杏MAP导航

Tafuta

Oaoa Leo atafungua mwaka wa Kichungaji wa Jimbo Kuu la Roma tarehe 19 Septemba 2024. Oaoa Leo atafungua mwaka wa Kichungaji wa Jimbo Kuu la Roma tarehe 19 Septemba 2024.  (@Vatican Media)

Ijumaa,Septemba 19 Papa Leo XIV atafungua mwaka wa kichungaji Jimbo Kuu Roma huko Lateran

Kardinali Baldo Reina Makamu wa Papa wa Jimbo Kuu la Roma katika barua aliyowaandikia waamini wote wa Jimbo kuu la Roma aliwajulisha kuhusu Baba Mtakatifu Leo XIV, atakutana kufungua rasimi mwaka mpya wa kichungaji 2025/2026 katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yohane huko Laterano Roma,tarehe 19 Septemba 2025.

Vatican News.

Baba Mtakatifu Leo XIV anatarajia  kufungua rasmi mwaka mpya wa kichungaji wa Jimbo kuu la Roma na kusanyiko la jimbo zima. Mkutano utafanyika alasiri ya Ijumaa tarehe 19 Septemba 2025, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yohane Laterano, Roma. Washiriki wanatarajiwa kuwasili na kukaribishwa saa 11:15 jioni; wakati  Baba Mtakatifu atawasili saa 11:45 Jioni ambapo  saa 12.00 saa za Ulaya, ataongoza Ibada ya Neno na kutoa miongozo ya kichungaji. Hotuba inatarajiwa kufungwa saa 1.30 za usiku.

Kwa vile hili ni tukio la kijimbo na lina viti 2,000, pamoja na mapadre wa Parokia, mapadre wasaidizi wa parokia, mashemasi, pia kutakuwa na walei watatu kutoka kila parokia, wawakilishi wa Baraza la Mashirika ya Walei, na wawakilishi wa taasisi za kitawa za kike na kiume.

Pasi zinaweza kuchukuliwa kwenye Vicariate, kwenye Ofisi ya Liturujia, kuanzia Jumatatu, tarehe 8 Septemba 8 (wakati wa saa za kazi). Tangazo rasmi la tukio hilo lilitolewa na Kardinali Baldo Reina Makamu wa Papa wa Jimbo Kuu la Roma katika barua aliyowaandikia waamini wote wa Jimbo kuu la Roma. "Tulipitia siku za neema wakati wa Jubilei ya Vijana na bdo tunathamini kumbukumbu yake na tunatumaini - zaidi ya yote - kuthamini kile tulichopata kwa uwepo na maneno ya Askofu wetu na kwa upendo wa vijana waliofika kwa wingi kutoka pande zote za ulimwengu." Pia alitafakari kuhusu hija ya Jimbo kuu huko Lourdes, inayohitimishwa tarehe Mosi Septemba 2025, ambapo “mwaka wa kichungaji unaokaribia kuanza uliwekwa mikononi mwa Maria na safari ya Kanisa letu ikakabidhiwa kwake.”

02 Septemba 2025, 21:15