杏MAP导航

Tafuta

Papa Leo XIV:Tuombe na Maria,Malkia wa Mashahidi,atusaidie kuwa mashuhuda na wajasiri!

Katika muktadha wa Injili ya Siku ambayo Yesu anasema hakuja kuleta amani duniani,bali moto na ambao tayari amewasha,Papa kabla ya Sala ya Malaika wa Bwana,Agosti 17:“Kutenda katika ukweli kuna gharama,kwa sababu katika dunia hii kuna anayechagua uongo,kwani shetani mara nyingi anatumia kutafuta namna ya kuweka vizingiti kwa wale watendao mema.Lakini Yesu anatualika,tusikate tamaa na kufanana na mawazo hayo,bali kuendelea kutenda wema wetu."

Na Angella Rwezaula – Vatican.


Na Baba Mtakatifu Leo XIV akitoa tafakari yake kabla ya Sala ya Malaika wa Bwana akiwa katikaJengo la kipapa,  mbele ya lango kuu huko Castel Gandolfo, tarehe 15 Agosti 2025, alisema: “Injili ya leo inatuwakilisha andiko gumu(Lk12,49-53),ambamo Yesu, kwa picha kali na uwazi mkubwa, anawambia wanafunzi wake juu ya utume wake, na hata wale ambao wanamfuata, ambao sio kazi rahisi, lakini ishara ya mafarakano….(Lk 2,34). Kwa kusema hivyo, Yesu anatanguliza kile ambacho atapaswa kukabiliana nacho, wakati Yesu atakapokwenda Yerusalemu, atakuwa mateka, atakamatwa, atatukanwa, kupigwa na kusulubishwa; wakati ujumbe wake licha ya kuzungumza upendo na haki, atakataliwa; na wakati viongozi wa watu watamgeuka na watamshambulia kuhusu mahubri yake.

Sala ya Malaika wa bwana Castel Gandolfo
Sala ya Malaika wa bwana Castel Gandolfo   (@VATICAN MEDIA)

Zaidi ya yote, jumuiya nyingi ambamo mwinjili Luka alikuwa akiwaelekea kwa maandishi yake, alikuwa akiishi uzoefu ule ule. Alikuwa kama vile kitabu cha Matendo ya mitume kisemavyo kwa jumuiya ya amani ambayo licha ya vizingiti vyake ilikuwa ikitafuta kuishi vema ujumbe wa upendo wa Mwalimu (Mdo 4,32-33). Pamoja na hayo walikuwa wanateseka mateso hayo. Papa Leo XIV aliendelea kuwa: “Hayo yote yanatukumbusha kuwa si kwamba wema daima unapata ukaribu wa jibu chanya. Badala yake wakati huo huo hasa kwa sababu ya uzuri wake unasumbu wale ambao hawaupokei, wale ambao wanautenda wanashia kukutana na upinzani mgumu, hadi kufikiwa mateso ya nguvu na kukataliwa.

Papa alisema “Kutenda katika ukweli kuna gharama, kwa sababu katika dunia hii kuna anayechagua uongo, na kwa sababu ya shetani anatumia mara nyingi kutafuta namna ya kuweka vizingiti kwa wale watendao mema. Yesu lakini anatualika kwa msaada wake, tusikate tamaa na kufanana na mawazo hayo, bali kuendelea kutenda wema wetu na kwa wote, hata kwa yule anayeteseka. Anatualika tusijibu kwa nguvu na kulipiza visasi, bali kubaki waaminifu katika ukweli. Mashahidi wanatupatia ushuhuda wa kumwaga damu kwa imani, hata sisi, katika muktadha na katika namna tofauti tunaweza kuiga mfano.

Waamini huko Castel Gandolfo
Waamini huko Castel Gandolfo   (@VATICAN MEDIA)

Kwa kutoa mifano hai, Papa alisema "Tunaweza kwa mfano, katika gharama ambayo lazima kulipa kwa mzazi mzuri, ikiwa unataka kuelimisha vizuri watoto, kwa mujibu wa misingi mizuri kwani: mapema au baadaye ujue namna ya kusema hapana, kusahihisha na kwa hiyo itamgharimu mateso. Na hiyo ni sawa na walimu ambao wanatamani kufunda kwa usahihi wanafunzi wao, kwa ajili ya utaalaamu, mtawa, mwanasiasi, ambaye wanapendekeza kujikita katika utume kwa uaminifu na kwa kila mmoja, anajibidisha kutenda kwa uangalifu kwa mujibu wa mafundisho ya Injili na uwajibikaji wake."

Sala ya Malaika wa Bwana huko Cstel Gandolfo
Sala ya Malaika wa Bwana huko Cstel Gandolfo   (@VATICAN MEDIA)

Papa Leo XIV kwa kukazia zaidi alisema: “Mtakatifu Ignatius wa Antiokia, katika muktadha huo wakati alikuwa safarini kuelekea Roma, mahali ambapo angekumbana na kifodini, aliwaandikia Wakristo wa mji huu: “ Sitaki ninyi mkubaliwe na watu, bali na Mungu (Rm 2,1) na aliongeza: “ Ni vizuri kwangu kufa kwa ajili ya Yesu Kristo zaidi, badala ya kutawala hadi miisho ya dunia”(Rm 6,1). Kwa njia hiyo Papa Leo kwa kuhitimisha alisema “Tuombae pamoja na Maria, Malkia wa Mashahidi, atusaidie kuwa kwa kila muktadha, mashuhuda waaminifu, na wajasiri wa Mwanae, na kuwasaidia kaka na dada ambao leo hii wanateseka kwa ajili ya imani.”

Papa kabla ya Angelus, Agosti 17
17 Agosti 2025, 12:30