杏MAP导航

Tafuta

2023.01.31 Bwana Filippo Grandi Kamishna Mkuu wa Umoja wa mataifa kwa ajili ya Wakimbizi akiwa Radio Vatican. 2023.01.31 Bwana Filippo Grandi Kamishna Mkuu wa Umoja wa mataifa kwa ajili ya Wakimbizi akiwa Radio Vatican. 

Grandi,Unhcr:sauti ya Papa ni msingi kwa wakimbizi

Hali ya wakimbizi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Sudan Kusini,vifo katika Bahari ya Mediterania na jukumu la lazima la mashirika ya kiraia.Ni masuala yaliyoibuka wakati ambapo Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Kuhudumia Wakimbizi alipokutana na Papa Francisko siku moja wa kabla ya ziara yake barani Afrika Afrika.

Na Angella Rwezaula;-Vatican.

Baada ya siku sita akiwa katika nchi ya Ukraine iliyoharibiwa na mabomu, ambapo takriban watu milioni 5 tayari wameachwa bila makao na wengine milioni 6 kulazimika kukimbia kuvuka mipaka, Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Wakimbizi aliwasili nchini Italia ili kushughulikia ripoti tata ya mtiririko wa wahamiaji kupitia Bahari ya Mediterania. Baada ya mazungumzo na Rais wa Jamhuri, ya Italia Bwana Sergio Mattarella, Filippo Grandi tarehe 31 Januari 2023 alikutana na viongozi wa serikali ya Italia wanaohusika katika makabiliano makali na Umoja wa Ulaya kuhusu uhamiaji na katikati ya mabishano juu ya jukumu la mashirika yasiyo ya kiserikali dhidi ya Umoja wa Ulaya na utafutaji na uokoaji baharini.

Kamisha Mkuu wa UN na  Papa Francisko

Jumatatu asubuhi tarehe 30 Januari alifika mjini Vatican, Bwana Filippo  Grandi na kukutana na  Papa Francisko na Makatibu  wa Sekretarieti ya Vatican. Ni mkutano ambao ulifanyika kwa muda mfupi kabla ya ziara yake ya 40 ya kitume kuelekea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Sudan Kusini. Nchi mbili zinazopitia kwa muda mrefu na machafuko makubwa ya kisiasa na kijamii,na athari kubwa za kibinadamu, lakini pia majimbo mawili ambayo yana idadi isiyohesabika ya wakimbizi na watu waliohamishwa ndani ya mipaka yao, mara nyingi wakikimbia migogoro inayoendelea katika nchi jirani. Mkuu wa UNHCR akizungumza na  Radio Vatican,  hana shaka kwamba sauti ya Papa Francisko katika mazingira ya Afrika ina umuhimu msingi.

Migogoro inayochochea mzozo wa wakimbizi

Katika miaka thelathini iliyopita, unyanyasaji dhidi ya raia, hasa dhidi ya wanawake, umekuwa wa kutisha ameeleza  Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa hivyo nni matumaini  kuwa sauti ya Papa inaweza kukumbusha ulimwengu kwamba ni muhimu kuunga mkono majibu ya kibinadamu kwa machafuko hayo. Majaribio ya kuanzisha mchakato wa amani yamekuwa ya woga na hayana tija na kwa hakika shinikizo linalotokana na kuwepo kwa wakimbizi wengi kutoka barani Afrika limewakilisha kipengele kingine cha mvutano. Ni hali ngumu sana ambapo jukumu la watu wanaokimbia, wakati mwingine, pia lina ushawishi katika mzozo na wakimbizi kwa maana fulani wanasabishwa kati ya mizozo miwili.

Ngome ya Ulaya

Ili kuelewa athari za migogoro na hali ya migogoro kwa idadi kubwa ya wakimbizi duniani itatosha kuangalia kile kinachotokea nchini Ukraine. Katika mwaka mmoja tu wa vita watu wasiopungua milioni 7 wamepata hifadhi nje ya nchi na milioni 5 wamekimbia makazi yao ndani ya nchi. Mgogoro wa kibinadamu ambao uliamsha mshikamano wa haraka wa Umoja wa Ulaya ambao ulipitisha chombo cha ulinzi wa muda kwa ajili ya wakimbizi wa Ukraine. Kipimo ambacho Bwana Filippo Grandi anakizingatia kuwa sio tu chanya sana, lakini pia kielelezo cha uingiliaji kati wa siku zijazo. “Ikiwa tumefaulu barani Ulaya kuwakaribisha wakimbizi wa Kiukreni vizuri sana tunaweza kufanya vivyo hivyo na wengine, kwa sababu hata kama kunaweza kuwa na changamoto ngumu zaidi katika kuunganisha na kukaribisha vikundi vingine, matibabu ya kibaguzi au tofauti hayawezi kuzalishwa, kwa hivyo tunatumia mazoea haya kwa vikundi vingine pia na ninaamini tutapiga hatua katika mapokezi”.

NGOs na uokoaji baharini

Iwapo mjadala barani Ulaya unapamba moto kuhusu masuala ya upokeaji wahamiaji, hasa kuhusu mgawanyo wa idadi ya wakimbizi na Nchi Wanachama, utata unazidi juu ya jukumu la mashirika yasiyo ya kiserikali katika shughuli za utafutaji na uokoaji wa wahamiaji katika  bahari ya Mediterania. Kwa hiyo “Mashirika ya kiraia ni nyenzo muhimu sana inayosaidia hatua za serikali. Ingawa Walinzi wa Pwani ya Italia hufanya kazi nzuri ya uokoaji, rasilimali zilizowekwa na Ulaya katika operesheni hizi hazitoshi na kwa hivyo mashirika ya kiraia hushughulikia hayo mapungufu, na hakuna shaka hatua hii lazima itetewe na kuungwa mkono,” alieleza Bwana Filippo Grandi.

Kamishna mkuu wa UN kwa ajili ya Wakimbizi
31 Januari 2023, 17:12