杏MAP导航

Tafuta

Nia za Maombi ya Papa Septemba 2025:‘Dunia ina matatizo mengi ya kusuluhisha’

Tunachapisha maandishi na sala ya Papa kwa njia ya Video kwa nia ya Sala ya Baba Mtakatifu kwa mwezi Septemba 2025,inayochapishwa na Mtandao wa Kimataifa wa sala za Papa,kwa kuongozwa na Mada:“Kwa ajili ya uhusiano wetu na Uumbaji wote:Tusali ili kwa kuhuishwa na Mtakatifu Francis wa Assisi,tunaweza kufanya uzofu wa kutegemeana kwetu na viumbe vilivyoumbwa na vyenye hadhi ya upendo na heshima.

Na Angela Rwezaula - Vatican.

“Kwa ajili ya uhusiano wetu na Uumbaji wote: Ndiyo mada ya Nia za Papa za sala kwa Mwezi Septemba 2025 zinazochapishwa na Mtandao wa Kimataifa wa Nia za sala ya Papa. Kwa hiyo Papa anaihimiza kwamba "Tusali ili kwa kuhuishwa na Mtakatifu Francis, tunaweza kufanya uzoefu wa kutegemeana kwetu na viumbe vyote, kupendwa na Mungu na kustahili kupendwa na kuheshimiwa.” Baba Mtakatifu kwa lugha ya kiingereza katika nia yake ya sala ya Mwezi Septemba anasali hivi:

Ee Bwana, wewe unapenda kila kitu ulichokiumba na hakuna kitu kilichopo nje ya fumbo la upole wako. Kila kiumbe, ambacho ni kidogo, ni tunda la upendo wake, na kina nafasi katika dunia hii. Hata maisha yaliyo rahisi au mafupi yamezungukwa na utunzaji wako. Kama Mtakatifu Francis wa Assisi, hata leo sisi tunataka kusema: Usifiwe Ee Bwana wangu!

Kwa njia ya uzuri wa uumbaji, unajionesha kama chemichemi ya wema. Tunakuomba; ufungue macho yetu ili tukujue, kwa kujifunza kutoka fumbo la ukaribu wake, kwa uumbaji wote, ambapo ulimwengu una matatizo mengi zaidi yasiyoisha ya kusuluhisha.

Ni fumbo la kutafakari kwa shukrani na tumaini. Utusaidie kugundua kwa uwepo wake wa uumbaji wote, ili kwa kujua wewe kikamilifu, tunaweza kuhisi na kujua ya kuwa wahusika wa nyumba hii ya pamoja, ambamo wewe unatualika kulinda, kuheshimu na kutetea maisha kwa aina zake zote na uwezekano. Asifiwe ee Bwana. Amina.” Papa anahitimisha.

Heshima ya maisha inatokana na kuheshimu asili

Video inayoambatana na nia ya maombi ya Papa inachanganya maadhimisho mawili: karne ya nane ya utunzi wa Wimbo  wa Sifa kwa viumbe na kumbukumbu ya miaka kumi ya kuchapishwa kwa waraka wa Papa Francisko wa Laudato si'. Kwa mujibu wa Kardinali Michael Czerny, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Fungamani ya Binadamu ambaye aliunga mkono utayarishaji wa video hiyo, Papa anatuhimiza tutafakari kuhusu uumbaji, “kuupatanisha, kuishi kwa amani, kuulinda kwa roho ya kinabii, kuheshimu kila mwanadamu, na kuendeleza amani ya kudumu na endelevu.

Uzuri wa dunia iliyounganishwa na  ubinadamu

"Ustawi wa mwanadamu hauwezi kutenganishwa na wakaaji wengine wa dunia na kwa  'afya' ya sayari yetu." Ndivyo asemavyo mkurugenzi wa kimataifa wa Mtandao wa Maombi ya Papa Ulimwenguni Pote, Padre Cristóbal Fones, ambaye anatualika kumtazama Mtakatifu Francis wa Asisisi kufanya uchaguzi rahisi wa maisha ya watumiani, ili yaweze kuwa "maisha ya msingi katika uhusiano wa kidugu na wengine na asili, na uhusiano wa kimwana, wa upendo na shukrani, na Mungu."

02 Septemba 2025, 16:31