杏MAP导航

Tafuta

Tarehe 10 Oktoba ni Siku ya Kupinga adhabu ya kifo Tarehe 10 Oktoba ni Siku ya Kupinga adhabu ya kifo 

Ask.Mkuu Jurkovi?:Maisha ya binadamu hayakiukwi!

Adhabu ya kifo ni adhabu ya kikatili na inakiuka haki ya msingi ya kuishi na kudumisha utamaduni wa ‘jicho kwa jicho’. Adhabu hii inapingana na misingi ya haki za binadamu kwa vile ni adhabu ya kikatili inayokatisha haki ya binadamu ya kuishi.Ni katika muktadha wa siku ya kupinga Adhabu ya Kifo.Kuna mwelekeo wa kupunga duniani kote,lakini idadi ya mauaji katika nchi nyingine bado haijulikani.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Tarehe 10 Oktoba ni siku ya 18 kimataifa ya kupinga Adhabu ya Kifo, iliyoanzishwa tangu tarehe 26 Septemba 2003. Licha ya jitihada za  wanaharakati wa kutafuta kufuta sheria katika miaka ya hivi karibuni suala hili bado halikuwahi kupungua,  na bado linaendelea kuwa  na maamuzi zaidi, licha ya ukweli kwamba kumekuwa na ongezeko la idadi ya nchi ambazo zimekomesha mauaji, kwa sheria au kwa vitendo, na kupungua, katika  mwaka 2019, katika utekelezaji na hukumu hiyo ya kifo. Pia mwaka huu, takwimu ambazo zinashuhudia mwenendo wa adhabu ya kifo, kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa  Amnesty International zinazungumzia mwenendo wa kukabiliana  nchi ya  China, Iran, Saudi Arabia, Iraq na Misri ambazo zinazoendelea na sera yao ya kunyonga, bila hata kutoa idadi  rasmi ambayo, tena  kulingana na Amnesty, inawez kuwa hata maelfu kila mwaka, hasa nchini China ambapo pia ni pamoja na Belarusi, Vietnam na Korea Kaskazini, zinazoainisha takwimu hiyo kuwa siri ya serikali. Marekani ambayo mwaka jana iliashiria kiwango cha chini kabisa cha mauaji katika miaka 10, badala yake imeanzisha tena mauaji katika shirikisho   nchini Marekani mwezi Juni mwaka huu.

Papa Francisko katika Waraka wake wa 'Fratelli tutti', anaelezea kuwa adhabu ya kifo ni jibu la uongo ambalo haliondoi matatizo. Kwa mujibu wa Askofu Mkuu Ivan Jurkovi?, mwakilishi wa kudumu wa Vatican wa Umoja wa Mataifa na mashirika mengine ya kimataifa yaliyoko Geneva amesema haki ya binadamu inashindwa, lakini adhabu ya kifo haibadiliki. Ili  kuondoa adhabu hii, anasema  yapo mambo muhimu sana.  Kwanzai sio kuzingatia adhabu ya kifo isiyokubalika ni imani ambayo imekuwa ikiishi kila wakati na ni ukweli kwamba tumekuwa tukikumbuka  tarehe hii ambapo sasa ni miaka 18 tu inamaanisha kuwa ni ufahamu wa hivi karibuni. Kwa jumla, kama kawaida katika mifumo yetu yote ya kisheria,  pia katika maisha ya kijamii, kuna ngazi mbili: moja ya maadili na nyingine ya kisheria. Hapo zamani ilionekana kuwa kitu kimoja na hata leo wameunganishwa kwa karibu, lakini kuna tabia, katika maisha ya Mataifa, kutenganisha mambo haya mawili kwa njia ya kisheria iliyoainishwa zaidi, wakati, katika hali ya maadili, huruma  na haki kila wakati vinakwenda pamoja. Hata katika sheria inasemekana kwamba ‘summum ius’, summa iniuria’, (haki kuu, dhuluma kuu,), inamaanisha jambo la kutisha zaidi. Hapana, haki lazima kila wakati iambatane na huruma, wakati katika mfumo wa sheria, ulioandikwa, kutungwa sheria na kadhalika, tofauti hii hupotea kidogo, ambayo inamaanisha kuwa uhalifu uliotokea unahitaji jibu. Hii yenyewe kwa kila mwanadamu, hasa vijana, ni wazi kabisa kuwa kuua mtu, haijalishi wamefanya nini, na kwa uwezo wa wengi kuweza kujirekebisha, ni jambo nje ya mantiki ya maisha ya kawaida.

