杏MAP导航

Tafuta

2025.09.06Papa akutana na washitiki wa Kongamano la Kimataifa la Maria 2025.09.06Papa akutana na washitiki wa Kongamano la Kimataifa la Maria   (@Vatican Media)

Papa kwa washiriki wa Mafunzo ya Maria:Hujenga madaraja na hubomoa kuta&kusaidia wanadamu kuishi kwa amani

Papa Leo XIV amehitimisha kikao cha siku 4 cha Kongamano la XXVI la Kimataifa la Maria kwa hotuba katika Ukumbi wa Paulo VI,Vaticanhuku akiwashukuru washiriki takriban 600 wa mafunzo kuhusu Bikira Maria:"Mama Maria haachi kufungua milango,kujenga madaraja,kubomoa kuta na kusaidia binadamu kuishi kwa amani na utofauti.Kuwa na mtazamo wa Maria inasaidia watu na tamaduni kutemba kwa amani."

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV ametoa  hotuba yake ya kufunga Kongamano la 26 la Kimataifa la Maria, lililofanyika mjini Roma, kwenye Ukumbi wa Antonianum, kuanzia tarehe 3 Septemba hadi  tarehe 6 Septemba 2025 ambalo lilihamasishwa na Chuo cha Kipapa cha Kimataifa cha Maria. Kwa washiriki wa tukio hilo la siku nne karibu wasomi 600 wa Mafunzo ya Maria kutoka Mabara manne, walijikita na mjadala wa mada: "Jubilei na Sinodi: Kanisa lenye Uso na Matendo ya Maria." Kwa njia hiyo wakiwa katika Ukumbi wa Paulo VI, mjini Vatican, Baba Mtakatifu alitoa muhtasari wa mada na matokeo ya kazi yao.

Awali ya yote Papa alionesha furaha kuwapokeaa katika hitimisho la Kongamano la Chuo cha Kimataifa cha Maria na kumsalimia Rais, Katibu, Wajumbe wa Halmashauri Kuu, washiriki na wafadhili wote. Bikira Maria, Mama wa Kanisa, anatufundisha kuwa Watu watakatifu wa Mungu; ndiyo maana kuna umuhimu wa Chuo hiki cha Kipapa, jukwaa la mawazo, mambo ya kiroho na majadiliano, lenye jukumu la kuratibu masomo na wasomi wa Mafunzo ya Maria (Mariology), katika huduma ya ibada ya Maria halisi na yenye matunda. Katika Kongamano hili la 26, ikiwa mwelekeo wa Maria wa Kanisa ni mabaki ya zamani au unabii wa siku zijazo, wenye uwezo wa kukomboa akili na mioyo kutoka katika desturi na shauku ya "jamii ya Kikristo" ambayo haipo tena.

Washiriki wa Kongamano la Maria
Washiriki wa Kongamano la Maria   (@Vatican Media)

Papa Leo aliendelea kuwa katika Kongamano hilo, walijadili malengo na maadili ambayo ibada ya Maria inatoa kwa waamini, wakizingatia kama wanaunga mkono tumaini na faraja ambalo Kanisa limeitwa kutangaza.  Wametambua katika Jubilei na katika sinodi mada mbili za kibiblia na kitaalimungu zinazoelezea vyema wito na utume wa Mama wa Bwana. Kama mwanamke “mwenye furaha,” Maria daima yuko tayari kujibu kwa kusikiliza kwanza Neno, kulingana na tabia iliyoelezwa na Mtakatifu Augustino: “Wote wanashauriana nanyi kuhusu kile wanachotaka, lakini huwa hawasikii jibu wanalotaka. Mtumishi wako mwaminifu zaidi ni yule ambaye hatafuti kusikia kutoka kwako kile anachotaka, lakini badala yake kutaka kile anachosikia kutoka kwako” (Confessions, X, 26). Kama mwanamke wa “mtaguso”, anajishughulisha kikamilifu na kimama katika utendaji wa Roho Mtakatifu, ambaye huwaita wale ambao hapo awali waliamini kwamba walikuwa na sababu za kugawanyika kutokana na kutoaminiana na hata uadui kama kaka na dada (taz. Mt 5:43-48).

