杏MAP导航

Tafuta

2025.09.04 Ajali ya Mfumo wa waya ya usafiri(Elevador Gloria, Lisbon nchini Ureno. 2025.09.04 Ajali ya Mfumo wa waya ya usafiri(Elevador Gloria, Lisbon nchini Ureno. 

Papa Leo XIV aonesha huzuni kufuatia na ajali ya Mfumo wa Usafiri wa lift kudondoka huko Lisbon

Katika ujumbe wake wa Telegramu uliotiwa saini na Katibu Mkuu wa Vatican,Kardinali Parolin,Papa Leo XIV anawaombea wahanga na kueleza ukaribu wake wa kiroho kwa wale wote walioathiriwa Septemba 3 na ajali ya Mfumo wa usafiri wa lift ya Glória,iliyo sababisha vifo vya watu 17 na 23 kujeruhiwa.Kulingana na wazima moto,sababu ya ajali inaweza kuwa cable iliyovunjika.Septemba 5 ni siku ya maombolezo ya kitaifa nchini Ureno.

Vatican News.

Papa Leo XIV alituma "rambirambi zake za dhati" na "ukaribu wa kiroho" kwa familia zote zinazoomboleza mkasa wa kuanguka kwa Mfumo wa lifti ya Gloria huko Lisbon nchini Ureno uliotokea tarehe 3 Septemba 2025. Papa alifanya hivyo, tarehe 4 Septemba, katika telegram iliyoelekezwa kwa Patriaki wa Lisbon, Askofu mkuu Rui Manuel Sousa Valério S.M.M., iliyotiwa saini na Katibu Mkuu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin. Katika ujumbe wake, Papa anawaombea "ahueni kamili" waliojeruhiwa na kuwaombea "nguvu ya matumaini ya Kikristo kwa wale wote walioathiriwa na janga hilo," akiwakumbuka "kwa shukrani" wale wote walioshiriki katika shughuli za uokoaji.

Idadi ya vifo

Idadi ya waliofariki kutokana na kukatika na Mfumo lift ya Glória, huko Lisbon inafikia 17 waliokufa na 23 kujeruhiwa, wengi wao ni watalii. Taarifa kuhusu matokeo ya ajali iliyotokea alasiri ya Jumatano, tarehe 3 Septemba 2025, ilitolewa na mkurugenzi wa Huduma ya Ulinzi wa Raia wa mji mkuu wa Ureno, Margarida Castro Martins, ambaye alitoa maelezo zaidi kwamba: “Wakati wa usiku, vifo viwili vilitokea hospitalini. Waliopoteza maisha akiwemo dereva wa gari hilo ni wanaume saba na wanawake wanane, "wote ni watu wazima, wengine ni raia wa kigeni, na bado hatuna taarifa za umri wala uraia wa wahanga hao," Martins aliongeza. Kwa wakati huu, hakuna maelezo yoyote ambayo yametolewa juu ya hali ya waliojeruhiwa, lakini inajulikana kuwa "wanne ni Wareno, Wajerumani wawili, Wahispania wawili, Mkorea mmoja, Mcape Verde mmoja, Mkanada mmoja, Mwitaliano mmoja, Mfaransa mmoja, Mswiss mmoja na Mmorocco 1."

Nadharia zinazozungukia mkasa

Mfumo wa lift ya Glória, ni moja ya tatu katika mji mkuu wa Ureno, pamoja na Mnara wa kitaifa. Ukijumuisha mabehewa mawili, ulizinduliwa mnamo 1885 na unaunganisha sehemu ya chini na sehemu ya juu ya jiji. Unaweza kubeba hadi watu 45 na unatumiwa, kwa wastani, na takriban abiria milioni tatu kwa mwaka. Kulingana na kazi ya awali ya wazima moto ilielezea upya tukio hilo, ambalo Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Umma imefungua uchunguzi, huenda kebo ilishindwa na kusababisha hitilafu, kuanguka kwa moja ya lifti mbili, na kuanguka kwa jengo karibu na Praça dos Restauradores. Lakini kwa mujibu wa mafundi, ajali hiyo huenda ilisababishwa na hitilafu ya breki. Wakati huo huo, Carris, kampuni ya umma ya Ureno ambayo inasimamia Lift ya Glória, ilihakikisha kwamba "itifaki ya matengenezo ilifuatwa kwa uangalifu mkubwa."

Miitikio ya mkasa huo

Nchini Ureno, Waziri Mkuu Luis Montenegro alitangaza tarehe 5 Septemba kuwa siku ya maombolezo ya kitaifa, huku Rais Marcelo Rebelo de Sousa akitoa "rambirambi zake za kina." Ilikuwa "ajali mbaya sana, isiyo na kifani," alitoa maoni Meya wa Lisbon Carlos Moedas, ambaye alihudhuria shughuli za uokoaji Septemba 3 pamoja na Waziri wa Miundombinu Miguel Pinto Luz.

Umoja wa Ulaya pia ulionesha mshikamano wake kupitia Rais wa Bunge la Ulaya Roberta Metsola:

"Mioyo yetu inawaendea wahasiriwa wa mkasa wa lifti ya Glória, alama ya kihistoria kwa wakaazi wa Lisbon na wageni kutoka kote ulimwenguni. Ulaya inasimama katika mshikamano na waathirika, wapendwa wao, na jumuiya nzima ya Lisbon. Nawatakia ahueni ya haraka waliojeruhiwa."

Usaidizi huu ulisisitizwa tena na Rais wa Tume ya Ulaya, Bi Ursula von der Leyen: "Nilihuzunishwa kujua kuhusu kuharibika kwa Lifti maarufu ya Glória. Rambirambi zangu ziende kwa familia za waathiriwa." Bendera ziko nusu mlingoti katika makao makuu ya Ulaya.

04 Septemba 2025, 17:04