杏MAP导航

Tafuta

Vijana wawili watakaotangazwa wakatifu wamewekwa kwenye Stemp za Italia. Vijana wawili watakaotangazwa wakatifu wamewekwa kwenye Stemp za Italia.  (ANSA)

Papa Leo XIV: Ombeni wenyeheri Pier Giorgio Frassati na Carlo Acutis zawadi ya imani ya kina!

Papa Leo XIV,mara baada ya Katekesi yake,Septemba 3,akisalimia wanahija wanaozungumza Kipoland kuhusiana na mwezi wa sala na watoto kurudi shuleni,alihimiza wao“waombe kwa maombezi ya Wenyeheri Pier Giorgio Frassati na Carlo Acutis,zawadi ya amani ya kina katika safari ya ukomavu.”

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV mara baada ya tafakari yake, pamoja na miito mbali mbali ametoa salamu kwa lugha mbali mbali, Jumatano tarehe 3 Septemba 2025. Papa alisema: “Ninawasalimu kwa moyo watu wa Poland! Mwezi  Septemba uwe mwezi wa maombi kwa watoto na vijana wanaorejea shuleni na kwa wale wanaojali elimu yao. Waombee, kwa maombezi ya Wenyeheri, na ambao watakiwa Watakatifu hivi karibuni, Pier Giorgio Frassati na Carlo Acutis, zawadi ya imani ya kina katika safari yao ya ukomavu. Ninawabariki kwa moyo wote!”

Uwanja wa Mtakatifu Petro wakati wa Katekesi
Uwanja wa Mtakatifu Petro wakati wa Katekesi   (@VATICAN MEDIA)

Kwa wanaozungumza kijerumani  Papa alisema “Wapendwa kaka na dada wanaozungumza Kijerumani, damu na maji yanayotiririka kutoka ubavuni mwa Yesu aliyesulubiwa inatuonesha upendo mkuu wa Mungu kwetu. Tusisahau kwamba Yeye pekee, Asiye na mwisho, anaweza kukata kiu yetu kwa ajili ya ukomo.”

Na kwa upande wanaozungumza kifaransa Papa alisema “Ninawasalimu kwa moyo mkunjufu waamini wanaozungumza Kifaransa, hasa mahujaji kutoka Luxembourg na Ufaransa. Kaka na dada, tujifunze ufundi wa kuomba bila aibu na kutoa bila hesabu, ili tujenge uhusiano wa kidugu, wa kweli na wa dhati,  wabeba furaha isiyojulikana kwa ulimwengu. Mungu awabariki ninyi na  familia zenu.”

Katekesi ya Papa
Katekesi ya Papa   (@Vatican Media)

Hatimaye, Papa aliwageukia mahujaji wanaozungumza kiitaliano na kusema kuwa “Ninawakaribisha kwa moyo mkunjufu mahujaji wanaozungumza Kiitaliano. Kwa namna ya pekee, nawasalimu waamini wa Jimbo kuu la Mantova, pamoja na Askofu Mario Busca, na waamini wa Jimbo kuu la Messina-Lipari-Mtakatifu Lucia wa Mela, pamoja na Askofu Mkuu Giovanni Accolla na Askofu Msaidizi. Wapendwa kaka na dada, ninatumaini kwamba hija yenu ya Jubile inaweza kuwa wakati mwa kina wa ushirika na Mungu; mnaporudi nyumbani, mtahisi kuimarishwa katika imani yako na kuchochewa kufanya mema.”

Kisha ninasalimia vikundi mbalimbali vya parokia, hasa zile za Carinaro, Ogliara, Lamporecchio, na Cologno al Serio, nikihimiza jumuiya zao kuzidi kujifungua kwa maisha mapya ambayo ni Kristo. Hatimaye, “ mawazo yangu yanageukia vijana, wagonjwa, na wenye ndoa wapya. Leo tunasherehekea ukumbusho wa kiliturujia wa Mtakatifu Gregory Mkuu, ambaye mwili wake unapumzika katika Kanisa kuu la Mtakatifu Petro. Papa huyu anaitwa "mkuu" kwa kazi yake ya kipekee kama mchungaji na mwalimu wa imani katika nyakati ngumu sana kwa jamii na Kanisa: "ukuu" uliopata nguvu kutokana na imani katika Kristo. Ninatumaini  kwamba kila mmoja wenu atatambua katika Bwana nguvu pekee ya kweli ya kuwepo. Baraka yangu kwa wote!

Katekesi ya Papa Leo XIV 3 Septemba 2025
03 Septemba 2025, 16:47