杏MAP导航

Tafuta

Papa Leo XIV,misa Albano,Agosti 17:Tuangushe kuta,kila mmoja ni zawadi kwa mwingine!

Misa inamwilisha uamuzi ambao huwezi kuishi kibinafsi tena,wa kupeleka moto katika ulimwengu.Sio moto wa silaha wala wa maneno yanayochoma wengine.Hapana.Ni moto wa upendo unaoinamana kuhudumia,unapopingana na sintofahamu ya utunzaji na kuleta upole juu ya kiburi;moto wa wema,usio na gharama kama silaha,wa bure unaopyaisha dunia.Unaweza kuwa wa gharama ya kutoeleweka,dhiaka,hadi kuteswa,lakini hakuna amani kubwa zaidi ya kuishi ndani ya moto wake.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV, katika Dominika ya 20 ya mwaka C wa kawaida, tarehe 17 Agosti 2025 aliongoza Ibada ya Misa Takatifu katika Madhabahu ya Bikira Maria wa Rotonda, na Maskini, wanaohudumiwa na Jimbo la Albano pamoja na wahudumu wa Caritas Jimbo. Kwa kuongoza na Injili ya Siku kutoka Luka 12,49 -53 inayojikita na mada ya moto unaotupwa duniani na Yesu, Baba Mtakatifu Leo alianza kusema kuwa: “Ni furaha kukutana pamoja na kuadhimisha Ekaristi ya Dominika ambayo inatuzawadia furaha tena ya kina zaidi. Ikiwa kiukweli tayari ni zawadi ya kuwa karibu na kushinda umbali wa kutazamana machoni, kama kaka na dada wa kweli, kikubwa zaidi ni katika Bwana  kishinda kifo. Yesu alishinda kifo, Dominika ni siku yake, Siku ya Ufufuko na sisi tunaanza tayari kushinda naye.

Misa ya papa na maskini wa Jimbo la Albano
Misa ya papa na maskini wa Jimbo la Albano   (@VATICAN MEDIA)

Ni hivyo: kila mmoja wetu anakuja Kanisani na uchovu flani na hofu, wakati mwingine kidogo sana, na wakati mwingine kubwa zaidi, na mara moja tunajikuta hatuko peke yetu, tuko pamoja na kupata Neno na Mwili wa Kristo. Kwa namna hiyo mioyo yetu inapokea maisha ambayo yanakwenda mbali  zaidi ya kifo. Ni Roho Mtakatifu, roho wa Mfufuka, anaye fanya hayo kati yetu na ndani yetu, kwa ukimya, Dominika baada ya dominika na siku baada ya siku. Papa Leo XIV aliendelea kusema, “Tunajikuta katika Madhabahu ya zamani, mahali ambapo  kuta zinatukumbatia. Yanaitwa “Rotonda”(yaani Mzunguko, na mtindo wa mzunguko, kama ulivyo Uwanja wa Mtakatifu Petro na kama kila makanisa mengine ya kizamani na mapya, yanatufanya kuhisi kukaribishwa katika umbu la Mungu. Ukiwa nje ya Kanisa, kama kila hali halisi ya binadamu, linaweza kuonesha kwetu kuwa kali (spigolosa). Hali halisi yake ya kimungu, lakini linajionesha wakati tunavuka kizingiti chake na kukutana na makaribisho.

Baba Mtakatifu alisema kwa hiyo umaskini wetu, udhaifu wetu na hasa kushindwa ambako tunaweza kudharauliwa na kuhukumiwa, na wakati mwingie sisi wenyewe kujidharau, na kujihukumu, hatimaye vinakaribishwa katika utamu wa nguvu ya Mungu, katika upendo bila ukali, na upendo bila masharti. Maria, Mama wa Yesu kwa ajili yetu ni ishara na mwanzilishi wa umama wa Mungu. Katika Yeye tunakuwa Kanisa Mama, ambalo linazaa na kuzaa si kwa uwezo wa nguvu za kidunia, bali kwa fadhila za upendo. Papa alikazia kusema kuwa “ Inawezakana labda kutushangaza kwamba, katika Injili iliyosomwa, ile ambayo Yesu anasema:  “Sisi tunatafuta amani na tulisikiliza: Je! Mwadhani ya kwamba nimekuja kuleta amani duniani? Nawaambia, La, sivyo, bali mafarakano(Lk 12,51). Na karibu tungeweza kumjibu “ kwa jinsi gani Bwana? Hata wewe? Tayari tuna mifarakano mingi. Siyo wewe uliyesema wakati wa karamu kuu kwamba: “Ninawaachia amani, ninawapa amani yangu?” “Ndiyo, Bwana anaweza kutujibu  kwamba: ‘Ni mimi.’ Kumbukeni kwamba usiku ule  katika karamu yake ya mwisho aliongeza kwa haraka katika muktadha wa amani kwamba: “ amani niwapayo mimi, si kama ulimwengu utoavyo. Msifadhiake mioyoni mwenu na wala msiogope (Rej. Yh 14,27).

