Papa katika Siku ya Familia ya Vatican:Tunahitaji ushuhuda wenu leo!
Na Salvatore Cernuzio - Vatican.
Viputo,michezo , slaidi zinazoweza kuwekwa upepo, stendi za chakula, na nafasi za kuchora na kupaka rangi, michezo, na muziki wa moja kwa moja. Lakini kivutio kikubwa zaidi kwa watoto wengi kilikuwa ni yeye: Papa Leo XIV, ambaye alikuja kusalimiana na mamia ya familia za wafanyakazi wa Jiji la Vatican waliokusanyika jioni ya tarehe 6 Septemba 2025 kwenye uwanja mbele ya Ofisi ya Gavana kwa ajili ya Tamasha la Familia. Tukio ambalo limekuwa likifanyika kwa miaka kadhaa, limezidi kuwa na sura nyingi na rangi. Tamasha hilo lililopangwa kufanyika mwezi Mei mwaka huu, liliahirishwa hadi mapema Septemba. Mamia ya akina mama na akina baba walikusanyika pamoja na watoto wao, wengi wao ambao walihudhuria Kambi ya Vatican majira ya kiangazi ya mwaka huu kwa ajili ya tukio hilo. Tukio hilo likawa tukio na kuonekana kwa Papa Leo. Akitoka nje ya mlango mkuu wa Gavana , baada ya ishara iliyotolewa na Padre Franco Fontana, Padre Msalesiani mratibu wa mapadre wa Kurugenzi na Ofisi Kuu, Papa aliwasalimia watoto wengi waliomkaribisha kwa vifijo, vigeregere na nderemo.
Papa Leo XIV katika sherehe ya familia ya mji wa Vatican (@Vatican Media)
"Sote tuwe familia ya Mungu"
"Habari! Jioni njema! Inapendeza sana kuwa wote pamoja, hasa kwenye likizo hii ya familia! Inapendeza kuwaona ninyi watoto wote: makofi kwa ninyi nyote!" Papa alianza. “Kama vile Mama na Baba wanavyowapenda ninyi, vivyo hivyo sote tunapokusanyika pamoja, tunapendana kikweli, kwa sababu sisi sote ni familia ya Mungu, pamoja na ndugu yetu, rafiki yetu wa karibu sana, Yesu,” Leo XIV alisema, huku akitabasamu kwa wasikilizaji wa matineja, watoto, na hata baadhi ya watoto wachanga. "Tukiwa na mioyo iliyofunguka namna hii, tunataka kujionea wakati huu mzuri sana," aliongeza, akisisitiza "furaha ya kuwa familia, furaha ya kuwa na umoja, kufanya urafiki kati yetu, kusherehekea zawadi, hasa zawadi ya uhai, zawadi ya familia, ambayo Bwana ametupatia."
Ushuhuda na dhabihu za familia
"Karibuni nyote! Asanteni kwa ukaribisho huu!" Papa Leo aliendelea, pia akiwahutubia wazazi. "Ushuhuda huu wa familia ni muhimu sana katika ulimwengu wetu leo!" alisema. "Nawashukuru ninyi nyote kwa ushuhuda huu na kwa uwepo wenu jioni hii, na kwa yote mnayofanya, wakati mwingine kwa kujitolea sana, kuishi pamoja kama familia, kueneza ujumbe huu, na hivyo kushiriki katika roho ambayo Yesu Kristo alituachia."
Piza kwa Papa Leo XIV (@Vatican Media)
Sala na Salamu
Kisha sala ya Salamu Maria na baraka maalum kwa wote waliohudhuria. Pembeni ya Papa alikuwa Gavana Dada Raffaella Petrini, pamoja na Makatibu Wakuu wawili, Monsinyo Emilio Nappa na Giuseppe Puglisi-Alibrandi. Nyuma yake kulikuwa na makadinali watatu, walioelezwa na Papa kama "zawadi maalum": Marais wawili Mstaafu Fernando Vergéz Alzaga na Giuseppe Bertello. Pia alikuwepo Kardinali Lorenzo Baldisseri, Katibu Mstaafu wa Sinodi ya Maaskofu. Baada ya salamu hiyo, Papa Leo alijitumbukiza katika umati wa watoto na wazazi wao. Kukumbatiwa, baraka kichwani, kubembeleza, kupeana mikono, na picha zilizotandazwa kwenye mraba mzima kwa takriban saa moja, katikati ya umati, hata ikijumuisha zawadi ya pizza ya Margherita na mozzarella iliyopangwa kwa umbo la "W Papa Leo XIV." Kisha picha chache zilipigwa na watumbuizaji na wacheza juggle kabla ya kurudi nyumbani kwake. Wakati wa furaha, kwa hakika: furaha ya kuwa familia, pamoja na Papa.
Mtoto kati ya watoto aliyekuwa katika sherehe (@VATICAN MEDIA)