杏MAP导航

Tafuta

2025.09.05 Baraza la vijana wa Mediterania. 2025.09.05 Baraza la vijana wa Mediterania.  (@Vatican Media)

Papa Leo XIV kwa Baraza la Vijana wa Mediteranea wawe ishara za matumaini

Papa Leo XIV akikutana na Baraza la Vijana wa Mediteranea,alisema wao ni ishara ya matumaini na maelekezo yao ya juu na ubunifu huwaruhusu kutoa michango ya msingi kwa ajili ya amani katika eneo la Mediterania na duniani kote.Waendelee kuwa watangazaji wa Injili,Wapanzi wa amani na umoja."Muwe sauti ya wale wasio na sauti, na muwe wepesi,mwanga na chumvi mahali ambapo mwali wa imani na ladha ya maisha vinafifia.”

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV, Ijumaa tarehe 5 Septemba 2025 aliwaambia washiriki wa Baraza la Vijana la Mediterania kuwa wao ni "uthibitisho kwamba mazungumzo yanawezekana; kwamba tofauti ni chanzo cha utajiri na si chanzo cha migogoro; na kwamba wengine daima ni kaka na dada zetu,si wageni, au na mbaya zaidi adui. Mpango na Ishara za matumaini waendeleza na kuwa watangazaji wa Injili,na Wapanzi wa amani na umoja. Baraza hilo linaloundwa na wawakilishi kutoka nchi zinazopakana na Bahari ya Mediterania, linanuia kuwapa vijana fursa ya kutoa sauti zao na kuchukua hatua katika mazungumzo na mamlaka za kiraia.

Papa na kundi Baraza  la  Vijana wa mediteranea
Papa na kundi Baraza la Vijana wa mediteranea   (@Vatican Media)

Papa Leo XIV alisisitiza wakati akizungumza na vijana wa Mpango huo uliokabidhiwa na Papa Francisko, ili kurejesha uhusiano ambao umevunjika, kujenga upya miji iliyoharibiwa na vurugu, kufanya bustani kusitawi katika eneo ambalo sasa ni jangwa, kutia tumaini kwa wasio na tumaini, na kuwatia moyo wale walio na woga au ndugu zao wenyewe."Speaking in both Italian. Papa kwa kuzungumza kiitaliano na Kiingereza, aliendelea kusema kwamba “vijana wenyewe ndio ishara: ishara ya kizazi kisichokubali bila kukosoa kinachotokea, kisichoangalia upande mwingine au kungoja mtu mwingine kuchukua hatua ya kwanza.” Badala yake, Papa alisema, "Wanawakilisha kizazi ambacho kinatazamia maisha bora ya baadaye na kuchagua kusaidia kuijenga." Baba Mtakatifu aliwaalika vijana kuendelea kuwa ishara za matumaini kwa kumtolea ushuhuda Yesu Kristo, kwa kuwa watangazaji wa Injili yake, hasa katika eneo la Bahari ya Mediterania, ambao wanafunzi wa kwanza walitoka katika ufukwe wake.

Papa na vijana wa Mediteranea
Papa na vijana wa Mediteranea   (@Vatican Media)

Kwa waamini, wakati ujao ni wa kukubalika, unaokita mizizi katika urithi wa kiroho wa eneo hilo, na kukataa kufuru kwa wale ambao wangetumia vibaya mila hizo kwa kuzitumia kuhalalisha vurugu na migogoro ya silaha. Papa alisema “Tumeitwa kukuza sala na hali ya kiroho, pamoja na vitendo, alisema, kama vyanzo vya amani na mahali pa kukutana kati ya mila na tamaduni." Baba Mtakatifu Leo XIV alihitimisha hotuba yake kwa kuwaomba  vijana wasiogope, bali wapande mbegu za amani… “muwe na subira wajenzi wa umoja… muwe sauti ya wale wasio na sauti, na muwe wepesi, mwanga na chumvi mahali ambapo mwali wa imani na ladha ya maisha vinafifia.”

05 Septemba 2025, 15:34