杏MAP导航

Tafuta

2023.09.25 Nembo ya mkesha wa kiekemeni utafanyika mnamo  septemba 30 katika Uwanja wa Mtakatifu  Petro mjini Vatican. 2023.09.25 Nembo ya mkesha wa kiekemeni utafanyika mnamo septemba 30 katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican. 

Mkesha wa Maombi kiekumeni kuombea Sinodi unakaribia!

Alasiri tarehe 30 Septemba,Papa atakuwa katika Uwanja wa Mtakatifu Petro pamoja na Patriaki wa Kiekumeni Bartholomew I,Askofu Mkuu wa Canterbury Welby na viongozi wengine wa kikanisa kuombea Sinodi kuanzia 4 Oktoba.Tukio limeandaliwa na Jumuiya ya Taizé kwa ushirikiano na Mabaraza ya Kipapa na Vicariate ya Roma.Maelfu ya vijana wa Ulaya,Marekani,Afrika na Asia wanatarajiwa.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Mkesha ulioandaliwa na Jumuiya ya Taizé kati ya waandaaji wakuu, kwa ushirikiano wa Sekretarieti ya Sinodi ya Maaskofu, Baraza la Uhamasishaji wa Umoja wa Kikristo, Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha na Vikariati yenyewe, ambayo inathamini uwepo wake na  kuwasili hasa kutoka Poland watu (470), kisha Ufaransa (400), Hispania (280), Hungaria(220), lakini pia kutoka Misri, Vietnam, Korea, Marekani, na pia kutoka Italia.  Kwa njia hiyo Uwanja wa Mtakatifu Petro utakuwa kitovu cha mfululizo wa mipango kama hiyo ulimwenguni kote pamoja na Mkesha wa tarehe 30 Septemba 2023.

Hadi sasa, ni zaidi ya viwanja 200 vimepangwa, huku Wakristo kutoka Makanisa mbalimbali watashiriki maombi na tafakari pamoja katika nchi zao, lakini orodha hiyo inasasishwa. Katika kipindi ambacho Makanisa yanaadhimisha Kipindi cha kazi ya Uumbaji, Uwanja wa Mtakatifu Petro wenyewe utageuzwa kuwa ‘bustani,’ iliyojaa miti na maua, ambapo Msalaba wa Mtakatifu Damiano wa Mtakatifu Francis wa Asisi utawekwa. Kwa maelfu ya vijana wenye umri wa miaka 18 hadi 35 ambao Roma inawaandalia, pamoja na mkesha huo, ratiba ya warsha na mikutano inapangwa. Itafanyika kuanzia tarehe 29 Septemba hadi 1 Oktoba 2023 na itajumuisha sala ya sifa na kuabudu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yohane huko Laterano mapema alasiri ya Jumamosi 30 Septemba kabla ya Mkesha katika Uwanja wa Mtakatifu Petro.

Mada za warsha hizo pamoja na mambo mengine, ni kuwasikiliza wakimbizi, mang’amuzi yao, kujifunza kutoka katika maadhehebu na dini nyinginezo, kutembelea kazi za uutume za jiji pamoja na watu waliotengwa, kumtambua Kristo katika utofauti wa mambo mbalimbali, mila na utamaduni katika , kushiriki katika meza za pande zote za kiekumeni na zaidi katika kuhangaikia Uumbaji. Wazo la mkusanyiko wa maombi lilizaliwa, kulingana na taarifa rasmi, mnamo Oktoba 2021, wakati Ndugu Alois, aliyekuwa Mkuu wa Jumuiya ya Kiekumeni ya Taizé, alialikwa kuzungumza kwenye ufunguzi wa mchakato wa sinodi ya Kanisa Katoliki. Alitangaza hivi: “Kupitia ubatizo, sisi ni kaka  na dada katika Kristo, tukiwa tumeunganishwa katika ushirika ambao bado si mkamilifu,  lakini wa kweli kabisa, hata wakati maswali ya kitaalimungu yanabaki bila kujibiwa."

25 Septemba 2023, 15:39