Kanisa lenye moyo wa Maria,  daima huhifadhi na kuelewa vyema uongozi wa  ukweli wa imani, kuunganisha akili na moyo, mwili na roho, ulimwengu na mahali, mtu na jamii, ubinadamu na ulimwengu. Ni Kanisa ambalo haliepuki kujiuliza yenyewe, wengine na Mungu maswali yasiyopendeza:  "hii itakuwaje?" (Lk 1:34) na kutembea katika mapito yenye kudai mengi ya imani na upendo: “Tazama, mimi ni mjakazi wa Bwana; na nitendewe kama ulivyonena”(Lk 1:38). Tamaduni za Maria na mazoezi yanayoelekezwa kwenye huduma ya matumaini na faraja hutuweka huru kutoka katika imani, ujuu juu na msingi; inachukua ukweli wote wa kibinadamu kwa uzito, kuanzia mdogo na uliotupwa; inachangia kutoa sauti na heshima kwa wale wanaotolewa dhabihu kwenye madhabahu za sanamu za kale na mpya.

Washiriki wa Kongamano la Maria
Washiriki wa Kongamano la Maria   (@Vatican Media)

Kwa kuwa wito wa Mama wa Bwana unaeleweka kuwa ni wito wa Kanisa, taalimungu  ya Maria ina jukumu la kukuza ndani ya Watu wote wa Mungu, kwanza kabisa, nia ya "kuanza upya" na Mungu, Neno lake na mahitaji ya jirani yetu, kwa unyenyekevu na ujasiri (taz. Lk 1:38-39). Inapaswa pia kukuza hamu ya kutembea kuelekea umoja unaobubujika kutoka kwa Utatu, ili kutoa ushuhuda kwa ulimwengu, kwa uzuri wa imani, matunda ya upendo na unabii wa matumaini usiokatisha tamaa. Kutafakari fumbo la Mungu na historia ya mtazamo wa ndani wa Maria hutulinda kutokana na upotoshaji wa propaganda, itikadi na habari zisizofaa, ambazo haziwezi kamwe kusema neno la kupokonya silaha na kunyang'anya silaha, na hutufungua katika uhuru wa kimungu, ambao peke yake hufanya iwezekane kwa watu, idadi ya watu na tamaduni kutembea pamoja kwa amani (rej. 36 Lk 26: 24).

Hii ndiyo sababu Kanisa linahitaji Mafunzo ya Maria(Mariology). Inapaswa kuzingatiwa na kukuzwa katika vituo vya kitaaluma, madhabahu na jumuiya za Parokia, Vyama na Harakati za Kanisa, taasisi za maisha ya kuwekwa wakfu, na pia mahali ambapo tamaduni za kisasa zinadanganya, tukithamini msukumo usio na kikomo unaotolewa na sanaa, muziki na fasihi. Katika miaka ya hivi karibuni, Chuo cha Maria pia kimezindua mipango mbalimbali ya kuendeleza sura na ujumbe wa Mama wa Yesu kama njia ya kukutana na mazungumzo kati ya tamaduni. Hakika, kama mshiriki kamili wa Roho Mtakatifu, Mama Maria haachi kufungua milango, kujenga madaraja, kubomoa kuta na kusaidia wanadamu kuishi kwa amani na upatano wa utofauti.

Washiriki wa Kongamano la Maria
Washiriki wa Kongamano la Maria   (@Vatican Media)

 

Baba Mtakatifu Leo XIV alikushukuru huduma hiyo ya kikanisa, ambayo inaendelea kutukumbusha kwamba Kanisa daima lina "uso" wa Maria na Hatua za Maria. Pia aliwapongeza wale ambao wamewasilisha kazi zao za muziki na kisanii kwa ajili ya tuzo ya kila mwaka ya kimataifa  ya: "Maria, Njia ya Amani kati ya Tamaduni." Papa Leo alihitimisha kwa kusema kuwa, Chuo chao  kiwe nyumbani na shule iliyo wazi kwa wale wote wanaotaka kujifunza  masomo yao ya Maria katika huduma ya Kanisa. Kwa njia hiyo ameombea na kuwapatia baraka zake na kuwashurkuru tena. Ikumbukwe walishiriki waliokutana na Baba Mtakatifu Leo XIV,walikuwa  makardinali, maaskofu, Mapadre, watawa, Mamlaka Mashuhuri za Kidini, Kiraia na Kijeshi, Mabalozi na Wanafunzi wa Mafunzo ya Maria (Mariology), kutoka Ulimwenguni kote.

Papa na washiriki wa Kongamano la Maria

 

06 Septemba 2025, 11:48