Watoto wawili wauawa kwa kupigwa risasi katika shule Katoliki nchini Marekani.Papa anaonesha huzuni
Vatican News
Papa Leo XIV alielezea masikitiko makubwa" kuhusu ufyatuaji risasi katika Kanisa la Kupashwa habari huko Minneapolis. Hii ni kwa mujibu wa barua iliyotiwa saini na Kardinali Pietro Parolin, Katibu Mkuu wa Vatican iliyotumwa na Baba Mtakatifu kwa Askofu Mkuu Bernard Hebda wa Mtakatifu Paulo na Minneapolis nchini Marekani. Mkasa huo kwa sasa una wahanga wawili, ambao ni watoto wote wenye umri wa miaka 8 na 10—na majeruhi 17 wakiwemo watoto wengine 14, saba kati yao hali zao ni mbaya. Mwanamume aliyefyatua risasi, kupitia madirishani mhali ambamo watoto waliokuwa wameketi kwenye viti wakati wa Misa, lililoko ndani ya eneo la shule, anaaminika kujitoa uhai.
Maombi kwa wale wanaoomboleza "kupoteza mtoto"
Papa, katika maandishi hayo: "anatoa rambirambi zake nyingi pamoja na hakikisho la ukaribu wake wa kiroho kwa wale wote walioathiriwa na janga hili baya," hasa kwa familia "ambazo sasa zinaomboleza kifo cha watoto." Aidha Papa Leo XIV "anakabidhi roho za watoto waliokufa kwa upendo wa Mungu Mwenyezi" na anahakikishia sala zake "kwa waliojeruhiwa, na vile vile waokoaji, wafanyakazi wa matibabu na washiriki, mpadre wanaowajali na wapendwa wao."
Baraka kwa Jumuiya mahalia
Telegramu inahitimishwa na Baraka ya Kitume iliyotolewa na Papa Leo XIV kwa jumuiya ya Shule ya Kikatoliki ya Kupashwa habari kwa Jimbo kuu la Mtakatifu Paulo na Minneapolis, na kwa wakazi wote wa eneo la miji mikuu ya Twin Cities, kama "ahadi ya amani, nguvu, na faraja katika Bwana Yesu."
Sababu zinachunguzwa
Sababu ya shambulio hilo lililotokea misa ya (saa 9:30 alasiri za Italia) tarehe 27 Agosti ambalo lilimfanya mtu mmoja kuwafyatulia risasi wamini waliokusanyika katika Kanisa Katoliki la Kupashwa habari huko Minneapolis, jiji kubwa la Minnesota, haijulikani. Shambulio hilo lilitokea saa 2:30 asubuhi kwa saa za ndani , Marekani wakati wa Misa ya mwanzo wa mwaka wa shule. Ndani humo limezungukwa Shule ya watoto kuanzia shule ya awali hadi ya kati. Saa chache tu baada ya kupigwa risasi ndipo Polisi waliripoti kwamba angalau watoto wawili, wenye umri wa miaka 8 na 10, waliuawa na wengine 14 walijeruhiwa. Inasemekana kwamba mshambuliaji alijiua. Kulingana na ripoti za vyombo vya habari vya ndani, watoto sita waliojeruhiwa katika shambulio hilo walilazwa hospitalini.
Gavana wa Minnesota
"Nimearifiwa kuhusu tukio la kupigwa risasi katika Shule ya Kikatoliki ya Kupaswaha habari na nitaendelea kutoa taarifa kadri tunavyopokea taarifa zaidi," Gavana wa Minnesota Tim Walz alisema. Aliongeza, "Nawaombea watoto wetu na walimu, ambao siku yao ya kwanza shuleni iliyogubikwa na kitendo hiki cha kutisha cha ukatili."
Rais wa Marekani
Hata Rais Donald Trump pia alitumia mitandao yake ya kijamii: "Nimesasishwa kuhusu tukio la kusikitisha la Minneapolis, Minnesota. FBI ilijibu haraka na tayari iko kwenye eneo ikiendelea na uchunguzi zaid. Ikulu ya White House itaendelea kufuatilia hali hii mbaya. Ninaaalika kuungana nami katika kuwaombea wote wanaohusika!"