Papa Leo XVI:kukabiliana na migogoro kwa uwelewa na uvumilivu!
Vatican News.
"Kushughulikiachangamoto na migogoro ya sasa kwa kufuata mfano wa watakatifu kama Mtakatifu Alphonsus Maria de' Liguori, "ambao walijua jinsi ya kupata mchanganyiko uliosawazishwa kati ya matakwa ya sheria ya Mungu na mienendo ya dhamiri ya mwanadamu na uhuru, huku wakikuza mtazamo wa upendo, uelewa, na subira na hivyo kuwa ishara inayoonekana ya huruma ya Mungu isiyo na kikomo," ndiyo mwaliko wa Baba Mtakatifu Leo XIV alioutoa katika telegramu iliyotumwa kwa waandaaji na washiriki wa Kongamano la XVII la Kimataifa la Taalimungu ya Maadili, linalofanyika Bogota, nchini Colombia, kuanzia tarehe 20 hadi 21 Agosti 2025.
Kongamano hilo liliandaliwa na Mfuko wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Alfonsi, kwa kushirikishana na Taasisi ya Kipapa ya Alphonsianus ya Elimu na mfuko wa Déjame Nacer, kwa kuongozwa na mada: “ Maadili katika Karne ya 21: Mabadiliko na Migogoro katika Jamii, Jinsia, Akili Unde(AI,) na Ikolojia Fungamani." Katika telegramu iliyotiwa saini na Katibu Mkuu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin na kuelekezwa kwa Mkuu wa Mfuko wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Alfonsi, Padre Oscar Báez Pinto, Papa Leo XIV pia alielezea matumaini yake kwamba: "siku hizi zitakuwa ni tukio la kutafakari juu ya changamoto za sasa, mabadiliko, na migogoro katika nuru ya ufunuo wa Mungu, unaopata utimilifu wake katika Yesu Kristo." Hatimaye, akiomba ulinzi wa Bikira Maria, Baba Mtakatifu Leo amewapa Baraka zake za Kitume washiriki wote na familia na wapendwa wao.