杏MAP导航

Tafuta

Hija ya kitume Papa Francisko nchini Iraq:Mkutano na Al-Sistani na kwenda Uru

Papa Francisko mara baada ya kufika Najaf,katika siku ya pili ya ziara yake amekutana na kiongozi wa jumuyia ya Washia nchini Iraq.Mazungumzo yao ni kuhusu ushirikiano kati ya Jumuiya za kidini.Katika maoni ya kiongozi wa Iran amebainisha mkutano huo unaweza kusaidia kusitisha vurugu za kidini

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Umuhimu wa ushirikiano na urafiki kati ya jumuiya za kidini ili, kwa kukuza kuheshimiana na mazungumzo, vinaweza kuchangia wema wa Iraq, kanda na wanadamu wote, ilikuwa moja wapo ya mada iliyoangaziwa na Baba Mtakatifu Francisko katika mkutano wake wa faragha asubuhi Jumamosi tarehe 6 Machi 2021 huko Najaf na Ayatollah Sayyid Ali Al-Husayni Al-Sistani, kiongozi wa jumuiya ya Washia nchini humo.

MKUTANO NA KIONGOZI WA WASHIA
MKUTANO NA KIONGOZI WA WASHIA

Video fupi inaonesha namna ambavyo Baba Mtakatifu  Francisko alivyofika katika makao ya kiongozi huyo.  Wanaoneskana Vijana ambao wamepeperusha bendera za Iraq na Jiji la Vatican, vile vile hata eneo lote la makao ya kiongozi huyo. Kwenye mabango ya kukaribisha kando ya barabara, maneno yameandikwa “Wewe ni sehemu yetu na sisi ni sehemu yako” ambayo yanaonekana na sura za Papa na Al-Sistani.

MABANGO KANDO YA BARABARA YA KUKARIBISHA PAPA
MABANGO KANDO YA BARABARA YA KUKARIBISHA PAPA

Miongoni mwa maoni ya ulimwengu wa Kiisilamu juu ya tukio la Najaf, ni ya yaliyo funguliwa katika ukurasa wa  tweet na Mohammad Ali Abtahi, aliyekuwa mhudumu wa karibu wa rais wa zamani wa Irani Khatami.  Katika maneno yake amesema: “Mkutano kati ya Francisko na Ayatollah Al-Sistani, unaweza kuzuia vurugu za kidini au angalau kuunda mipaka kati ya ukweli wa amani wa dini na vurugu za kidini”.

PAPA ANAPOKEA ZAWADI
PAPA ANAPOKEA ZAWADI

Baada ya Mkutano huo Papa ameendelea na safari yake Nassiriya  ili aweze kufika huko Uru kwa ajili ya Mkutano wa kidini.

06 Machi 2021, 13:38