杏MAP导航

Tafuta

2025.06.27 Santa Messa con Ordinazioni Sacerdotali. 2025.06.27 Santa Messa con Ordinazioni Sacerdotali.  (@Vatican Media)

Misa za Papa Leo XIV kwa mwezi Oktoba 2025

Papa ataadhimisha Jubilei kadhaa na katika miktadha mbali mbali kwenye Uwanja wa Mtakatifu Petro kwa mwezi Oktoba:Kutangazwa Wenyeheri 7 kuwa Watakatifu miongoni mwao ni Bartolo Longo na "daktari wa maskini" wa Venezuela,José Gregorio Hernández Cisneros.Kisha,mwishoni mwa mwezi,Misa kwa wanafunzi wa Vyuo Vikuu wanaohudhuria Vyuo Vikuu vya kipapa,ikiwa ni ufunguzi wa mwaka wa masomo 2025/2026.

Vatican News

Mwezi Oktoba kwa Papa Leo XIV, utakuwa na mwendelezo wa kuadhimisha Jubilei ya Matumaini kwa sherehe kadhaa katika Uwanja wa Mtakatifu Petro kuanzia tarehe 5 Oktoba, ambapo Baba Mtakatifu ataadhimisha Misa kwa ajili ya Jubilei ya Harakati za Kimisionari Duniani na Jubilei ya Wahamiaji, saa 4:30 asubuhi majira ya Ulaya. Siku nne baadaye, siku ya Alhamisi, tarehe 9 Oktoba, ataadhimisha Misa tena saa 4:30 asubuhi, masaa ya Ulaya katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, Jubilei ya Watawa Ulimwenguni.

Dominika  itakayofuata, tarehe 12 Oktoba 2025,  Baba Mtakatifu  Leo XIV ataongoza Misa ya asubuhi kwa ajili ya Jubilei ya Tasaufi ya Maria. Juma moja baadaye, tarehe 19 Oktoba saa 4:30 asubuhi, Dominika ya Kimisionari Ulimwenguni, Misa ya kutangazwa  kwa wenyeheri saba kuwa watakatifu imepangwa. Miongoni mwao ni wafia imani Ignatius Choukrallah Maloyan, Askofu Mkuu wa Kiarmenia wa Kikatoliki wa Mardin, aliyekufa wakati wa mauaji ya kimbari ya 1915, na Peter To Rot, mlei na katekista wa Papua, aliyeuawa mwaka wa 1945 kwa kufuata utume wake licha ya marufuku iliyowekwa na Wajapani. Atakuwa mtakatifu wa kwanza wa Papua New Guinea.

Watakaotangazwa kuwa watakatifu ni Vincenza Maria Poloni, mwanzilishi wa Taasisi ya Masista wa Huruma ya Verona; Maria wa Mlima Carmeli  Rendiles Martínez, mwanzilishi wa Shirika la Watumishi wa Yesu; na Maria Troncatti, mtawa wa Shirika la Mabinti wa Maria Msaada wa Wakristo. Pia tarehe 19 Oktoba, walei wawili watatangazwa kuwa watakatifu: José Gregorio Hernández Cisneros, daktari wa Venezuela na mwanachama wa Shirika la Wafransiskani Wasekulari, anajulikana kama "daktari wa maskini," ambaye aliwatibu na hata kulipia dawa zao; na Bartolo Longo, mwanzilishi wa Basilika ya Maria huko Pompeii, mtu anayependwa sana nchini Italia na duniani kote. Kuna wafiadini Ignazio Choukrallah Maloyan, Askofu Mkatoliki wa Kiarmeni wa Mardini, aliyekufa wakati wa mauaji ya kimbari kunako 1915, na Peter To Rot, Mlei na Katekista wa Papua New Guinea aliyeuawa kunako 1945 kwa sababu ya kuendeleza utume wake licha ya kukataliwa na ukoloni wa kijapani. Atakiwa Mtakatifu wa kwanza wa Papua New Guinea.

Hatimaye, tarehe 26 Oktoba, Papa ataadhimisha Misa katika Uwanja wa Mtakatifu Petro saa 4:00 kamili, Masaa ya Ulaya, kwa ajili ya Jubilei ya Vikundi vya Kisinodi na Vyombo Shirikishi. Haya ni makundi au watu binafsi ambao ni sehemu ya Baraza la kikanisa, Baraza la kichungaji, au baraza la mambo ya kiuchumi, linalofanya kazi katika ngazi ya Kijimbo, Kipatriaki, kitaifa, au mahalia. Siku ya Jumatatu, tarehe 27 Oktoba 2025, sherehe nyingine itaongozwa na Papa Leo XIV katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro saa 5:30 asubuhi, pamoja na wanafunzi kutoka Vyuo Vikuu vya Kipapa wakiwa katika Ufunguzi wa Mwaka wa masomo 2025/2026.

Ratiba ya Papa kwa mwezi Oktoba 2025
01 Septemba 2025, 19:27