Papa Leo XIV:Amani kwa Nchi Takatifu,Misaada ya Kibinadamu kwa Gaza na kukomesha kuhama kwa kulazimishwa
Na Angella Rwezaula – Vatican
Mara baada ya tafakari hiyo wakati wa salamu kwa lugha mbali mbali, kwa waamini na mahujaji waliunganika katika Ukumbi wa Paulo XIV, Mtakatifu Petro, na Ua la Petrine, tarehe 27 Agosti 2025 Papa Leo XIV alitoa wito kwa mara nyingine tena katika Nchi Takatifu, huko ukanda wa Gaza ambao unazidi kuleta wasi wasi juu ya watu wasio na hati. Papa alisema: “Ijumaa iliyopita,(22 Agosti 2025) tuliandamana na kaka na dada zetu wakiteseka kwa sababu ya vita na maombi na kufunga. Leo hii kwa mara nyingine tena ninatoa wito kwa pande zinazohusika na Jumuiya ya Kimataifa kukomesha mzozo katika Nchi Takatifu, ambao umesababisha vitisho vingi, uharibifu na vifo. Ninaomba kwamba mateka wote waachiliwe, usitishaji wa kudumu wa mapigano ufikiwe, uingiaji salama wa misaada ya kibinadamu uwezeshwe, na sheria ya kibinadamu iheshimiwe kikamilifu, hasa wajibu wa kuwalinda raia na makatazo ya adhabu ya pamoja, matumizi ya nguvu kiholela, na kulazimishwa kwa watu kuhama makazi yao.”
Baba Mtakatifu Mtakatifu katika hili ameonesha kuunga mkono mapatriaki wa Nchi takatifu kwamba “ Ninaunga mko “Azimio la Pamoja la Mababa wa Kanisa la Kiorthodox la Kigiriki na Wafuasi wa Upatriaki wa Kilatini wa Yerusalemu, ambao jana (26 Agosti 2025) walitoa wito wa kukomeshwa mfululizo huu wa vurugu, kukomesha vita, na kipaumbele kwa manufaa ya watu wote. Tumuombea Maria, Malkia wa Amani, chemchemi ya faraja na matumaini: maombezi yake yapate upatanisho na amani katika nchi hiyo inayopendwa sana na watu wote!”
Kwa wanaozungumza lugha ya kiitaliano Papa aliwakaribishwa kwa moyo mkunjufu mahujaji. Kwa namna ya pekee kabisa, “nawasalimu mapadre wa Jimbo kuu la Milano na waseminari wanaoshiriki katika mkutano wa majira ya kiangazi: wapendwa, ninawatia moyo kudumu kwa furaha katika kushikamana na Kristo, anayewaita kuwa mashahidi wa udugu na watenda kazi wa amani.” Kisha Papa alisema “ ninawasalimu waamini wa Romano huko Lombardy, Biancavilla, na Fossombrone, pamoja na Jumuiya ya Maria ya “Oasi della Pace” yaani Chemi chemi ya Amani ya huko Fara Sabina: marafiki wapendwa, ninabariki nia yenu njema na ninawasihi kuwa na uvumilivu kwa sala na Ekaristi.”
Hatimaye, “mawazo yangu yanageukia vijana, wagonjwa, na waliofunga ndoa wapya. Mtazame Kristo kwa uaminifu usioweza kushindwa, mwanga katika matatizo, usaidizi katika majaribu, na mwongozo katika kila dakika ya kuwepo kwa mwanadamu. Baraka yangu kwa wote! “