杏MAP导航

Tafuta

2025.08.29 Ujumbe  wa Shule ua Uinjilishaji ya "Mtakatifu Andreas" 2025.08.29 Ujumbe wa Shule ua Uinjilishaji ya "Mtakatifu Andreas"  (@Vatican Media)

Papa Leo XIV kwa Shule ya Mtakatifu Andrea:kila Mbatizwa aeneze alichokipokea!

Papa Leo XIV akikutana na Ujumbe kutoka Shule ya Uinjilishaji ya Mtakatifu Andrea waliwa mjini Roma kwa hija ya Jubilei ya Mwaka Mtakatifu, tarehe 29 Agosti 2025 ametoa“mwaliko kwa namna ya pekee kutafakari maisha ya watakatifu ambao kama Yohane Mbatizaji,walikuwa waaminifu wafuasi wa Yesu Kristo,kwa kujionesha katika Neno na katika matendo mema.”

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV amekutana mjini Vatican,  Ijumaa tarehe 29 Agosti 2025 na Ujumbe kutoka Shule ya Uinjilishaji ya “Mtakatifu Andrés. ” Kama kawaida ya Papa alianza kwa  kuwatakia amani wote, na kuwakaribisha mjini Roma katika mwaka huu wa Jubilei  ambapo wengi wanatoka Nchi mbali mbali kama wanahija wa matumaini. Aliwakaribisha na kumsalimia Kardinali Gérald Cyprien Lacroix, Askofu Mkuu wa  Québec, aliyewasindikiza,  Bwana  José Prado Flores na wajumbe wote wa Shule hiyo ya Unjilishaji ya “Mtakatifu Andrés” waliokuwapo.

Papa akihutubia Shule ya Uinjilishaji
Papa akihutubia Shule ya Uinjilishaji   (@Vatican Media)

Papa Leo XIV akikumbuka kumbukizi ya Liturujia ya Siku, amebainisha kuwa “ Leo hii Kanisa la Ulimwengu linaadhimisha kumbu kumbu ya kiliturujia ya Kifodini cha Mtakatifu Yohane Mbatizaji.” Kwa njia hiyo kuwa aliongeza kusema kuwa “wasifu wake unaweza kutusaidaia sana kutafakari juu ya utume wake wa uinjilishaji katika dunia ya sasa. Katika mwanzo wa Injili ya Mtakatifu Yohane, anathibitisha kuwa: “ Ni Neno lililofanyika Mwili na kuja kukaa katikati yetu(Yh 1,14) na kisha anaelekeza Yohane Mbatizaji, kama alitoa ushuhuda (Yh 1,15).

Ikiwa  tunasoma kwa umakini sura 4 za kwanza za Injili,  tunaweza kugundua, ni ufungua gani wa kila shule ya Uinjilishaji yaani: Kutoa ushuhuda kwa kile ambacho kimetafakariwa, ya Mkutano  uliofanyka na Mungu katika maisha. Kwa njia hiyo Papa alikazia “Mwinjili anatueleza hata katika barua yake ya kwanza kwamba : “hilo tuliloliona na kulisikia, twawahubiri na ninyi; ili nanyi pia mpate kushirikiana nasi: na ushirika wetu ni pamoja na Baba, na pamoja na Mwana wake Yesu Kristo”(1Yh 1,3).” Kwa kuongeza: “Huu ndiyo utume wa Kanisa na wa kila Mkristo.”

Wajumbe wa Shule ya Uinjilishaji
Wajumbe wa Shule ya Uinjilishaji   (@Vatican Media)

Baba Mtakatifu kadhalika alisema, “ huu ni wito wetu kama wabatizwa, na kwa njia hiyo tunapaswa kueneza kile ambacho kwa mara nyingine tulipokea, ili wote waweze kuwa wamoja katika Kristo. Katika siku hizi za hija Papa Leo XIV,  ametoa “mwaliko kwa namna ya pekee kutafakari maisha ya watakatifu ambao kama Yohane Mbatizaji, walikuwa waaminifu wafuasi wa Yesu Kristo, kwa kujionesha katika neno na katika matendo mema. Kwa kuhitimisha aliwashukuru kwa kazi yao wanayopeleka mbele kwa ajili ya Uinjilishaji, kupitia vyombo mbalimbali, na aliwatia moyo kuendelea kutembea kwa upyaisho wa matumaini. Na Mungu awabariki na Mama Yetu wa Guadalupe awalinde daima katika utume wao. Safari njema .”

Papa kwa Shule ya Uinjilishaji

 

29 Agosti 2025, 16:07