Hija ya kitume Papa Francisko nchini Iraq:Mwenyeheri siyo shujaa ni shuhuda
Na Sr. Angela Rwezaula-Vatican.
Yesu anabadilisha historia na nguvu ya unyenyekevu ya upendo.Mwenye mara nyingi siyo shujaa bali ni shuhuda daima. Ni kutoka katika takari ya mahubiri ya Papa Francisko wakati wa Misa takatifu iliyofanyika katika Kanisa kuu la jijini Baghdad kwa kuhitimish siku yake ya pili ya ziara yake ya kitume, Papa mejikita kwenye tafakari juu ya maana ya 'Heri za mlimani' na amewahimiza waamini kushuhudia kila siku ule mtindo wa maisha unaoongozwa na Yesu na ambao unapindua mawazo ya wanadamu. Katika Video Fupi inaoenesha ufupisho wa misa hiyo takatifu katika Kanisa Kuu la Baghdad na yenye maana kuu katika ziara hiyo ya Kitume nchini Iraq, iliyoanza Ijumaa, tarehe 5 na itahitimishwa tarehe 8 Machi 2021.
Sehemu ya pili ya Video inaonesha wakati waamini wako tayari wanamsubiri Papa Francisko kuadhimisha Misa katika Kanisa Kuu, jijini Baghdad akiwa katika ziara hii ya kitume kwa siku tatu. Lugha zilizoambatana na sherehe ya Ekaristi hiyo zilikuwa ni Kiitaliano, Kikaldayo na Kiarabu na katika maombi ya waamini pia ilikuwa ni lugha ya kiharamu, Kurdish, Turkmen na Kiingereza. Kuna maneno matatu muhimu yaliyomo kwenye mahubiri ambayo Papa Francisko amefafanua kwa Kiitaliano na ambayo yamependekezwa na Masomo yaliyosomwa yaani:hekima, shahidi na ahadi.