杏MAP导航

Tafuta

Ratiba ya Papa Francisko ya Ziara yake kwenda Cyprus na Ugiriki Ratiba ya Papa Francisko ya Ziara yake kwenda Cyprus na Ugiriki 

Ziara ya Papa Francisko Cypurs na Ugiriki,ratiba elekezi ya safari hiyo!

Imetolewa ratiba ya ziara ya kitume ya Papa Francisko kuanzia tarehe 2 hadi 6 Desemba 2021 kuelekea Cyprus na Ugiriki.Mikutano na sala ya kina inatarajiwa wakati wa ziara hiyo ya kitume katika nchi hizo mbili.

Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.

Siku tano, zitakazo jikita kwenye matukio ya hotuba tisa, homelia mbili na sala ya Malaika wa Bwana ikiwa ni baadhi ya  idadi yake zinazoashiria ziara ya kitume ya Papa Francisko itakayofanyika kuanzia tarehe 2 hadi 6 Desemba 2021. Kituo cha kwanza ni Cyprus cha pili ni Ugiriki. Kulingana na mpango uliotangazwa na Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican, Papa Francisko, ambaye ataondoka kiwanja cha Ndege cha Kimataifa Fiumicino, Roma saa 11.00 siku ya Alhamisi tarehe 2 Desemba 2021, na baada ya takriban saa nne za safari ya ndege, atakaribishwa rasmi kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Larnaca huko Nicosia na atakuwa na mipango mbalimbali ya mikutano huko.

Hotuba ya kwanza imepangwa kufanyika mapema kama 10.00 jioni katika mkutano na mapadre, watawa, mashemasi, makatekista, vyama vya kitume vya kikanisa huko Cyprus katika Kanisa Kuu la Kimaronite la Mama Yetu wa Neema. Kuanzia hapo Papa atahamia kwenda Ikulu ya Rais kwa afla  ya kukaribishwa saa 11.15 jioni, na mara baada ya hapo atakwenda kwenye Jumba la Sherehe kwa ajili ya mkutano na Mamlaka, Mashirika ya Kiraia na Wanadiplomasia ambaoo atawahutubia katika hotuba ya pili.

Siku itakayo fuata, Ijumaa tarehe 3 Desemba, itafunguliwa saa 8.30 asubuhi  kwa ziara ya ukarimu kwa Askofu Mkuu wa Kiorthodox Chrysostomos II wa Cyprus kwenye jumba la uaskofu mkuu, ikifuatiwa na mkutano na Sinodi Takatifu saa 3.00 asubuhi, kwenye Kanisa Kuu la Kiorthodox huko Nicosia. Papa Francisko atahutubia hotuba yake hapo. Mahubiri ya kwanza ya Papa badala yake yatakuwa katika Misa Takatifu saa 10.00 huko huko Nicosia, kwenye Uwanja wa GSP. Alasiri, ratiba inaonesha kuanzia saa 10.00 jioni kwa sala ya kiekumene na wahamiaji katika Kanisa la parokia ya Msalaba Mtakatifu  huko Nicosia, ambapo hotuba ya Francisko imepangwa pia.

Hatua ya ziara yake utahitimishwa huko Cyprus  asubuhi Jumamosi tarehe 4 Desemba 2021. Muda mfupi baada ya saa 3.00, kuondoka kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Larnaca kuelekea Athene, Papa anatarajiwa kuwasili saa 5:10. Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa sherehe rasmi ya mapokezi na baadaye kukaribishwa katika Ikulu ya Rais kuanzia saa 6.00 mchana. Baada ya ziara ya heshima kwa Rais wa Jamhuri katika ofisi yake binafsi, saa 12.30 kutakuwa na kikao na Waziri Mkuu na baadaye na Mamlaka, Jumuiya za Kiraia na Kikundi cha Wanadiplomasia.

Alasiri huko Athene, kuanzia saa 10.00 jioni kutakuwa na mfululizo wa mikutano ya kidini. Kwanza, ziara ya heshima Askofu  mkuu  Ieronymos II, askofu mkuu wa Athene na Ugiriki yote, katika uaskofu mkuu wa Kiorthodox ya Ugiriki, baadaye mkutano nawahusika katika chumba kikuu cha uaskofu mkuu ambapo Papa atatoa hotuba yake. Baadaye atahamia shemu nyingine saa 11.15 jioni katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Dionysius huko Athene kwa ajili ya mkutano na hotuba iliyoelekezwa kwa maaskofu, mapadre, watawa, waseminari na makatekista. Siku ya Fransisko itakamilika saa 12.45 jioni kwenye makao makuu ya kitume ambapo kwa faragha, atafanya mkutano ulipangwa  na wanashiriki wa Shirika la Yesu (Jesuit).

Dominika asubuhi Papa atasafiri kwa ndege kutoka Athens hadi Mytilene - Lesvos ambapo atafika karibu saa 4.10 kufikia Kituo cha Mapokezi na Utambulisho kwa ajili ya mkutano na hotuba yake kwa wakimbizi, ambao wanakaribishwa huko, iliyopangwa kuanzia saa 10.45. Mwisho atarudi Athene. Hapo, alasiri saa 10.45 jioni, adhimisho la Ekaristi Takatifu katika Ukumbi wa Tamasha la Megaron, baadaye atarudi ubalozi kwa wa kitume  ambapo saa 1.00 usiku Papa atapokea ziara ya heshima kutoka kwa Askofu Mkuu Ieronymus II.

Siku ya mwisho nchini Ugiriki, itakuwa Jumatatu tarehe 6 Desemba 2021, ambapo itaona matukio mawili makuu kabla ya sherehe ya kuagwa. Saa 2.15 alfajiri Papa Francisko atapata ugeni kutoka kwa Rais wa Bunge kwenye hafla akiwa Ubalozi wa kitume  na saa 9.45 asubuhi atafikia Shule ya Mtakatifu Dionigi ya Masista wa Ursula huko Maroussi kwa ajili ya mkutano mzuri  na vijana ambapo atahutubia hotuba ya mwisho iliyopangwa katika safari hiyo. Saa 5.15 asubuhi ahahamia katika  Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Athens kwa sherehe ya kuagwa na kuondoka kuelekea Roma katika uwanja wa Ciampino, ambapo anatarajiwa kuwasili majira ya  saa 6.35 mchana.

14 Novemba 2021, 10:17