Papa:Wakristo wawe wajenzi wa upatanisho katika ulimwengu uliojeruhiwa
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu amewatumia Ujumbe washiriki wa Juma la Kiekumene huko Stockholm ulifunguliwa tarehe 18 na hutahimishwa tarehe 24 Agosti 2025, katika muktadha wa maadhimisho ya miaka 100 ya kongamano la kiekumene la Kikirsto ulimwenguni juu ya maisha na kazi mwaka 1925 pamoja na miaka 1700 ya Mtaguso wa kwanza wa kiekumene wa Nicea. Katika ujumbe huo Papa anabainisha kuwa ni tukio la nguvu katika historia ya kikristo. Kunako mwaka 325, maaskofu kutoka ulimwenguni kote waliunganika huko Necea. Kwa kuthibitisha umungu wa Yesu Kristo walitoa Kanuni ya Imani kuwa “Yeye ni Mungu kweli kutoka kwa Mungu wa kweli, ya kuwa mmoja na Baba.” Waliweza kuweka imani hivi ambayo inaendelea kufungamanisha Wakristo kati yao. Mtaguso huo ulikuwa ishara ya ujasiri wa umoja katika utofauti, ushuhda wa kwanza wa kuamini kuwa imani yetu ya pamoja inaweza kushida migawanyiko, na kuamasisha ushirika.
Baba Mtakatifu anabainisha kuwa shauku inayofanana, iliuhishwa na Kongamano la mwaka 1925 huko Stockholm, lililoitishwa na mwanzilishi wa kwanza wa kiekumene, Askofu Mkuu Nathan Söderblom, ambapo enzi zile alikuwa Askofu Mkuu wa Kiluteri wa Uppsala. Mkutano uliwaona viongozi 600 wa kiekumene, kianglikani na kiprotestanti. Söderblom alikuwa anaamini kwamba: “huduma inaunganisha.” Na kwa njia waliibuka kaka na dada zake wakristo kutoweza kusubiri uwepo wa ruhusa kuhusu mtazamo wa taalimungu, lakini wa kuungana katika“Ukristo wa vitendo” ili kuhudumia pamoja Ulimwengu katika kutafuta amani, haki na hadhi ya binadamu.
Papa Leo XIV aliongeza kuwa: “ingawa Kanisa Katoliki halikuwakilishwa katika mkutano huo wa kwanza, ninaweza kuthibitisha kwa unyenyekevu na kwa shangwe kwamba leo hii tunasimama pamoja nanyi tukiwa wanafunzi wenzenu wa Kristo, tukitambua kwamba kinachotuunganisha ni kikubwa zaidi kuliko kinachotutenganisha.” Tangu Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican, Kanisa Katoliki limekumbatia kikamilifu safari ya kiekumene. Hakika, Hati ya Unitatis Redintegratio, ya Kanuni ya upatanisho juu ya uekumene, ilitualika katika mazungumzo katika udugu wa unyenyekevu na upendo, unaokita mizizi yake katika ubatizo wetu wa pamoja na utume wetu wa pamoja ulimwenguni. Tunaamini kwamba Kristo anatamani umoja kwa Kanisa lake ambalo lazima uonekane, na kwamba umoja huo unakua kupitia mazungumzo ya kitaalimungu, ibada ya pamoja inapowezekana, na ushuhuda wa pamoja katika uso wa mateso ya wanadamu.
Papa Leo anabainisha kwamba tangu Mtaguso wa II wa Vatican, Kanisa Katoliki limekumbatia kabisa safari ya kiekumene. Wito huu kwa ushuhuda wa pamoja unapata usemi wenye nguvu katika mada iliyochaguliwa kwa Juma hili la Kiekumene: "Wakati wa Amani ya Mungu." Ujumbe huu unafaa zaidi. Ulimwengu wetu una makovu makubwa ya migogoro, ukosefu wa usawa, uharibifu wa mazingira, na hisia inayoongezeka ya kutengwa kwa kiroho. Hata hivyo katikati ya changamoto hizi, tukumbuke kwamba amani si mafanikio ya kibinadamu tu, bali ni ishara ya uwepo wa Bwana kati yetu. Hii yote ni ahadi na kazi, kwa kuwa wafuasi wa Kristo wameitwa kuwa mawakala wa upatanisho: kukabiliana na mgawanyiko kwa ujasiri, kutojali kwa huruma, na kuleta uponyaji ambapo kumekuwa na majeraha.
Utume huu umeongeza nguvu asante kwa misingi adhumu ya kiekuemene. Kunako 1989 Papa Yohane Paulo II alikuwa Papa wa Kwanza kutembelea Sweden na kupokelewa kwa shange katika Kanisa Kuu la Uppsala, la Askofu Mkuu Bertil Werkström, na Mkuu wa Kanisa la Sweden. Wakati huo ulitoa ishara mpya katika mahusiano kati ya wakatoliki na waluteri. Na baadaye ilifuatilia kumbukumbu ya Pamoja ya Mageuzi ya Lund, kunako 2016 wakati Papa Francisko aliungana na viongozi wa kiluteri katika sala na kitubio cha pamoja. Hapo tulithibitisha safari yetu ya pamoja ya kushirikishana kutoka katika mgogoro hadi muungano.”
Baba Mtakatifu Leo XIV alieleza kuwa wakati wa Juma hili la majadiliano, na maadhimishi ya pamoja, anayo furaha kwamba wawakilishi wake wanaweza kuwapo kama ishara ya juhudi za Kanisa katoliki kuendelea katika safari ya sala na kazi ya pamoja, kila mahali iwezekanavyo, kwa ajili ya amani, haki na wema wa wote. Roho Mtakatifu ambaye aliuhisha Mtaguso wa Nicea na ambaye anaendelea kutuongoza sisi sote, aweza katika Juma hili, kuwa katika urafiki wa kina zaidi na kuamsha matumaini mapya kwa ajili ya umoja ambao Bwana anatamani hivyo kwa shauku kati ya wafuasi wake. Katika Juma hili, Papa anaomba amani ya Kristo iwe pamoja nao wote.