Misa na maskini huko Madhabahu ya Maria wa Rotonda, Albano
Misa na maskini huko Madhabahu ya Maria wa Rotonda, Albano   (@VATICAN MEDIA)

Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu Leo XIV aliendele kusema, dunia  inatufanya tuzoee kubadilisha amani, faraja, wema kwa utulivu. Kwa njia hiyo ili amani iweze kuja katikati yetu, amani ya Mungu, Yesu anapaswa kutueleza: “Nimekuja kutupa moto duniani; na ukiwa umekwisha washwa, ni nini nitakalo zaidi?!” (Lk 12,49). Labda wanafamilia wetu wenyewe, kama Injili ilivyosema, na hadi kufikia marafiki, watafarakana juu ya hilo. Na mmojawapo atatuambia tusithubutu, kujisalimisha, kwa sababu ni vema kakaa watulivu na wengine hawastahili kupendwa. Yesu kinyume chake aliingia katikati ya ubinadamu wetu na ujasiri. Na ndiyo tazama “ubatizo” ambao anazungumza (Lk 12,50) ni ubatizo wa msalaba wa kujiingiza kabisa katika hatari ambayo inayopelekea   upendo. Na sisi kama wasemavyo kwamba tunapokomunika, tunamwilishwa zawadi yake hiyo ya ujasiri. Misa inamwilisha uamuzi huu. Ni uamuzi ambao huwezi kuishi  kibinafsi tena, wa kupeleka moto katika ulimwengu.

Papa aliongoza Misa ya Makini huko Madhabahu ya Maria wa Rotonda,
Papa aliongoza Misa ya Makini huko Madhabahu ya Maria wa Rotonda,   (@Vatican Media)

"Sio moto wa silaha, Papa aliongeza - na wala ule wa maneno yanayochoma wengine. Hiyo hapana. Lakini ni moto wa upendo ambao unainama, na kuhudumia, unapopingana na sintofahamu ya utunzaji na kuleta upole juu ya kiburi; moto wa wema, ambao hauna gharama kama silaha,  bali  wa bure unaopyaisha dunia. Inawezeka kuwa na gharama ya kutoeleweka, dhiaka, hadi kuteswa, lakini hakuna amani  kubwa zaidi ya  kuishi ndani ya moto wake. Papa Leo XIV,  kwa hiyo, alipenda kumshukuru Askofu  wao pamoja na wote ambao katika Jimbo la Albano wanajitahidi kupeleka moto wa upendo. Na anawatia moyo wa kutotofautisha kati ya anayehudumia na anayehudumiwa, kati ya wale wanaofikiriwa kutoa na wale ambao utadhani wanapokea, wale wanaonekana masikini  na wale wanahisi kutoa muda wao, uwezo wao na msaada. Wote ni Kanisa la Bwana, Kanisa la Maskini   na wote ni wa thamani, wote kila mmoja mbebaji wa Neno pekee la Mungu. Kila mmoja ni zawadi kwa ajili ya wengine. Papa aliomba“kuangusha kuta.” Ameshukuru anayetoa huduma kwa kila jumuiya ya kikristo ili kurahisha kukutana kati ya watu tofauti kutoka maeneo mbali mbali, kwa hali halisi ya kiuchumi, kimwili, upendo, na ni kwa pamoja, inawezekana kugeuka mwili mmoja tu ambao hata walio wadhaifu  wanashiriki kikamilifu, hadhi, na ni mwili wa Kristo, na wa Kanisa la Mungu.

Wakati wa kupokelewa
Wakati wa kupokelewa   (@VATICAN MEDIA)

Haya yanakuja pale ambapo Moto ambao Yesu alikuja kuleta  unachoma hukumu, busara na hofu ambazo bado zipo kwa anayekuja na umaskini wa Kristo katika historia. Tusiache nje Bwana katika makanisa yetu, katika nyumba zetu na katika maisha yetu. Katika maskini, kinyume chake tuache waingie na kufanya amani hata kwa umaskini wetu, ule ambao tunafikiria na kukataa tunapotafuta kila njia ya kujituliza na usalama. Kwa kuhitimisha Papa Leo XIV  alisema atuombee  Bikira Maria ambaye anasikika akielekezwa na Mtakatifu Simoni kwa Mwane Yesu kama “Ishara ya mafakano… (Lk 2,34). Mawazo ya mioyo yetu yaweze kuoneshwa, na moto wa Roho Mtakatifu uweze kufanya mioyo kuwa ya nyama na siyo mawe. Mtakatifu Maria wa Rotonda utuombee!

Mahubiri ya Papa Leo 17 Agosti 2025
17 Agosti 2025, 11:30