Papa Leo XIV,Sherehe ya Maria Mpalizwa:Ni wenyeheri wanaoona yasiyoonekana!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Katika Mahubiri ya Misa Takatifu ya Baba Mtakatifu Leo XIV, wakati Mama Kanisa anafanya Sherehe ya Bikira Maria Mpalizwa Mbinguni, tarehe 15 Agosti 2025, iliyofanyika katika Parokia ya Mtakatifu Thomas huko Vilanova, Castel Gandolfo, alianza kusema kuwa: “leo sio Dominika, lakini kwa namna tofauti, tuanaadhimisha Pasaka ya Yesu ambaye anabadilisha Historia. Kwa Maria wa Nazareth, kuna historia yetu, historia ya Kanisa iliyondani ya umoja wa ubinadamu. Kwa kufanyika mwili ndani yake, Mungu wa maisha, Mungu wa uhuru alishinda kifo. Ndiyo Leo tunatafakari jinsi ambavyo Mungu alishinda kifo, lakini kamwe bila kuwa na sisi. Ufalme ni wake, lakini wa kwetu ni ‘ndiyo’ ya upendo wake ambao kila kitu kinaweza kubadilika. Juu ya Msalaba, Yesu kwa uhuru wake alitangaza ‘ndiyo? Ambayo ilikuwa inaondoa uwezo wote wa kifo, kifo kile ambacho bado kimesambaa wakati mikono yetu inayosulibisha na mioyo yetu iliyofungwa na hofu na kutokuaminiana. Juu ya Msalaba imani ilishinda, upendo ulishinda unaotazama kile ambacho bado hakipo, na ulishinda. Baba Mtakatifu aliendelea kueleza kuwa na Maria alikuwa hapo, ameungana na Mwanae. Leo hii tunaweza kutambua kwamba Maria ni sisi, ikiwa hatukimbii, ikiwa sisi tunajibu tazama mimi hapa katika ndiyo yake. Katika mashahidi wa wakati wetu, katika mashuhuda wa imani na wa haki, wa unyenyekevu na wa amani, ile ndiyo, inaishi bado na bado inaweza kupinga kifo. Kwa njia hiyo siku hii ya furaha, ni siku ambayo inatuwajibisha, kuchagua namna gani ya kuishi, na kwa ajili ya nani.
Lituruji ya sherehe hii ya kupalizwa mbinguni inapendekeza neno la Injili la Bikira kumtembelea Elizabeti(…) Mtakatifu Luka, anaonesha sura hii ya kumbukumbu kwa wakati mgumu wa wito wa Maria. Ni vizuri kurudi katika wakati ule, siku ambayo tunaadhimisha mtazamo wa uwepo wake. Kila historia, hata ile ya Mama wa Mungu duniani ni fupi na inaisha. Lakini hakuna lolote linalopotea. Na hivi wakati maisha yanapofungwa , upekee wake unaang’aa zaidi. Wimbo wa Sifa, ambao Injili inapendekeza katika mdomo wa kijana Maria, sasa unafunguliwa nuru katika siku zake zote. Siku moja ile ya kukutana na binadamu yake Elizabetu, inafungamanisha siri ya siku nyingine ya kila kipindi. Na maneno hayatoshi, inafaa wimbo, ambao katika Kanisa unaendelea kuwa wito wa kizazi hadi kizazi (Lk1,50), mawio ya jua ya kila siku. Matunda ya kushangaza, ya utasa wa Elizabeti, ulithibitisha Maria imani yake: ulitanguliza matunda ya mwitikio wake wa “tazama mimi hapa” ambao unaendelezwa na matunda ya muda mrefu ya Kanisa, na ubinadamu mzima, unapokuwa kribu na neno linalopyaishwa na Mungu. Siku ile wanawake wawili, walikutana katika imani na baadaye wakabaki miezi mitatu pamoja wakisaidiana, si katika matendo , lakini namna mpya ya kujua historia.
