杏MAP导航

Tafuta

Video na tovuti katika muktadha wa Siku ya I ya Kimataifa ya Udugu kibinadamu!

Katika mkutadha wa Siku ya Kimataifa ya Udugu wa kibinadamu imetengenezwa video na Tovuti mpya inayofafanua kwa kirefu Siku hii ambapo unaweza kujua maana yake kwa kina kupitia nyenzo ya kusikiliza,kuona picha na video nyingi lakini pia maelezo katika lugha mbambali za dunia hata Kiswahili.Kwa sasa tovuti ni kwa lugha ya kiingereza.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Tarehe 4 Februari imewekwa na Umoja wa Mataifa ili kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Udugu kibinadamu ambapo inaturudisha nyuma katika tukio moja msingi la kumbukumbu ya  "Hati juu ya Udugu wa Kibinadamu kwa ajili ya amani ya ulimwengu na kuishi pamoja", iliyosainiwa huko Abu Dhabi, katika Falme za Kiarabu, mnamo tarehe 4 Februari 2019 na Papa Francisko na Imam Mkuu wa Al-Azhar, Ahmad Al- Tayyib. Katika fursa ya siku hii, Alhamis tarehe 4 Februari 2021, mchana Papa Francisko ameungana na shughuli yote ya kimataifa iliyopangwa kufanyika huko Abu Dhabi kwa njia ya mtandao kwa ushiriki wa Sheikh Mohammed bin Zayed, Imam Mkuu wa Al-Azhar, Ahmad Al-Tayyeb, katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana António Guterres, na viongozi wengine wakuu.

Ni nini maana ya siku ya Udugu kibinadamu?

Ili kuelewa umuhimu wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Udugu wa Binadamu, imetengenezwa, Tovuti mpya inayoelezea kwa kina vidokezo muhimu ili kupata maana ya maadhimisho haya maalum. Kupitia nyenzo ya kusikiliza yenye kuvutia inayojumuisha nakala, picha na video, mtumiaji anaweza kuelewa vizuri kusudi la mpango huu wa ulimwengu. Ndani mwake unawezekana kupata maneno ya Papa Francisko huko Abu Dhabi, maandishi ya Hati juu ya Udugu wa Binadamu ambayo yameandikwa kwa lugha nyingi sana hata. Kwa sasa, tovuti hiyo inapatikana kwa lugha ya Kiingereza: y

04 Februari 2021, 15:47