杏MAP导航

Tafuta

2025.08.23 Papa akutana na kikundi cha ujumbe wa wakimbizi kutoka Chagos - Port Louis. 2025.08.23 Papa akutana na kikundi cha ujumbe wa wakimbizi kutoka Chagos - Port Louis.  (@Vatican Media)

Papa Leo XIV:hakuna watu wanaoweza kulazimishwa kwenda uhamishoni

Papa Leo XIV akutana na ujumbe kutoka Kundi la Wakimbizi la Chagos,ambapo alikumbuka mateso na dhamira,hasa ya wanawake wa Chagossia,katika kudai haki zao kwa amani.Watu,hata wale wadogo na wanyonge zaidi,lazima waheshimiwe na wale walio na mamlaka katika utambulisho wao.Kwamba hakuna watu wanaweza kulazimishwa kwenda uhamishoni.Aliwahimiza kutazamia siku zijazo,wakitumaini neema ya msamaha.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV Jumamosi tarehe 23 Agosti 2025, alikutana mjini Vatican na wawakilishi wa Kikundi cha Wakimbizi wa Chagos ambao wanajikita na shughuli za kurudi kwa wakimbizi katika  Visiwa vya Chagos vya Jamhuri ya Mauritius. Suala hili lilihitimishwa mwezi Mei 2025 kwa nchi ya Uingereza kutia saini mkataba unaoruhusu kusitishwa kwa visiwa hivyo katika nchi hiyo ya Kiafrika na matengenezo ya kambi ya kijeshi ya Marekani kwenye kisiwa cha Diego Garcia, katika Bahari ya Hindi.  Papa Leo akianza hotuba yake alisema:“ Ninawasalimu kwa moyo mkunjufu, wajumbe wa Kikundi cha Wakimbizi cha Chagos, ambao wamevumilia kwa miaka mingi kurudishwa kwao kwenye visiwa vyao. Ninamuunga mkono kabisa Hayati  Papa Francisko, ambaye mlikutana naye mnamo Juni 2023 na  ambaye aliwatia moyo katika matendo yenu."

Papa akutana na wawakilishi wa wakimbizi wa Chagos
Papa akutana na wawakilishi wa wakimbizi wa Chagos   (@Vatican Media)

Papa Leo aliendelea kusema kwamba miwili baadaye, ameonesha furaha kwamba kazi yao wamepata mafanikio makubwa, kwani kurejea kwa Visiwa vya Chagos katika Jamhuri ya Mauritius kuliidhinishwa hivi karibuni na kutiwa saini kwa mkataba. Hii ni hatua muhimu kuelekea kurudi kwao nyumbani. Papa ameshiriki furaha yao na matumaini yao. Kwa pamoja, aliongeza: “tumshukuru Mungu, tukirudia maneno mazuri ya zaburi: “Bwana ametutendea mambo makuu; ametujaza furaha! ... Wapandao kwa machozi watavuna kwa vigelegele vya furaha” (rej. Zab 125).”

Papa alikutana na kikundi cha wawakilishi wa wakimbizi wa Chagos
Papa alikutana na kikundi cha wawakilishi wa wakimbizi wa Chagos   (@Vatican Media)

Papa aliwashukuru wahusika wote ambao, kwa kufungua mioyo yao, walielewa mateso ya watu wao na kufikia makubaliano haya. Furaha ya Papa Leo, pia ni kwamba “mazungumzo na heshima kwa maamuzi ya sheria za kimataifa, kama mtangulizi wake alivyotarajia aliporejea kutoka ziara yake ya kitume ya Mauritius, hatimaye yameweza kurekebisha dhuluma mbaya (Mkutano wa Wanahabari, Septemba 10, 2019). Kwa njia hiyo  Papa Leo XIV  alitoa pongezi  kwa azma ya watu wa Chagos, na hasa ile ya wanawake, katika kudai haki zao kwa amani. Matarajio mapya ya kurudi kwao katika visiwa vyao vya asili ni ishara ya kutia moyo na ina nguvu ya ishara katika hatua ya kimataifa: watu wote, hata wale wadogo na walio hatarini zaidi, wanapaswa kuheshimiwa na wenye nguvu katika utambulisho na haki zao, hasa haki ya kuishi katika nchi zao wenyewe; na hakuna anayeweza kuwalazimisha kwenda uhamishoni kwa lazima.”

Papa na kikundi cha wawakilishi wa wakimbizi wa Chagos
Papa na kikundi cha wawakilishi wa wakimbizi wa Chagos   (@Vatican Media)

Papa ameeleza matumaini kwamba mamlaka ya Mauritius na jumuiya ya kimataifa itafanya kazi ili kuhakikisha kwamba kurudi kwao, baada ya miaka 60, kunafanyika chini ya hali bora zaidi. Kanisa mahali halitakosa kutoa mchango wake, hasa wa kiroho, kama lilivyofanya siku zote nyakati za majaribu. Miaka hii ya uhamisho imesababisha mateso mengi miongoni mwao. Wamejua umaskini, dharau, na kutengwa. Bwana, kwa matumaini ya maisha bora yajayo, awaponye majeraha yao na awape neema ya msamaha kwa wale waliowadhuru. Katika hilo Papa amewaalika kutazama kwa uthabiti siku zijazo. Bikira Maria akwasindikize na kuwalinda wao na familia zao. Kwa moyo alitoa Baraka yake ya Kitume kwao na  Wachagos  wote.

Hotuba ya Papa kwa Kundi la Chagos
23 Agosti 2025, 15:02