Jambo lingine ambalo linaonekana kuwa muhimu kwake ni kusisitiza kwamba viwango vitatu vya maarifa vinaweza kutambuliwa: ya kwanza ni ile ya utambuzi. Mtu husoma takwimu, anasikiliza hotuba, na anaelewa mambo. Halafu anakuja mtu ambaye anakuletea picha, kama ile ambayo sisi sote tumeona ya mtoto aliyezama maji, na kila kitu ambacho tumesikia hapo awali hakionekani kuwa chochote ikilinganishwa na nguvu ya picha ya janga la kweli. Vile vile akifafanua amesema  kama vile Papa mara nyingi  anasema, wewe ukiona watu, kila kitu huanguka hapo. Inamaanisha kwamba imani zote, hotuba zote zinaanguka, unapoona kuwa mtu huyo anaumia, kwamba yuko katika hali isiyokubalika ambayo inakera kila mtu. Kwa njia hiyo Askofu Mkuu anafikiria kuwa ukatili wa adhabu ya kifo hufichwa kila wakati. Inaishi na sisi, ni sheria, lakini ni mbaya sana kutazama. Adhabu hii mbaya hutolewa kwetu kwa njia ya iliyofichwa, na labda hiyo ndiyo haifanyi tuhukumu ukweli kama inavyopaswa kuhukumiwa vibaya sana.

Haki haikiukwi katika maisha kwa maana ni zawadi ya Mungu na hata kwa muhalifu kwa mujibu wa Papa Francisko. Lakini kwa walio wengi msingi huo siyo rahisi kuupokea na mara nyingi inatokea kushindwa kuzuia utelekezwaji huo hadi kufikia kulipa visasi vya jino kwa jino, kwa mujibu wa Askofu Mkuu anasema “Sisi kama Kanisa tunatazama Injili na Injili haitoi msaada wowote kwa mtu yeyote ambaye anaweza kusema kwamba adhabu ya kifo inaruhusiwa. Injili ni mwelekeo wetu, Kanisa linafuata Injili, Kanisa linakua na Injili. Kwa  maana hiyo tuna hakika kwamba sisi pia lazima tukuze na kueneza usadikisho huo, ambao ni maono ya Injili, ya utakatifu wa maisha ya mwanadamu ambao hautakiwi kukiukwa. Ni kanuni ambayo lazima idhibitishwe kisheria na kulindwa. Karibu nchi zote duniani zina uwezo wa kuchagua adhabu mbadala: lazima tukuze msimamo huu kwa umakini, na kusadikika.

Kama wawakilishi wa Vaticana amesema “tunaona kwamba sauti ya Papa, inayoongozwa na mwanaga wa ndani, ni sauti inayosubiriwa sana. Kila mtu anataka kuisikia. Tunaona kwamba mielekeo, yenyewe, siyo mbaya, lakini haitoshi. Kwa maana hiyo sauti ya kinabii ya Kanisa na ya Papa, katika muktadha wa kimataifa, inaonekana na ni muhimu sana. Lazima tathmini tena upendo kama kanuni ya lazima kwa maisha ya kijamii, lazima tufanye hivyo tu! Lazima tujue kuwa msamaha, upendo na huruma ni kanuni ambazo zinapaswa kutubadilisha. Na kwa njia hiyo baada ya muda, lakini pia na kukomaa kwa dhamiri za wanadamu, na ukuaji wa uwajibikaji kwa ujumla, tutafanya maendeleo. Tuna imani na moyo, pia shukrani kwa Waraka mpya, kuendelea na vita hivi", amehitimisha

10 Oktoba 2020, 17:00