wa Madhehebu ya Kilatini mjini Yerusalemu:  Askofu mkuu Stephen BRISLIN, wa Jimbo kuu la Cape Town, Afrika ya Kusini,  Askofu mkuu Ángel Sixto ROSSI, S.J., wa Jimbo kuu la Córdoba; Askofu mkuu Luis José RUEDA APARICIO, wa Jimbo kuu la Bogotá; Askofu mkuu Grzegorz RY?, wa Jimbo kuu la ?ód?, Askofu mkuu Stephen Ameyu Martin MULLA, Jimbo kuu la Juba, Sudan ya Kusini.

Orodha inaendelea: Askofu mkuu José COBO CANO, wa Jimbo kuu la Madrid, Askofu mkuu mwandamizi Protase RUGAMBWA, wa Jimbo kuu la Tabora, Tanzania;  Askofu mkuu Sebastian FRANCIS, wa Jimbo kuu la Penang; Askofu Stephen CHOW SAU-YAN, S.J., Askofu wa Hong Kong: Askofu François-Xavier BUSTILLO, O.F.M. Conv., wa Jimbo la Ajaccio, Askofu msaidizi Américo Manuel ALVES AGUIAR, wa Jimbo kuu la Lisbon, Ureno pamoja na Padre Ángel FERNÁNDEZ ARTIME, s.d.b., Mkuu wa Shirika la Wasalesian wa Don Bosco. Aidha Makardinali wengine wateule ni  pamoja na Askofu mkuu Agostino MARCHETTO, Balozi; Askofu mkuu mstaafu Diego Rafael PADRÓN SÁNCHEZ, wa Jimbo Cumaná; Padre Luis Pascual DRI, OFM Cap., Muungamishi wa Madhabahu ya Mama Yetu wa Pompei, Buenos Aires nchini Argentina.

Kundwa makardinali 30 Septemba&misa na makardnali wapya na ufunguzi wa sinodi Oktoba 4
18 Septemba 2023, 16:45