Papa Leo XIV:Mazungumzo yasaidie kuhudumia jamii katika upatanisho na maelewano!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Katika telegramu iliyotiwa saini na Kardinali Parolin,Katibu Mkuu wa Vatican,Papa Leo XIV alimwandikia Kardinali Sebastião do Rosário Ferrão wakati wa maadhimisho ya mwaka wa 400 wa kuwasili nchini India kwa Mjesuiti wa kwanza wa Kilithuania,Padre Rudamina:ushuhuda wake"unahimiza wengi katika wakati wetu wa kujibu kwa uvumilivu sawa na kazi ya Uinjilishaji."
Matashi mema ya Papa Leo XIV
Baba Mtakatifu ametuma telegram yake iliyotiwa Saini na Kardinali Parolin Katibu Mkuu wa Vatican, kwa washiriki wa maadhimisho ya miaka 400 ya kuwasili nchini India kwa Mjesuit wa kwanza wa kilithuania Padre Andrius Rudamina, SJ. Katika Telegram hiyo imeelekezwa kwa Kardinali Filipe Neri António Sebastião Rosário Ferrão, Askofu ambapo Baba Mtakatifu Leone XIV anatuma “salamu za dhati na kutoa matashi mema kwa wote ambao wameunganika huku katika Kanisa Kuu la Old Goa ili kufanya kumbukizi ya miaka 400 ya kufika nchini humo.
Ujumbe unaookoa wa Injili kwa watu wote
Kwa kuungana na kushukuru Mwenyezi Mungu, kwa ushuhuda wa padre huyo mmisionari, ambaye imani yake thatibi katoliki inaonekana bado leo hii huko Lithuania, Baba Mtakatifu Leo “anasali ili katika maadhimisho ya ukarimu mkubwa hivyo na ujasiri katika kupeleka ujumbe unaookoa wa Injili kwa watu wote, uwatie moyo wengi, wakati wetu kwa kujibu kwa uvumilivu sana na kujua wajibu wa shughuli za uinjilishaji.”
Mwaka wa Jubileo:kuhudumia jamii nzima iwe mfano wa maelewano kidugu
Papa aidha “anawakabidhi kujenga juu ya msingi imara wa kimisionari wa Padre Rudamina na umarufu wake usio na kifani wa kufanya mazungumzo, ya ushirikiano wa kiutamaduni, Wakristo wa Kanisa hilo mahalia” wanahimizwa, hasa katika “mwaka huu wa Jubilei, unaojikita juu ya matumaini, kuhamasisha mazungumzo, yawe ya kiekumene na yale ya kidini ambayo yanaweza kuhudumia jamii nzima kama mfano wa maelewano ya kidugu, upatanisho na maelewano.” Kwa hisia hizo, Baba Mtakatifu anatoa kwa moyo Baraza za kitume kwa wote waliopo na kuzipanua kwa familia zao, kama jitihada ya furaha na amani katika Bwana Yesu Kristo.”