GCE itakuwa Lisbon kwa WYD inayohamasishwa na Baraza la Kipapa la Elimu na Utamaduni
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Katika siku ya XXXVII Vijana Duniani 2023 inayoanza tarehe 1 hadi 6 Agosti 2023 huko Lisbon nchini Ureno. Baraza la Kipapa la Elimu na Utamaduni, linatoa taarifa kuwa litakuwapo katika Siku ya Vijana Duniani (WYD)ambapo limeamua kutumia fursa hiyo kwa kuzindua kwa upya yale ambayo Baba Mtakatifu Francisko aliyaanzisha mnamo mwaka 2019 ili kujenga Mkataba wa Kimataifa wa Elimu kwa manufaa ya vizazi vijana na kupitia kwao, iwe dunia nzima. Kwa maana hiyo, shughuli zifuatazo zimepangwa kama sehemu ya Siku ya vijana (WYD): Watakuwepo katika Jiji la Furaha na Stendi inayolenga kuonesha Mkataba wa Kimataifa, kwa lengo kufanya Mkataba wa Kimataifa wa Elimu ujulikane lakini zaidi ya yote katika kuvutia vijana wageni (kupitia shughuli zenye msimamo na pia uchunguzi wa mtandaoni) maoni, mawazo na mapendekezo juu ya elimu na matarajio ya siku zijazo.
Vijana wageni watawaalika kushiriki uzoefu wa ziara yao kwenye stendi kwa kutumia:#globalcompactoneducation katika historia zao, Post na Reel, kwa kutumia:@globalcompactoneducation, Instagram au @GConEducation katika Twitter. "Tutaomba hata utengeneze Reel/video (angalau ya sekunde 90) kuhusu uzoefu muhimu wa kielimu ambao umeshiriki na kututumia kwa kupitia: info@educationglobalcompact.org: na uzoefu wa kuvutia zaidi utahamasishwa kwenye tovuti: . Tarehe 1 Agosti kuanzia saa 2.30 asubuhi hadi saa 10 jioni katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Ureno kama sehemu ya mipango ya “Nyumba ya Uchumi wa Francisko” kutakuwa na mkutano wa (Global Compact) wa Mkataba wa kielimu Kimataifa ambapo utaingiliwa kati kama mzungumzaji mkuu. Mnamo tarehe 2 Agosti kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 10 jioni katika Ukumbi wa Kitivo cha Chuo Kikuu cha Lisbon, kama sehemu ya mipango ya Tamasha la Vijana, mkutano utafanyika juu ya mada: “Tumaini. Wito wa kuelimisha” unaohamasishwa na Baraza la Kipapa la Elimu na Utamaduni pamoja na kikundi cha maprofesa kutoka shule za Kikatoliki za Ureno ambapo, kupitia ushuhuda fulani, watazingatia jukumu la msingi kuelimisha na jinsi ilivyo muhimu kwa vijana wenye vipaji kuzingatia aina hizi za kazi.
Tarehe 3 Agosti 2023 saa tatu kamili asubuhi katika mchakato wa mkutano aliofanya Baba Mtakatifu pamoja na wanafunzi wa chuo kikuu cha Kikatoliki cha Ureno kutakuwa na ushuhuda wa mwanafunzi kijana kuhusu uzoefu wa Global Compact na wanajua kwamba Baba Mtakatifu atagusa mpango huu katika hotuba yake tarehe 4 Agosti saa 2.30 usiku katika Jiji la Furaha kutakuwa na ushuhuda juu ya Mkataba wa Elimu Kimataifa. Kwa maelezo zaidi bonyeza: