Velletri kutangazwa Jiji la Maria.Papa:Na iwe ni chachu ya ushuhuda wa Injili
Vatican News
Velletri, mji wa eneo la Castelli Romani, umekuwa chini ya vazi la ulinzi na uzazi la Bikira Mtakatifu tangu tarehe 26 Agosti. Na ndiyo tunayosoma katika ujumbe uliotiwa saini na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Mkuu wa Vatican ambaye alituma kwa niaba ya Baba Mtakatifu Leo XIV kwa Askofu wa Velletri-Segni-Frascati, Stefano Russo, katika fursa hiyo ya Kutatangwa kwa Velletri kuwa “Civitas Mariae" yaa “Mji wa Maria”
Katika baraka hiyo inabainisha kuwa: “Baba Mtakatifu Leo XIV anatoa Salamu za dhati kwa wale ambao watashiriki Maadhimisho makuu, wakati Velletri ikitangazwa kwa umma kuwa CIVITAS MARIA(“Mji wa Maria.”)Ni matumaini ya Baba Mtakatifu kuwa tuikio hilo ambalo Jumuiya inawekwa chini ya vazi la ulinzi na Umama wa Bikira Maria, liwawezeshe kupyaisha na udhati wa ibada kwa Mama, kwa kuhuisha waamini kuwa mashuhuda wakarimu wa kiinjili, kwa shauku na jitihada ya kuhamasisha wema wa pamoja na kwa kuishi vizuri katika hali ya makaribisho hasa kuelekea watu wadhaifu zaidi.”
Kwa matashi hayo Baba Mtakatifu anaomba kwa maombezi ya Mama wa Mwokozi , anayeheshimiwa na mji huo kama Mama wa Neema, awape msaada mwingi wa Mbinguni na kwa utashi wake anawatumia Baraka ya Kitume kwa mwashamu, mapadre, Mamlaka ya raia na wote walioko , lakini kwa wazo maalum kwa wagonjwa na wazee.” Baraka hiyo iliyosaniwa na Kardinali Parolin, Katibu Mkuu wa Vatican, ilitiwa saini tarehe 26 Agosti 2025.
Jana jioni, tarehe 26 Agosti saa 12.00 jioni masaa ya Ulaya , tangazo la umma na uhamisho wa sanamu ya Mari kwenye Jumba la Jiji, ambapo maandishi ya kumbukumbu yalitolewa, yalifanyika. Hii ilifuatiwa na maandamano hadi Kanisa kuu, ikifuatiwa na Misa Takatifu iliyoadhimishwa na Askofu Russo. Kwa upade wake tangazo la "Civitas Mariae" ni "wito kwa ahadi ya pamoja ambayo inaalika kila mmoja wetu kuwa mpatanishi katika maisha yetu ya kila siku na kuishi uwajibikaji pamoja kama ishara thabiti ya imani."
Utambuzi huu unakusudiwa kuwa "dira kwa maisha ya kila mtu," aliongeza Askofu Russo, "ambayo inaongoza sasa na kufungua njia ya siku zijazo." Wito wa "kuwa jiji la kukaribisha na kushirikisha watu wote," "mwaliko wa kubadilisha tofauti kuwa utajiri na kukuza kukutana kama njia ya matumaini," na kuwa wapenda amani.”