杏MAP导航

Tafuta

2021.05.23 Nembo ya Jukwaa la Laudato Sì 2021 2021.05.23 Nembo ya Jukwaa la Laudato Sì 2021 

Kard.Tagle,Injili ya Uumbaji:Utume ni zawadi kwa Kanisa lote

Katika utume wa Kanisa kila mbatizwa amepokea Roho Mtakatifu zawadi ambayo inapaswa kuendelezwa kwa kushiriki katika utume wenyewe na kuhusu suala la Laudato si’, ni utunzaji wa nyumba yetu ya pamoja.Utume kama wito kwa ajili ya maisha yote ni hata kusindikiza wengine na kubaki kufanya hatua moja moja na si kurudi nyuma.

Na Sr. Angela rwezaula – Vatican.

Kardinali Luis Antonio Tagle, Kardinali Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu, wakati anazungumza kweny radio Vatican juu ya utume wa kimisionari uliokabidhiwa kwa wahudumu wa Laudato si' wa Harakati Katoliki Ulimwenguni kwa ajili ya Tabianchi na wahudumu wengine wa kichungaji, vijana, watu wenye mapenzi mema amesema: “Katika utume wa Kanisa kila mbatizwa amepokea Roho Mtakatifu zawadi ambayo inapaswa kuendelezwa kwa kushiriki katika utume wenyewe na kuhusu suala la Laudato si’,  ni utunzaji wa nyumba yetu ya pamoja”.

Alithibitisha hayo mara tu baada ya Papa Franciko Jumapili wakati wa Sala ya Malkia wa Mbingu alikuwa amezungmzia juu ya utume wa kueneza Injili ya Kazi ya Uumbaji na kuanza utunzaji wa mazingira nyumba yetu ya pamoja. Katika mtazamo wa kumbukumbu ya miaka sita ya Waraka wa Papa Francisko juu ya utunzaji wa nyumba ya pamoja, uliochapishwa mnamo tarehe 24 Mei 2015, na katika Wiki ya Laudato Si, ambayo imehitimisha mwaka maalum uliotangazwa na Papa kutafakari na kujikita kwenye matendo ya dhati ya  waraka huo, vile vile  Kardinali Tagle ameongoza mkutano wa maombi katika Shirika la Watawa Wafranciskani (OFM) Roma.

Katika siku ya Pentekoste, siku ya kushuka kwa Roho Mtakatifu ambaye alitoa mwanzo wa utume wa Kanisa au kuzaliwa kwa Kanisa, Kardinali Tagle amesema Pentekoste ni kuonesha kuwa Kristo aliyefufuka anandelea kubaki nasi.  Wito wa Kardinali ni kuwa shuhuda wa ukweli wa ulimwengu, hata baada ya wakati huu ambao ni wa mgogoro uliokumbwa na janga la virusi vya covid-19. Kufanya uzoefu wa Kristo ni kuelewa kuwa Yesu anatusindikiza kama alivyofanya kwa wafuasi wake. Utume kama wito kwa ajili ya maisha yote ni hata kusindikiza wengine na kubaki kufanya hatua moja moja na si kurudi nyumba

Kwa upande mwingine, ameunga mkono wa maneno ya Padre Augusto Zampini, katibu msaidizi wa Kitengo cha Baraza la Maendeleo Fungamani ya Binadamu na mjumbe wa mwelekeo wa Tume ya Vaticani Covid-19. Padre Zampini yeye alisema Injili ya Uumbaji imeunganishwa na Kanisa linalotoka nje, kwa maana ni Kanisa ambalo hutunza nyumba yetu ya pamoja na ya wengine kila mahali kwenye sayari hii. Huu ndio uzuri wa maana ya kimisionari wa kuleta ujumbe wa Injili na Laudato si ', wa utunzaji wa nyumba yetu ya pamoja na wengine, katika kila sehemu ya sayari, katika kila sekta ya jamii, pia kukumbuka jinsi Papa ambavyo anaomba mabadiliko makubwa ya uchumi iliougua, kwa sababu husababisha ukosefu wa usawa, magonjwa ya kijamii, mizozo na uharibifu wa kazi ya uumbaji, ameongeza Padre Zampini.

Kutoka Rio de Janerio, Nairobi, Washington, Roma, Assisi limefika jibu la ndio la utume wa kimisionari, kuchukua jukumu la Wahuishaji ili kusikiliza kilio cha Dunia na maskini, wale waathiriwa wa shida na mateso katika nchi ya India kama, ilivyo Brazil ambapo Padre Michael Perry, Mkuu wa Shirika la Ndugu wadogo Wafransiskani ( OFM) alitaka kukumbusha katika hotuba yake kwamba  wao ni watu ambao kiukweli wanabeba Msalaba, ambao lazima kuwapa fursa, kwa   mtazamo wa udugu na utume. Jitihada ya mwisho ilikuwa kuangazia ukarimu, upendo na unyenyekevu  kama alivyosisitiza Kardinali Tagle kwamba ni kuwasha mshumaa na washiriki  ile  nuru katika maisha ya Kanisa na  ulimwengu. Matashi mema kwa ajili ya upyaisho wa jitihada zaidi kwa waamini ilitoka katika  Bustani ya Botaniki ya Roma, ambapo Padre Joshtrom Isaac Kureethadam, Mratibu wa Sekta ya Ekolojia na Uumbaji ya Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya binadamu  alikuwa ameadhimisha Misa Takatifu kwa kumbukumbu ya miaka sita tangu kuchapishwa kwa Waraka wa  Laudato si '. “Tumepokea bustani, hatuwezi kuiacha kama jangwa kwa vijana wetu na kwa maana hiyo amesisitizai ju ya Waraka huo wa Papa wa kulinda viumbe vyote na utunzji wa mazingira nyumba yetu ya Pamoja.

25 Mei 2021, 15:05