Baba Mtakatifu Leo XIV alisisitiza kuwa “ ufufuko inaingia hata leo katika dunia yetu. Maneno na chaguzi za kifo utafikiri yanashinda, lakini maisha ya Mungu yanakatisha mahangaika kwa njia ya dhati, uzoefu wa udugu, kwa njia za ishara mpya za mshikamani, kabla ya kuwa hatima yetu ya mwisho, kiukweli, Ufufuko unasasisha, roho na mwili, kuishi kwetu duniani. Wimbo wa Maria, wa Sifa kwa Bwana, unaongeza nguvu ya matumaini kwa wanyenyekevu, wenye njaa, na watumishi wa Mungu. Ni wanawake na wanaume wa heri, ambao bado wapo katika mahangaiko wanaona tayari yasiyoonekana: wenye nguvu kuanguka kwenye viti vyao,, matajiri kuwa mikono mitupu, ahadi za Mungu kutimizwa. Huu ni uzoefu ambao kila jumuiya ya kikristo, lazima wote tuweza kusema tumeishi. Inaonekana haiwezekani, lakini kwa Neno la Mungu bado inajitokeza katika nuru. Ni pale panapozaliwa uhusiano na kile ambacho tupinga ubaya kwa wema, kifo kwa maisha, hapo tunaona kuwa “hakuna kisichowezekana kwa Mungu”(LK 1,37).
Baba Mtakatifu aidha alisema wakati mwingine kwa bahati mbaya, uhakika wa kibinadamu unashinda,kwa namna ya ustawi wa mali na ule wa kupumzika, ambao unafanya kusinzia dhamiri,na imani hiyo inaweza kuzeeka. Kwa hiyo kifo kinaingia, katika mitindo ya kushindwa, na kulalamika, kujutia na kukosa uhakika. Badala ya kuona ulimwengu unaishia kuzeeka, ni kutafuta bado msaada; msaada wa matajiri, wenye nguvu ambao kwa kawaidia wanasindikiza masikini kwa kudharau na walio wa mwisho. Lakini Kanisa linaishi katika viungo vya udhaifu wake, shukrani kwa wombo wa Sifa yao. Hata leo hii, Jumuiya za kikristo wako na maskini, na wanaoteseka, mashuhuda wa huruma na msamaha, katika maeneo ya migogoro, wahudumu wa amani na wajenzi wa madaraja, katika ulimwengu uligawanyika vipande, ni furaha ya Kanisa, na ndiyo matunda yake ya kudumu, Ufalme wa kwanza unaokuja. Wengi wao ni wanawake, kama vile Mzee Elizabeti na kijana Maria: Wanawake wa Pasaka, mitume wa Ufufuko. Tuache tuongoke kwa sababu ya ushuhuda wao!
Papa Leo XIV akirejea somo la Kwanza alisema kwamba “iwapo katika maisha haya tunachagua maisha(Dt,30,19, basi Narua, aliyepalizwa Mbingi, tunasababu ya kuona hatima yetu. Yeye alijitoa kama ishara ambayo Ufufuko wa Yesu hakuwa kitu kilichojienga, cha kipee. Wote katika Krito, tunaweza kumezwa na kifo (1Kor 15,54). Hakina ni kazi ya Mungu na siyo yetu. Hata hivyo Maria katika msuko huo wa neema na uhuru unaotusikua kila mmoja wetu katika imani, ujasiri, anatuhusisha katika maisha ya watu. Mwenyezi amenitendea mamo Makuu,(Lk 1,49): anaweza kufanya kila mmoja kufanya uzoefu wa furaha na kushuhudia kwa wimbo mpya. Tusiwe na hofu ya kuchagua maisha; Inawezekana kuleta hatari, na kutokuwa na busara. Ni sauti ngapi daima tunazisikia: ni nani anakutuma ufanye? Hachana navyo! Waza mahitaji yako: Hizi ni sauti za kifo. Kinyume chake sisi tu mitume wa Kristo. Ni upendo wake ambao unatusukuma, miwli na roho katika wakati wetu. Kama binafsi na kama Kanisa sisi hatuishi kwa ajili yetu wenyewe. Ni tu ndiyo hasa, ya kuweza kusambaza maisha na kufanya maisha kushinda. Ushindi wetu juu ya kifo unaanzia hapo, Papa alihitimisha.